Mpenzi wangu alinidanganya kuwa yule ni ‘Bestfriend’ kumbe ni zaidi

Doppelganger

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,858
748
Habari ndugu,

Napenda kueleza kisa kimoja kiliwahi kunitokea enzi bado nina mihangaiko mingi katika mahusiano. Kisa chenyewe kilikuwa kama ifuatavyo;

Nilibahatika kupata ajira kwenye Taasisi moja binafsi miaka kama 10 iliyopita. Kwa wakati huo nilikuwa bado naishi nyumbani, hivyo nilikuwa na nafasi kubwa sana ya kutunza pesa kwa ajili ya matumizi yangu mengine ikiwa ni pamoja na starehe.

Sasa, pale ofisini kwetu kulikuwa na mabinti wawili ambao walikuja kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo, ambao wao niliwakuta wakati mimi naanza kazi.

Kimsingi nilijitahidi sana kuwa nadhifu kuanzia mavazi hadi uchapa kazi, hivyo niliweza kujenga umaarufu na kupata sifa mbalimbali katika kazi na mahusiano baina ya wathmishi wengine.

Sasa, kama ujuavyo wanaume wengi tukishazoea sehemu zenye wadada, tunajikuta kuanza kujipenyeza kwenye mahusiano taratibu hata kama sio moja kwa moja. Ndivyo ilivyonitokea nikazama kwa mtoto wa field.

Kisa: Baada ya kuwa katika mahusiano na yule binti, tuliongea mengi na alitambulisha kwa marafiki zake, ambao alinitajia kwa majina, kati ya hao alitaha jina la kijana wa kiume.

Niliposikia jina la kiume, nilimhoji kwa kina kwanini alikuwa na urafiki na yule kijana wakati mimi ndiye mpenzi wake (nilikuwa na wivu sana). Dada akanijibu kuwa yule hakuwa mwanaume kamili, bali alikuwa ni kama yeye (mwanamke) na walisoma naye sekondari na kwamba alkmwonea huruma kwa sababu marafiki walimtemga kwasababu ya tabia za upunga, hivyo alinithibitishia kuwa hakuwa na madhara.

Binafsi, sikumwamini sana mpenzi wangu nikaamua kumfatilia yule kijana niliyeambiwa kuwa ni 'punga' niligundua alikuwa na tabia za kike naalishinda sana na watoto wa kike, japo sikuthibitisha.

Ikawa kila nilipotofautiana na mpenzi wangu, basi alikuwa anakimbilia kwa yule kijana (niliyeambiwa kuwa ni punga), nami nili-relax maana nilikuwa nina uhuru na girlfriend wangu wakati wote hata akiwa kule kwa yule kijana.

Tuluendelea na mahusiano yetu bila kuwa na tatizo kwa takribani mwaka na nusu hivi. Siku moja, girlfriend wangu aliniambia kwamba alienda nyumbani kwa yule kijana (best friend wake), kwa hiyo nikiwa narudi nyumbani nimpitie ili turudi pamoja. Alinijulisha pia kuwa simu yake ingezima kutokana na kuwa na asilimia kidogo za chaji maana umeme ulikuwa umekatika, hivyo akanipa namba ya binti mwingine waliyekuwa naye pale nyumbani kwa yule kijana.

Siku ile nilienda nikamchukua girlfriend wangu tukaenda nyumbani na maisha yaliendelea sawia. Ikawa sasa yule dada mwenye ile namba niliyopewa kuwasiliana naye wakati simu ya mpenzi wangu imezima aliendeleza mazoea ya kuwasiliana na mimi na alijitambulisha kwangu kuwa yeye alikuwa ni mpenzi wa yule kaka ambaye nilitambulishwa kuwa ni punga.

Na katikati ku-chat aliniambia kwamba alihisi kwamba jamaa yake (punga) alikuwa na mahusiano ya kkmapenzi na girlfriend wangu na alinipa baadhi ya vielelezo kuthibitisha maelezo yake, mfano picha wakiwa watupu pamoja, picha ambazo punga alimpiga girlfriend wangu kiwa mtupu kabisa n.k.

Of course, kuona vile nami ikabidi nijiongeze kwake ili nipungize hasira (japo hasira haikupungua, nilijiona mjinga zaidi).

Niliamua kumwambia girlfriend wangu niliyafahamu na kumhoji maana nilikuwa tayati nina ushahidi, ndipo alikiri kwamba jamaa hakuwa punga, na yule dada kweli ni girlfriend wa punga. Kwamba kama asingesema vile (kuwa jamaa punga) nisingempa uhuru wa kuwa naye.

Nilikata gamaa kabisa, na tangu siku ile sikuamini tena u-bestfriend kati ma mvulana na mpenzi wangu.
 
Hapo unajifanya kumtongoza na huyo jamaa, aking'aka unamuambia mbona uliambiwa na demu wako kwamba yeye ni choko, ili uwafurahishe zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilimwambia jamaa, na akaknekana kuwa sawa tu.

Nadhani kuna wanaume wanatumia ukaribu wa wanawake ili kuwalaghai na kuwapitia bila kuwahudumia.

Kwa maana yule jamaa 24hrs utamwona na wadada tu. Instagram yake hata sasa yeye na wadada "BFF" nyingi, namwangalia tu!!

Mpaka sasa yupo na style hake ile ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom