Mpendazoe Kuzindua Kitabu Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpendazoe Kuzindua Kitabu Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dickson Ng'hily, Jun 4, 2011.

 1. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  ]Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mpendazoe, anatarajia kufanya uzinduzi wa kitabu chake alichokipa jina la 'TUTASHINDA'. Uzinduzi huoo unatarajia kufanyika Dodoma tarehe 12/06/2011 na Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ni Mh. F. Mbowe Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni. Pamoja na mambo mengine yahusuyo harakati za mapambano ya kumkomboa mnyonge, kitabu pia kinaelezea mchakato mzima wa uanzishwaji wa kilichokuwa Chama Cha Jamii (CCJ).
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi inawezekana Mpendazoe akawa anatimiza ajenda za Lowassa na sio CHADEMA? Wengi tunajuwa bifu kati ya Lowassa na Sitta/Mwakyembe. Je ni kweli Mpendazoe anakerwa na Sitta au antumia chadema kufanya kazi za mtu? ni maono yangu tuuuu...
   
 3. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  zama za mwisho za ukombozi hizi
   
 4. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  ...inshaalah, nakisubiri kwa hamu niusome kwa kina ili niujue uchumia tumbo wa Nape et. al.
   
 5. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  @FJM.....Mpendazoe ni mtu mzima hivyo mwulize yeye mwenyewe na bila shaka atakujibu....
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  tutampata wapi huyo mpenda zoe ili tumuulize? Hivi umefikiria kabla ya kujibu kweli? Na kwa nini umekuja kuandika hapa kuwa mpenda zoe anazindua kitabu? Mpendazoe si ni mtu mima si ungeacha aandike mwenyewe.
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Duh..maisha ya kisiasa ya Mpendazoe yanaelekea kuwa mafupi kuliko nilivyodhania, anazidi kujining'iniza mwenyewe kitanzini kwa kujionyesha jinsi alivyo mtupu..
   
 8. r

  raffiki Senior Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na we tutajuaje kama haujatumwa na Sitta na mwakyembe....!mwache kila mwanasiasa afanye mchangowake anavyoweza:shut-mouth:
   
 9. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #9
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  Mt.Ivunga...Sijui ni nini kimekuumiza kutokana na jibu nililotoa,bila shaka wewe pia ni mtu mzima labda nikuulize...Unaweza kuujua moyo wa mtu!Sasa swali lililoulizwa linahusu motive bila shaka haya ni mambo ya ndani ya mtu mwenyewe na ndo maana nikaseama aliulizwe yeye mimi siwezi kumjibia...Mpendazoe anapatikana sana labda uwe huna haja ya kumtafuta, hta ukienda pale Kinondoni Makao Makuu ya CDM anapatika tu wala sio adimu kiasi hiko.Kuhusu kitabu, nimeandika hapa kozi sio kitu kinachohusu motive ila ni kitu halisi na copy yake nimeiona na taarifa za uzinduzi ninazo, sasa dhambi yangu hapo ni ipi?Labda Mtakatifu unisaidie......
   
Loading...