The Humble Dreamer
JF-Expert Member
- Oct 12, 2015
- 8,011
- 11,429
Wakuu Salaam;
Kila mmoja hupitia mambo kadhaa katika mahusiano na mojawapo ni hili la mahusiano kuvunjika kwasababu mbalimbali.
Binafsi Mpenzi wangu wa kwanza tuliachana kwasababu kadhaa baada ya yeye kumaliza kidato cha sita na mimi kwenda Chuo. Alikua akisoma huo ukanda ulipo mkoa wa Dar Kwa upande wa elimu ya sekondari ngazi ya A level.
Baadaye alichaguliwa kwenda Chuo morogoro maana aliniambia hadi fani aliyochaguliwa kwenda kusoma. Kwa kipindi tulichoachana hakukua na mawasiliano ya karibu tena.
Mwaka huu 2020 niliambiwa na rafiki yake kwa sasa yuko Dar na ameajiriwa na kampuni moja hivi kwenye kitengo kizuri tu. Kuna Nickname alikua akiipenda sana nimwite hivyo nimemtafuta instagram nimempata na kuona picha zake. Binafsi nimeshawishika sana kurudiana naye sema kwa sasa haiwezekani maana tayari kaolewa na ana watoto watatu.
Mme wake ana kazi ya kawaida tu hapo mjini ila huyo dada ndiyo ana kazi nzuri.
Niko nabungaa tu sahivi, sijajaribu hata kumtafuta kupitia instagram nimsalimie zaidi ya kucheki posts zake. Kuna siku niliona kaposti yuko na mmewe na watoto wao, nilikula kwa macho tuu.
Wakati mwingine naona posts yuko kwenye seminars, vikao mbalimbali n.k
Huenda tungekua mbali kimaisha kama tungekua pamoja. Nalolitambua ni kua kwenye maisha hamna haja ya kulalamika au kuhuzunika. Ni kuchukua ustaarabu tu.
Vipi upande wako, unafahamu alipo mpenzi wako wa kwanza kwa sasa na ungetamani kurudiana naye?