Habari wana Jf. Mimi nina miaka 33 nina mtoto wa miaka miwili na nusu. Baba wa mtoto nilipozaa mtoto tuliendelea na mahusiano nilimsihi aende kwetu hakwenda nikaamua niachane nae kwa sababu niliona anadharau wazazi wangu kwa kutokwenda nyumbani. Mwaka huu katika mawasiliano na mpenzi wangu wa zamani tukaanza mahusiano ila anataka nibebe mimba ndio aende kwetu. Na nyumbani hawataki nibebe mimba kabla mtu hajaenda. Anasema nampa masharti wakati niliezaa nae sikumpa masharti ya kwenda kwetu kabla ya kunipa ujauzito. Naombeni Ushauri hapa kuna muoaji kweli au anataka alipize kisasi. Nahisi kuchanganyikiwa.