Suala si kama ccj ingeandikishwa, bali je waliotajwa walishiriki? Ukweli ndio unatakiwa ujulikane. Tusubiri reaction ya waliotajwa.
SITTA AJIBU
Waziri Sitta alipoulizwa kuhusu madai ya Mpendazoe alisema:
"Sipendi kuzungumzia siasa za mtu mmoja mmoja badala ya kuzungumzia maendeleo. …waanzilishi wa CCJ wapo kwa msajili."
Aliongeza kwamba: "Kuingia au kutoka kwenye chama chochote cha siasa ni hiyari, lakini kama unavyojua, leo unaweza kuambiwa hata unataka kujiunga CUF au chama kingine lakini utakakokuwa ndiko kutaeleza msimamo wako."
Alisema uhakika wa tuhuma zilizotolewa na Mpendazoe unaweza kupatikana kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na si vinginevyo.
MWAKYEMBE ANENA
Dk. Mwakyembe alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikanusha madai hayo na kusema kuwa Mpendazoe aliwahi kumfuata yeye binafsi pamoja na wabunge wengine wengi wa CCM ili wamuunge mkono katika kutimiza ndoto yake ya kuanzisha chama cha siasa.
Alisema Mpendazoe walijuana kama mbunge mwenzake, na aliwafuata wabunge wengi wa CCM kutaka wamuunge mkono ili kutimiza ndoto yake, kitu ambacho si kosa la jinai.
Dk. Mwakyembe alifafanua kuwa Mpendazoe aliwafuata wabunge wengi wenye mvuto, kwani ni kawaida katika uwanja wa siasa wenye mvuto wa kisiasa kutafutwa na vyama vya siasa.
"Wanasiasa wenye mvuto hufuatwa na vyama tofauti vya siasa ili wajiunge navyo, " alisema ndivyo alivyofanya Mpendazoe na kuongeza kuwa:
"Mpendazoe alishindwa kuwashawishi wabunge hao ndiyo maana wakampuuza."
"Sisi tumeamua kubaki ndani ya chama tawala kuendesha mapambano dhidi ya ufisadi. Tutaendelea na mapambano tukiwa humu ndani na tunafanikiwa sana," alisema Dk. Mwakyembe.
Dk. Mwakyembe alisema alifuatwa na vyama vingi vikiwemo NCCR- Mageuzi na Chadema lakini akasema: "Akili ya mwingine changanya na yako."
Aliongeza kuwa tatizo la Mpendazoe ni kwamba ana papara wakati siasa hazitaki hivyo na wala siasa sio mdundiko ambao kila anayeusikia husindikiza kwa macho na kwa miguu.
MAKONDA ANG'AKA
Naye Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya Moshi Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kilimanjaro, Paul Makonda akizungumzia tuhuma hizo alikanusha madai hayo ya Mpendazoe.
Makonda akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu,
alisema kauli ya Mpendazoe ni jitihada za mafisadi kutaka kuteka ajenda ya kupambana na ufisadi hapa nchini na ndani ya CCM. Alisema yote hayo yameibuka dhidi yake baada ya kuonekana mstari wa mbele kupambana na ufisadi ndani ya CCM.
Aliongeza kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa anayo majina ya watu walioanzisha chama hicho na kuongeza kuwa ana uhakika hayumo katika orodha hiyo. Alimkejeli Mpendazoe na kusema kuwa hapo alipofika kisiasa anaweza kusema kitu chochote ili mradi ajikuze, lakini hana hoja zozote za msingi. Nape alikwisha kukanusha kuhisika na kuanzishwa CCJ. Naye Mbunge wa Lupa (CCM),
VICTO MWAMBALASWA
Victor Mwambalaswa, alipoulizwa kuhusiana na madai hayo ya Mpendazoe, alithibitisha kuwa alifuatwa na mwanasiasa huyo ili ajiunge na CCJ lakini alikataa. Alisema mwanasiasa yoyote mwenye mvuto kwa wapiga kura anafuatwa na vyama vya siasa unapokaribia uchaguzi, lakini kukubali ama kukataa kujiunga navyo ni hiari yake.
Alisema kauli ya Mpendazoe ni ya barabarani lakini ukweli ni kwamba kwa Msajili wa Vyama vya Siasa jina lake halipo kama miongoni mwa waasisi wa CCJ mwaka 2010.