Mpasuko mpya CCM

M

Msharika

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
937
Likes
4
Points
35
M

Msharika

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
937 4 35
HUKU Kamati ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ikiwa imeongezewa muda kukamilisha usuluhishi miongoni mwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kundi jipya limeibuka ndani ya chama hicho likitaka vigogo kadhaa wafukuzwe uanachama.

Kundi hilo limetoa majina 16 ya vigogo wa kufukuzwa, maazimio matano mazito na limezitaka serikali za nchi takriban nne zinazoaminika kutumika kuhifadhi mabilioni ya vigogo nchini zisaidie kurejesha fedha hizo.

Raia Mwema imetumiwa nakala ya tamko hilo, ambalo linaitaka Serikali za Tanzania kuomba msaada nchi za Uswisi, Costa Rica, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na serikali za visiwa vya Man na Jersey, na nchi nyingine zinazotumika kuficha taarifa za kodi, kurejesha fedha zilizowekwa huko na viongozi wa Tanzania.

Kutoka katika tamko hilo, wanaotajwa ili wafukuzwe ambao kwa sasa tunahifadhi majina yao ni pamoja na mmoja aliyepata kuwa waziri mkuu; mawaziri wawili wa Serikali ya Awamu ya Tatu; mbunge na mfanyabiashara maarufu; aliyepata kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi; na mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Katika orodha hiyo, wamo pia wabunge 11 wa Bunge la sasa wa Mikoa ya Arusha, Mara, Kagera, Kilimanjaro, Shinyanga, Dar es Salaam na Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Waziri. Sehemu kubwa ya wabunge hao ni wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na wengine ni waliowahi kuwa viongozi wa umma, wenye ukwasi mkubwa.

Kwa mujibu wa tamko la kundi hilo, vivogo hao wa ndani ya CCM wanahusishwa na kashfa 17 za kitaifa na kimataifa ambazo zimetajwa kuwa ni Loliondo, IPTL, Commodity Import Support, Mgodi wa Kiwira, Akaunti ya EPA, kampuni za Meremeta Ltd, Mwananchi Gold, Deep Green Finance, na Tangold.

Kashfa nyingine ni rada, ununuzi wa ndege ya Rais (Gulfstream 500), Richmond, Dowans, magari, silaha na helikopta za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), silaha haramu, dawa za kulevya, uuzaji wa maeneo wazi, misamaha ya kodi, ujenzi wa jengo Benki Kuu na uuzaji wa maeneo ya ufukwe Dar es Salaam.

Kundi hilo ambalo limesambaza tamko hilo kwenye mtandao, limejitambulisha kama wapiganaji wa kweli CCM- na kauli mbiu yake ni “Kwa ajili ya Taifa letu; sasa na baadaye.”

Katika mawasiliano hayo, ambayo Raia Mwema imeyapata, hakuna majina ya wanaoliunda kundi hilo, lakini limenukuu mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 na kuutumia kujenga hoja.

Mwongozo huo wa 1981 unasema: “Huko nyuma tulishinda katika mapambano yetu kutokana na umoja wetu wa kitaifa, usahihi wa siasa yetu na uongozi bora wa chama.

“Leo na katika siku za usoni tutahitaji umoja imara zaidi, siasa sahihi na uongozi bora wa chama.. vibepari na vibwanyenye vya humu nchini vimeonyesha dhahiri uhasama wao dhidi ya maslahi ya wakulima na wafanyakazi, umoja wa sasa lazima usimame juu ya misingi iliyo wazi na sahihi, misingi ya ujamaa; kwa hiyo ni umoja wa wakulima na wafanyakazi na wale wote wanaounga mkono kwa vitendo ujenzi wa ujamaa nchini.”

