Kwa kweli wana JF wenzangu na pia Watanzania wenzangu inasikitisha sana jinsi hatua waliyofikia CCM, si ya kuvumilika tena! Lakini inasikitisha sana kuona baadhi ya Watanzania hawana uchungu na nchi yao na maslahi ya nchi yao na ya Watanzania wenzao!
CCM kuendelea kuongoza nchi hii (kutokana na kupigiwa kura za ukweli na baadhi ya wana CCM na pamoja na uchakachuaji unaodaiwa na Dr Slaa na wana CHADEMA wenzake kufanywa na CCM) kuna tafsiri/implication kubwa. Tafsiri ya kuendelea kuongoza CCM ni kwamba:
-ufisadi utaendelea
-mikataba mibovu itaendelea,
-rushwa itaendelea n.k.
-na mwisho wake ni kuendelea kwa umaskini uliokithiri.
Lakini kubwa sana Watanzania tutakwazika! Tutakwazika kwasababu tutaendelea kuwa na hali ngumu za maisha, hivyo kulazimika kutumia njia mbadala ili tuweze ku-survive. With scarce and limited resources njia mbadala hizo mara nyingi huwa si za halali. Kwa mfano watu mishahara inapokuwa haitoshi maofisini watu watalazimika kuiba, kula rushwa, wafanyabiashara watalazimika kukwepa kodi, wakulima watadhulumiwa kwa kuuza mazao yao bei ya chini na vyama vya ushirika hivyo kulazimika kuachana na kilimo na kuja mijini na kubanana hukuhuku na kuanza uhalifu baada ya kukosa vibarua na maisha kuwashinda! Madhara ni mengi sana, hayo ni baadhi tu
Hiyo ndio CCM iliyochaguliwa na kuchakachua kura na hayo ndiyo madhara ya kuongozwa na CCM . Lakini haiingii akilini kwanini watu wengine ingawa ni haki yao kimsingi, lakini kwanini waliamua kuipigia kura CCM despite madhambi yake yote, kutojali maslahi ya wananchi na incompetence na underperformance yake?
Kwa mtazamo wangu mimi napata jibu moja kubwa, kwamba Watanzania walioipigia kura CCM ni watu wanaofaidika nayo zaidi ya wale ambao hawakuipigia kwa namna moja au nyingine kwa mfano, wengine:
-wanafaidika na ufisadi moja kwa moja, hizo ni zile familia zifaidikazo na ufisadi
-ni wafanya ufisadi makazini kwao waogopao uongozi kama wa Slaa ukija utapambana nao na kuwatoa ktk vyeo au kuwadhibiti, wengine wanaoogopa nyumba walizouziana zisije rudishwa serikalini, n.k.
-wengine ni wafanya biashara wafaidikao ka kutoa rushwa na wakwepa kodi n.k, wanamwogopa Dr Slaa.
-wanafaidika na viji favours vya CCM kama CLOUDS FM, n.k.
-wako wale waliofaidika kwa muda mfupi na rushwa za kampeni, vitisho vya kuvunjika kwa amani n.k (hao ni kundi kubwa) ambao baadhi yao hawako well informed (wa vijijini) kuhusu madhambi ya CCM kutokana na kuwa na miundo mbinu mibovu ya kimawasiliano, hao pia baadhi wana amini Nyerere yuko (au mzimu wake bado upo unawaona) na CCM ni Nyerere na Nyerere kwa kuwa alikuwa ni mwadilifu basi CCM ya kiadilifu mpaka leo (kama wangesomeshwa wangestuka).
Kwahiyo kura za watakazopata CCM zita reflect ni aslimia ngapi ya Wanatanzania wanafaidika na madhambi yaCCM na kukumbatia madhambi ya CCM na hivyo kudhihirisha how rotten some Tanzanians are.
It is noteworthy kwamba kuna wana CCM wachache ambao ni safi na wema, ambao nao pia wanatakiwa wakihame chama hicho badala ya kukipigia kura.
Dr Slaa kama kweli kura zako na za wabunge na madiwani wako zimeibiwa ni lazima uipiganie haki yako. Na baadhi ya wapenda haki tutakuwa nyuma yako! Usikate tamaa kwani you are not walking alone you and CHADEMA members. Watanzania wengi wanapenda kuona haki inatendeka ila hawajui pakuanzia. Wewe ni mwanga wao. Hakuna amani bila haki, kwani CCM kuendelea kuchelewesha maendeleo yetu Watanzania ni zaidi ya violence ambayo baadhi ya wana JF wana jaribu kuitetea kuwa haitakiwi, wakati hawajui indirectly amani inavunjwa kila mara CCM wanapoiba kura, wanafanya ufisadi, kwani kwa uongozi mbovu wa CCM watoto wengi wamekufa vifo mahospitalini, wameshindwa kusoma n.k. Idadi yao ni kubwa isiyoelezeka pamoja na consequences nyingine nyingi zinazoletea vifo, kupungua kwa life expectancy yetu, kupungua kwa quality ya life ya Watanzania (hayo yote hatuayaoni).
