Ukipata mtu anayekupenda kwa dhati kutoka moyoni, mpende pia na kumuonesha mapenzi ya dhati bila kumhukumu kutokana na historia yake ya nyuma kuwa alikuwa na nani na alifanya nini.
Huenda alikuwa vile kutokana na mtu aliekuwa naye kwa wakati ule pia hata aina ya marafiki aliokuwa nao, hivyo kumpima na kumhukumu kwa kutumia makosa ya zamani wakati alipokuwa kwa mtu mwingine ni kutomtendea haki kwani huwez jua kwanini alikuwa vile au alifanya yale kwa wakati ule
Pengine ni kutokana na maumivu aliyoyapata nyuma au huenda ilimlazimu kufanya yale kwa ajili ya mapenz wake wa wakati ule, usimkumbushe mambo yalivyopita na akayasahau.
Wewe anza ukurasa mpya kwake na kumfanya azidi kuyasahau yale huenda hata yeye yalikuwa yanamuumiza pia lakini hakuwa na jinsi.
Acha kuangalia historia yake huenda hata wewe itakuumiza bure wakati yale yalishapita na sasa hawezi kufanya tena yale mpende usimfanye akumbuke nyuma