Kama alama ya utambulisho wake, kundi hilo linasema: “Sisi ni wananchi wa Tanzania. Sisi vile vile ni wana CCM ambao tumechoshwa na mwelekeo wa kisiasa nchini, na hasa kuhusishwa kwa baadhi ya wana-CCM na vitendo vya ufisadi ambavyo vimekipaka matope chama, lakini zaidi tumechoshwa na Serikali inayoongozwa na chama chetu kuhusishwa na ufisadi katika wizara, idara, wakala na taasisi zake mbalimbali.

“Kama Watanzania hatuwezi tena kukaa kimya na kusubiri watu wengine waje kutuletea mabadiliko; hatuwezi tena kukaa pembeni na kuacha raslimali za nchi yetu ziendelee kugawanywa mikononi mwa kikundi cha watu wachache kana kwamba ni haki yao ya kuzaliwa; hatuwezi tena kukaa kimya tukizionea haya chembechembe za ufisadi ndani ya chama na kwenye serikali.”

Kwa mujibu wa maelezo ya kundi hilo, mabadiliko yanahitajika ambayo yanapaswa kuwa ajenda kuu ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Kipengele hicho cha kuhimiza mabadiliko kinasema:

“Mabadiliko ya kweli yatakayofumua fumua mtandao wa uhalifu na ufisadi nchini na hatimaye kurejesha imani ya wananchi kwa Serikali yao na kwa CCM na kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anayo nafasi ya kufanikiwa katika Taifa lake na kuhakikisha tunaweka misingi ya mafanikio kwa kizazi kipya cha Watanzania”.

Kundi hilo lmejitambulisha pia kuwa kuwa baadhi yao ni wabunge na viongozi wa CCM, wakiwamo kutoka baadhi ya jumuiya za chama hicho na wengine ni wanachama wa kawaida, na kwamba limetoa tamko hilo ikiwa ni sehemu ya juhudi ya wazi ya kujikosoa kwa mujibu wa mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 (ibara ya 5.

Tamko hilo linaeleza kuwa Watanzania wengi wamechoshwa na ufisadi uliokubuhu na utendaji duni na wa kusikitisha wa vyombo vya Serikali, hali inayowafanya kutojali masuala muhimu ya nchi huku kila mmoja akitazama masuala binafsi na ya familia.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, tamko hilo linaweka masharti kwa CCM kuekelea Uchaguzi Mkuu kwamba; “Chama cha Mapinduzi hakiwezi na hakipaswi kusimama kuomba kura tena kwa wananchi isipokuwa baada ya ushahidi wa wazi wa vitendo wenye kung'oa chembechembe zote zenye kuendeleza vitendo vya rushwa na hongo, uzembe, kutokuwajibika, ubadhirifu, ufujaji wa mali ya umma na matumizi mabaya ya madaraka kwa ajili ya manufaa binafsi ya watu wafanyao hayo, yaani ufisadi.

Kutokana na mtazamo huo, kundi hilo limebainisha maazimio yake matano. Azimio namba moja linasomekana: “Tunakataa mpango wowote, juhudi zozote na mchakato wowote utakaolenga kutafuta umoja na upatanishi kati ya chembe za ufisadi ndani ya chama, tunaamini hakuna umoja na ushirika wa kweli unaoweza kupatikana na mafisadi au na wale wanufaikaji wa ufisadi. Chama cha Mapinduzi hakina nafasi kwao au makuwadi wao.

Azimio namba mbili linaeleza: “Tunakataa juhudi zozote za kujaribu kuwaondoa wanachama wenye uwezo wa kuongoza na walioonyesha uwezo huo kwa vitendo kwa kisingizio cha umri ili kuwapisha “vijana”. Tunaamini kama Taifa tutafanya kosa kubwa sana kuamua mara moja kuliacha Taifa mikononi mwa vijana kwa sababu ya umri tu. Tunaamini kila mwana CCM mwenye uwezo wa kuongoza na anayekubalika kwa wananchi wake asinyimwe nafasi ya kuongoza kwa kisingizio cha umri.