Hivyo napenda kuwaambia kuwa amani imeishavunjika zamani tu, kwani kwa unyama na uharamia huo wa CCM madhara mengi yametokea na yataendelea kutokea! Na msidhanie niko nje ya nchi ndo maana sijali amani! Niko hukuhuku ila macho yangu angalau yamefumbuka. Kwangu mimi amani iliisha vunjwa kila mara niliposikia ndugu zangu wengi wamekufa kwa magonjwa ambayo kama CCM ingekuwa makini yasingekuwepo kama malaria, utapia mlo na pia ndugu zangu wengi kukosa elimu bora kutokana na wizi na kukosekana na umakini wa CCM. Kwakweli siwezi kuipenda na kwangu mimi ni chama kilichikwisha vunja amani muda mrefu! Uvunjaji amani wa CCM ni a long term problem (49 yrs) which needs to be eradicated.
Tusishabikie CCM kama tushabikiavyo Simba na Yanga, unless unafaidika nayo kwa njia nyingine ambazo ni illegal na informal. Unajua tatizo letu Watanzania wengi tunapenda kusikia hadithi tamutamu na za uongo ili tumchague mtu. Sometimes huwa natamani kama Dr Slaa angetoa ahadi tamutamu uku akificha makucha yake, ahalafu akishika urais atuchenjie Watanzania na kutuwajibisha na ilikutubadilisha kimaisha. Maendeleo ya nchi yetu hayatakuja kwa ujanja ujanja! Nchi nyingi za Asia ambazo tulipata nazo uhuru karibu sawa na zina rasilimali za asili chache kuliko sisi lakini sasahivi zimeendelea sana kutokana na kuwajibika kwao na si ujanja ujanja.
Tunampenda Dr Slaa kwa kuwa ni mtu safi (hata CCM na usalama wa Taifa wamemwinda wakakosa madhambi yake kama ya kwao wakabaki kumbambikia kesi ya wizi wa mke na eti kashindwa upadre) mwenye na uchungu na Wananchi wenye maisha magumu yaliyosababishwa na CCM. Na daima ili uwe kiongozi mzuri, mwenye mfano wa kuigwa inabidi uwe safi ili uweze kuwakaripia wenzako wakoseapo, sasa JK atamkaripiaje fisadi mwenzake wakati yeye ni fisadi tu kama wao? Siwezi kuipenda CCM kwani haijatimiza wajibu wake kwangu na kwa Watazania wengi!
Kwa kuwa Dr Slaa ni msafi basi ni haki kama kweli ameibiwa kura apewe haki yake, hata kama aliibiwa kura moja au za kutomtosha kutokuwa rais. Haki ni haki tu! Mimi kwa upande wangu ninaamini mengi asemayo Dr Slaa kuwa ni ukweli, kwani ni mtu afanyaye utafiti wa mambo yake kabla hajayaweka hadharani, ingawa mwanzoni huwa yanapingwa lakini mwishoni huwa ni ukweli. Kwahiyo ilo la kuibiwa kura kwa kiasi kikubwa mimi naamini ni ukweli na najua atatoa ushahidi, lakini CCM watagoma, hapo Dr Slaa usikate tamaa, tumia simulia ukweli umma wa Watanzania, mahakama na vyombo vya Kimataifa na sisi tuko nyuma yako, tutadai amani kwa njia yeyote ile hata ikibidi kufanya lolote lile! CCM mmeenda mbali! Mnatukwaza!
Ilikuwa hainiingii akilini CCM watakubalije kushindwa watakaposhindwa? Duh! Kumbe mabwana wajanja sana hawa! Wakaitumia usalama wa Taifa, majeshi, tume ya uchaguzi na TAKUKURU kuhakikisha wanatinga ikulu na mjengoni!
Wakaanza na kura feki za maoni ili tuamini hata wakiiba kweli walistahili wapate ushindi ukaribianao na asilimia ya kura hizo za maoni, (what a coincidence, ushindi wa unakaribiana na kura hizo za maoni)! Then likapitishwa container lenye karatasi za kura, usalama wa Taifa pamoja na akina Miraji na watu wake wa IT waanza training ya kuchakachua (huku BMW ikipita kila kona kuandaa mazingira mazuri) na mara uchapishwaji wa karatasi za kura ukaanza kuhamishwahamishwa na then mara tume ikaingiza computer kurekodi matokeo, kabla ya uchaguzi zikaanza hotuba za wapinzani watavunja amani na kura zilipoanza hesabiwa matokeo ya majimbo yenye nguvu ya wapinzani yakaanza cheleweshewa kura zao, na mara baadhi yalipotangazwa ikawa wagombea wa CHADEMA wakawa wameshindwa wakati walishinda na kali zaidi hata matokeo ya urais yalipoanza eti kwa bara hata baadhi majimbo yale yaliyochukua viti vya ubunge kwa upinzani, ilipokuja kwenye kura za urais Dr Slaa akawa wa pili baada ya JK!
