Mpenzi wangu ameanza kunywa pombe

Tulipokuwa wadogo mama jirani yetu alikuwa anapiga tungi si mchezo, mume wake alikuwa kubosile, mama akitoka job anaingia baa anaupiga mpaka wahudumu wana Mpigia mzee simu dereva anatumwa akamchukue mama. Kabla ya hapo hawajui yuko baa gani.
 
Aisee kama ni kweli basi pole sana. Na ninahisi Kuna watu wanamdanganya aachane na wewe kwa njia ya pombe. Na sijui sababu za yeye pia kutaka umuache. Ila mwisho Wa watu Wa aina hiyo huwa ni majuto na kukukumbuka. Na kama ni serious issue ameanza kunywa hivyo basi kaa uongee nae kwa kina sana juu ya mlikotoka,ulivyomchukulia na sasa unavyojisikia. Akishindwa kuacha shirikisha ndugu zake Wa karibu anaowaheshimu sana. Ikishindikana hapo shirikisha wazazi/walezi wake. Ikishindikana hapo achana nae kwa sababu mwanamke anaekunywa pombe tena kibaya mumewe hanywi pombe ni vigumu sana sana sana sana au haiwezekani kujisimamia,hivyo atageuka kuwa ni mwanamke rahisi sana kufanya mapenzi nje ya ndoa yake tena na wanaume wengi wengi.
 
niachie mimi uyo dem, au akiwa anataka kwenda bar nambie niwe nampitia, ntakua nakulindia bwana mlokole, japo nawe niombee shetani asinipitie nikapita nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…