Mpenzi kajilisha nyama ya kitimoto kinyume na Imani

mwanzo wetu

JF-Expert Member
May 4, 2014
1,581
461
Jamani naombeni ushauri demu wangu alikuja jana Geto ,kimsingi mimi ni mkristo na Yeye ni mwislamu, Mimi natabia ya kununua kilo ya nguruwe na kuitengeneza mwenyewe nyumban kutokana sipendi itengenezwe magengeni au mtaani nje na nyumbani.

Sasa mimi huwa mafuta yanayobaki huwa nayatunza ktk chupa ili nikinunua nianzie pia kupika.

Jana alikuja nikatulia nae geto baadae nikamuacha home mimi nikaenda ofisini bt akahis njaaa akachukua mchele akapika na akapikia yale mafuta ya kitimoto akijua ni korie pengine na aka kaangia mboga.

Nilipofika wakati huo alikuwa ameshaondoka kwake ila mafuta yale ya kitimoto yakawa yote yametumika na chakula amekula. Sasa nishauri jamani nimwambie akatubu msikitini au nitulie maana tayari nimemlisha haramu.
 
Kausha..✌️😂😂

Ila mkuu ukidate na mtu wa iman tofauti jitahidi vitu kama hivyo ukaloe huko huko mbali. Wengine wana mashetani hata vyombo tu ni havifai yeye kutumia.
 
Kama ameweza kuzini unadhani kula mafuta ya kitimoto kuna tofauti gani na kuzini? Maaana vyote haramu hivyo .

Sjui huwa watu wanapima uharamu kivipi unakuta mtu hali nguruwe ila haramu nyengine zoote anafanya ! Ni huwa tunatumia nini kufikiria?
 
Kama ameweza kuzini unadhani kula mafuta ya kitimoto kuna tofauti gani na kuzini? Maaana vyote haramu hivyo .

Sjui huwa watu wanapima uharamu kivipi unakuta mtu hali nguruwe ila haramu nyengine zoote anafanya ! Ni huwa tunatumia nini kufikiria?
Hilo Tendo siyo kama kula ngurwe mkuu kwa iman zao duh👏
 
Dah hapo kwenye kinyume nilishaanza kuwaza ujinga,anyway sio mbaya maana unaweza uaile kitimoto alafu ukawa mzinifu
 
Mkuu umechelewa sana kujua , kwanini kipindi cha mfungo flani biashara ya kitimoto inashuka?
 
Back
Top Bottom