Jamani hata kama mtu ulikuwa hutaki amini kura zimefanyiwa adulteration (chakachuliwa), lakini ina make sense kwa trend hiyo haswa kama unapendatumia logic na si ushabiki. Hivi hao wabunge wa CHADEMA waliochaguliwa kwa wingi ktk majimbo waliyopata aliyewafanya wachaguliwe ni nani? Ni Dr Slaa (huo ni ukweli usiopingika, Dr Slaa amechangia asilimia kubwa pamoja na juhudi zao binafsi), sasa iweje wananchi hao waliompenda Dr Slaa hadi kuamua kuwapigia kura wabunge wake hata kama hamfahamu vizuri (ili akiwa rais apate wabunge wengi) iweje leo wananchi haohao wamnyime kura Dr Slaa? Moja na moja ni mbili, the answer is very obvious, there was a fault play.
Na nnazidi kuamini CCM wamechakachua kura kutokana na historia yao ya nyuma, they are very good and proficient at that. Historia inaonyesha kura za Zanzibar waliisha iibia CUF mpaka CCM mzee Karume akatumia busara zake kwa kujua ni kweli CCM iliiba na yeye hapendi kwani roho ilimsuta akaamua muafaka! Skwizi Waafrika baadhi pindi tuibapo kura tunakimbilia muafaka ili tuwapoze tuliowaibia na pia tusikose zote na ndio maana hata pesa za EPA CCM walipoiba ukakimbiliwa muafaka wa kuwaambia walioiba warudishe pesa wakati sheria inajulikana ni kamata peleka mahakamani na funga kama wamepatikana na hatia! Pili CCM haohao walishawahi mwibia Dr Slaa jimboni mwake kura. Sasa kwanini Dr Wetu wa kiukweli anayejali maslahi yetu akisema ameibiwa nisimwamini? Akiamua lolote ili kutetea kura zake kwanini nisimtii?
Dr unachotakiwa ni kumwaga evidences zako zote kwenye vyombo vya habari, kwa Watanzania wote, mahakamani, vyombo vya kimataifa na ndio pia ikishindikana lolote liwalo na liwe! Watu wataumia na kwa muda, lakini for a just cause it is worth it! Mungu atatusuta sisi Watanzania kwa kukumbatia mafisadi na CCM kwa kuichagua tena wakati tunajua ni chama cha mafisadi. Dr tetea haki yako kuliko wakati wowote ulioishi hapa Duniani, tetea zaidi ya ulivyopiga kampeni! Mapambano ndo yanaanza, be very strong. Nchi hii haiwezi kuendelea kutawaliwa na wahuni, its time for a change. Hatuihitaji uongozi usio na tone la maadili hata kidogo! Tu convince zaidi kwa evidences zako nzuri, nasi tutapata mzuka! Katangaze vyombo vyo Kiamataifa jinsi ulivyoibiwa kura zako na Dunia itaujua ukweli na itapata mzuka pia, hata tukinyimwa misaada ya wafadhili potelea mbali! Lakini at the end of the tunnel there is a bright light shining out there, so don't give up Dr na CHADEMA.
Dr Slaa angalia na usije ukawa wiped out, kwa jinsi uanvyoitikishwa CCM na mafisadi hawatakuwa na amani mpaka wakuondoe kabsaa Dunia hii! Ni simple logic kwamba wewe ni threat to them, you've caused them alot of trouble kwa mafisadi, na bado utaendelea ku cause some more trouble. To them you're a big nuisance. So what is a much easier solution than to wipe you out for good? So jilinde jilinde jilinde, na sisi Watanzania tuchukiao umaskini na ufisadi na wana CHADEMA tutakulinda kwa kadri ya uwezo wetu na tunakuombea kwa Mungu akulinde!
Na mwisho Watanzania tuache uwoga! Nyerere angekuwa mwoga leo tusingekuwa na uhuru na wala asingempiga Idd Amini kwa kuogopa kufa yeye, familia yake na Watanzania kwa ujumla na wala asinge support kijeshi nchi za Africa ziondokane na makucha ya wakoloni na kupeleka majeshi yetu huko na pia kutoa mafunzo, n.k kwa kuogopa watakufa au watalipa kisasi. Mbona hakusema naogopa vunja amani tusije kufa? Na kwake maisha mazuri ya vizazi vijavyo yalikuwa ni muhimu kuliko amani feki ya muda mfupi na uhai wake na Wa Watanzania. Alifanya hivyo kwa sababu haki ilikuwa imevunjwa, na sisi ikibidi kudai amani kwa style hiyo itabidi iwe ivyo kwani tayari kwa umaskini huu wa kuletwa na CCM, kwa ufisadi huu na uchakachuaji huu amani imeisha vunjwa na tunakufa sana kila siku kwa umaskini uliokithiri in one way or another. Hopefully and i pray so much that, this issue will be resolved wisely and peacefully. God bless Tanzania.