Habari zenu wana JF,Naomba ushauri wenu kwa hili tatizo linalonisibu kuhusu mpenzi wangu.Nina mpenzi ambaye tunatokea wote mkoa mmoja huko kanda ya ziwa,pia tulisoma wote shule ya msingi lakini tulianza mahusiano kipindi ambacho mimi nilikuwa namaliza mwaka wa mwisho chuo kikuu hapa DSM na yeye alikuwa mwaka mmoja nyuma yangu chuo kikuu mkoa mwingine ,Mahusiano yaliendelea na mimi baada ya kumaliza chuo nikafanikiwa kupata kazi hapahapa DSM na kuanza maisha hapa kwenye jiji la Bwana Meck Sadick,sasa baada ya mpenzi wangu kumaliza shule pia akaja DSM kuja kutafuta kazi na alifikia kwa ndugu yake (Aunt yake)sasa tatizo lake kubwa lililonifanya niwashirikishe ndugu zangu ni kwamba mpenzi wangu huyu ana tabia kubwa ya uongo,yaani kudanganya watu wengine wanaomzunguka na hata marafiki na ndugu zangu mimi,yaani ukitaka kujua yeye anatokea wapi basi hata siku moja hatakutajia nyumbani kwao yaani mkoani kwao zaidi ya kukuambia hapa DSM na kila siku atakutajia mitaa tofauti,pia hata baada ya kumaliza chuo huko mkoani alirudi kwao na kukaa siku tatu tu toka hapo hajawahi kwenda tena na mie nimesharudi zaidi ya mara 10,Pia huyu Aunt yake anayekaa naye hapa DSM ndio anawatambulisha watu kama mama yake mzazi.Hata akiulizwa kabila lake basi anataja kabila linguine kabisa na hata Sir name pia hataji ya kwake na anataja nyingine.pia toka amekuja dsm ni mwaka wa tatu sasa hajafanikiwa kupata kazi lakini anapokutana na mtu yeyote wa karibu basi atadanganya kwa kusema anafanya kazi na kila siku atakutajia makampuni tofauti,nimejaribu mara kadhaa kumwambia na kumuuliza kwa nini ana tabia ya kusema uongo lakini hakuna jibu la maana analosema,sasa kikubwa last wiki alikutana na rafiki yangu ambaye tumepotezana kwa siku nyingi basi akamdanganya vitu vingi sana.Kusema kweli mimi nampenda sababu ukiacha hilo kuku tabia zingine zote yuko safi tu na pia nilikuwa na mpango siku ya mwisho ndio awe mama watoto,sasa wana JF naomba ushauri mtu kama huyu unamfanyaje aache kuongopa na kujikweza?,au nimfanyaje maana mie tabia hii inanikera na siipendi hata kidogo......