“Tunawaunga mkono wana CCM ambao mbali ya kuwa na uwezo wa kuongoza wameamua kukaa pembeni ili kuruhusu wanachama wengine kuingia katika safu ya uongozi. Uamuzi huu usionekane kuwa ni udhaifu au ni njia ya kuwalazimisha wengine kuufuata. Kustaafu nafasi ya uongozi kunaweza kufanywa na mtu yeyote pasipo kujali umri wake.

Azimio namba tatu linaeleza: “Kutetea raslimali za Taifa letu na utajiri wa nchi yetu kwa kukusudia kuzuia mikataba na mipango yoyote yenye kurundika utajiri wetu mikononi mwa wafanyabiashara wakubwa bila kujali maslahi ya leo ya Taifa au yale ya kizazi kijacho.

“Tunachukua msimamo huo tukiamini kuwa kama viongozi wa CCM tunalojukumu la kichama kueneza matunda ya Uhuru kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa jumla. Kwa mujibu wa Ibara ya 17:2 ya Katiba ya CCM. Jukumu hili si la wapinzani au wafadhili wa kigeni; ni jukumu letu kama Watanzania na kama wana CCM.”

Azimio namba nne: “Kupigania haki ya kila Mtanzania kugombania nafasi ya uongozi pasipo kulazimishwa kujiunga na chama cha siasa. Kama Watanzania kwanza na kama wana CCM, tunaamini haki ya kuchaguliwa isiunganishwe na ulazima wa kujiunga na chama
cha siasa kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vile vile kupingana na Tamko la Haki za Binadamu la 1948 ambalo Tanzania imeliridhia.

“Chama cha Mapinduzi na wana CCM hatuogopi wagombea binafsi, kwani tunaamini chama chetu kinakubalika, kina uwezo wa kuongoza bila kujali wagombea wengine wanatoka wapi au wanapatikana vipi.”

Azimio namba tano: “Kuhakikisha mfumo bora wa kuwajibika na kuwajibishana unakuwapo katika Serikali kwa kupendekeza mabadiliko ya Katiba na sheria mbalimbali ili hatimaye mfumo ambao umefungua milango ya kifisadi unakosolewa, kubomolewa na kubadilishwa na mfumo ambao hautatoa nafasi kwa watu na vikundi vya watu kuneemeka kwa kutumia mbinu za kifisadi.
“Bila ya kuubadili mfumo huu tunaamini mafisadi wataendelea kuibuka kati yetu na kama Taifa tutaendelea kupiga kambi kwenye hili bonde la ufisadi miaka nenda rudi. Ni lazima tuubadili mfumo huu tukizingatia vile vile malengo ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupamba na Umasikini namba mbili (MKUKUTA II).”

Katika hatua nyingine inayoweza kuhusishwa na juhudi za kundi mojawapo kati ya yanayopingana CCM, Chama Cha Jamii (CCJ) jana Jumanne kilipata usajili muda jana.

Chama hicho kama ilivyo kwa kundi hili linalojitambulisha kama wapiganaji wa kweli, kimekuwa kikihusishwa na baadhi ya vigogo wa CCM lakini ambao hawajajitokeza hadharani.

Hali hiyo ya kuhusishwa vigogo wa CCM na CCJ, na kisha kuibuka kwa kundi hili jipya la wapiganajii wa kweli, inatajwa kuchochewa na udhaifu wa kiuongozi ndani ya CCM.

Hata hivyo, wananchi wengi wamekuwa wakishangazwa na vigogo wanaodai wanapenda mabadiliko ndani ya CCM lakini waoga kujitokeza hadharani, ikielezwa kuwa kujificha huko ni udhaifu mkubwa kwa makundi hayo kwa kuwa huo si ujasiri unaostahili kuchochea mabadiliko nchini.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
31
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 31 0
Mmh,jamani si wapasuke tu mbona wanachelewa hivyo?
 
