Mpenzi wangu ana tabia ya uongo na hakutaki kwao

Mpenzi wangu ana tabia ya uongo na hakutaki kwao

BongeMwepesi

Senior Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
125
Reaction score
83
Habari zenu wana JF,Naomba ushauri wenu kwa hili tatizo linalonisibu kuhusu mpenzi wangu.Nina mpenzi ambaye tunatokea wote mkoa mmoja huko kanda ya ziwa,pia tulisoma wote shule ya msingi lakini tulianza mahusiano kipindi ambacho mimi nilikuwa namaliza mwaka wa mwisho chuo kikuu hapa DSM na yeye alikuwa mwaka mmoja nyuma yangu chuo kikuu mkoa mwingine ,Mahusiano yaliendelea na mimi baada ya kumaliza chuo nikafanikiwa kupata kazi hapahapa DSM na kuanza maisha hapa kwenye jiji la Bwana Meck Sadick,sasa baada ya mpenzi wangu kumaliza shule pia akaja DSM kuja kutafuta kazi na alifikia kwa ndugu yake (Aunt yake)sasa tatizo lake kubwa lililonifanya niwashirikishe ndugu zangu ni kwamba mpenzi wangu huyu ana tabia kubwa ya uongo,yaani kudanganya watu wengine wanaomzunguka na hata marafiki na ndugu zangu mimi,yaani ukitaka kujua yeye anatokea wapi basi hata siku moja hatakutajia nyumbani kwao yaani mkoani kwao zaidi ya kukuambia hapa DSM na kila siku atakutajia mitaa tofauti,pia hata baada ya kumaliza chuo huko mkoani alirudi kwao na kukaa siku tatu tu toka hapo hajawahi kwenda tena na mie nimesharudi zaidi ya mara 10,Pia huyu Aunt yake anayekaa naye hapa DSM ndio anawatambulisha watu kama mama yake mzazi.Hata akiulizwa kabila lake basi anataja kabila linguine kabisa na hata Sir name pia hataji ya kwake na anataja nyingine.pia toka amekuja dsm ni mwaka wa tatu sasa hajafanikiwa kupata kazi lakini anapokutana na mtu yeyote wa karibu basi atadanganya kwa kusema anafanya kazi na kila siku atakutajia makampuni tofauti,nimejaribu mara kadhaa kumwambia na kumuuliza kwa nini ana tabia ya kusema uongo lakini hakuna jibu la maana analosema,sasa kikubwa last wiki alikutana na rafiki yangu ambaye tumepotezana kwa siku nyingi basi akamdanganya vitu vingi sana.Kusema kweli mimi nampenda sababu ukiacha hilo kuku tabia zingine zote yuko safi tu na pia nilikuwa na mpango siku ya mwisho ndio awe mama watoto,sasa wana JF naomba ushauri mtu kama huyu unamfanyaje aache kuongopa na kujikweza?,au nimfanyaje maana mie tabia hii inanikera na siipendi hata kidogo......
 
Anapenda kujikwezaa na showoff!!!!!!!!!!! Kuonekana matawi ya juu na sifa za kijinga!
 
Ninyi ni waumini wa imani gani?
 
Mh hivi watu wa aina hio bado wapo anataka makubwa kuliko alokuwa nayo!Inamaana hajithamini yeye kwa jinsi yeye alivyo na ni hulka mbaya mno,mtu lazima uridhike na maisha na utu wako.Hiko kitu kinarekebishika ni maelewano tu,ongea nae mwambie kama habadiliki huwezi kuwa nae!
 
mh huyu ataleta majambazi ndani kwa mdomo wake wa makuuuu
 
Huwa kanisani hakuna kitu kama counselling hivi?
Kwangu mimi hilo tatizo has to be dealt spiritually...
Halitaisha hivi hivi na ukiiacha tatizo hili liendelee huenda likawapa shida mbeleni.
Mkuu asante sana nitafanya hivyo.
 
Daaaah kaz ipo hapo......ndo hao wanasemaga wanaishi masaki ila kipind cha mafuriko wameonekana juu ya bati jangwani!!!!!
 
Huyo anaugonjwa unaoitwa ---Mkataa kwao sio mtumwa---- matibabu yake usimzoeshe kutembelea sehem kama Mlimani city au Posta na Quality center na badala yake jaribu kufanya ziara za mara kwa mara manzese na ukipata muda mpeleke mikumi akaone tumbili baada ya mwaka mkatembee mwanza naamini atapona
 
Dah nakusikitikia sababu kuna tabia zingne za binadamu kama unaroho nyepesi huwezi kuzivumilia! Kiukweli tabia ya UONGO inakera sana hata kama ni kwarafik wakawaida INAKERA mno.nimeshawah kuwa na rafiki wa namna hiyo best friend nilimuonya sana but hakubadilika nikaamua kumpotezea,yaani kibaya zaid alikuwa anamdanganya hadi mpenzi wake ambaye alikuwa na malengo naye kama huyo dada mwisho wa cku bwana yule baada ya kugundua anadanganywa akaamua kuachana naye.so watchout broo tabia zingine ni kama ngozi hazivuliki kama unaona ni kero na itaweza athiri future yako/yenu ni better kustay away from her.
 
Dah nakusikitikia sababu kuna tabia zingne za binadamu kama unaroho nyepesi huwezi kuzivumilia! Kiukweli tabia ya UONGO inakera sana hata kama ni kwarafik wakawaida INAKERA mno.nimeshawah kuwa na rafiki wa namna hiyo best friend nilimuonya sana but hakubadilika nikaamua kumpotezea,yaani kibaya zaid alikuwa anamdanganya hadi mpenzi wake ambaye alikuwa na malengo naye kama huyo dada mwisho wa cku bwana yule baada ya kugundua anadanganywa akaamua kuachana naye.so watchout broo tabia zingine ni kama ngozi hazivuliki kama unaona ni kero na itaweza athiri future yako/yenu ni better kustay away from her.
Asante kwa ushauri na kwa mda niliomjua mpaka sasa bado anaendeleza uongo regardless kusema ataacha,Hapa naamini kweli tabia kama ngozi ya mwili
 
usijali bado anakua,ana utoto.
 
Back
Top Bottom