K

KunjyGroup

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2009
Messages
352
Likes
1
Points
33
K

KunjyGroup

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2009
352 1 33
Wacha kipasuke. Kipasuke hata vipande kumi. Bora. Tumechoka na sisiem
 
A

alles

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2006
Messages
356
Likes
0
Points
0
A

alles

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2006
356 0 0
Hakuna jipya kwenye ii news.Hiyo article ilijadiliwa hapa JF wiki mbili zilizopita, ikaonekana haina jipya kwa sababu wahusika hawakuweka majina yao wala saini zao.May be Raia mwema wameichukua ili kuuza gazeti.Kumbe nao huwa wanaokotaokota hata news zisizo na uthibitisho..ni aibu.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,032
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,032 280
Alles.. habari ndiyo ilivyo.. na mpasuko huo upo kama ulivyo.. kuweka majina yao au kutokuweka hakuondoi ukweli wa msimamo wao.
 
A

alles

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2006
Messages
356
Likes
0
Points
0
A

alles

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2006
356 0 0
mzee mwanakijiji, sikatai uwepo wa mpasuko ndani ya ccm(binafsi naomba ipasuke).Iila nilitegemea Raia mwema waende mbele zaidi ya walipoishia wana-Jf kuijadili iyo nakala wiki mbili zilizopita.
 
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
21,829
Likes
151
Points
160
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
21,829 151 160
as an ordinary TAnzanian with no political portfolio... nimechoka sasa na hekaya za mipasuko isiyo na kichwa wala miguu

nina mwaka wa saba sasa nasikia ccm inapasuka, mara wanamtandao, mara mamvi, mara loud spika!!! imetosha sasa, watanzania hasa waandihsi wa habari tumeanza kuchoka na speculative statements kama waingereza ambao ni rumour mongers...

i'd rather enjoy ripoti za ka-nzi kuhusu mapanki na national security involvement kwenye silaha kuliko kusikia hekaya za abunuwasi bin CCM

nafananisha hali ya CCM na malumbano yake na hadithi ya mawifi

ITS ABOUT TIME
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,032
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,032 280
mzee mwanakijiji, sikatai uwepo wa mpasuko ndani ya ccm(binafsi naomba ipasuke).Iila nilitegemea Raia mwema waende mbele zaidi ya walipoishia wana-Jf kuijadili iyo nakala wiki mbili zilizopita.
makosa makubwa yaliyofanyika kuanzia mwaka jana na tumeyaonesha hapa mara nyingi ni kuwa kile ambacho kimekuwa kikiitwa "mpasuko" ndani ya CCM si lolote si chochote isipokuwa mgongano wa watu na maslahi yao binafsi. Haukuwa mpasuko wa kiitikadi, kimtazamo au kimwelekeo.

Bila ya shaka wapiganaji wa kweli wa CCM wanatambua kuwa hilo halitoshi. Hivyo, hadi hivi sasa hakujawa na mpasuko ndani ya CCM na hao wapiganaji ninavyoelewa mimi wamejaribu kulazimisha mpasuko wa kiitikadi (ideological split).
 
A

alles

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2006
Messages
356
Likes
0
Points
0
A

alles

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2006
356 0 0
Big up mwanakijiji, ii hoja yako imekomaa
 
Babylon

Babylon

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2009
Messages
1,338
Likes
4
Points
135
Babylon

Babylon

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2009
1,338 4 135
Lete Mambo yenu ya Upwagu na upwaguzi kama kawaida ,maporojo ya kufurahisha ukumbi (Donda ndugu halina dawa )kiufupi Hamkijui mnacho kitaka.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,032
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,032 280
Lete Mambo yenu ya Upwagu na upwaguzi kama kawaida ,maporojo ya kufurahisha ukumbi (Donda ndugu halina dawa )kiufupi Hamkijui mnacho kitaka.
na wale wanaokijua wanachokitaka hawasemi..
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,350
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,350 280
HUKU Kamati ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ikiwa imeongezewa muda kukamilisha usuluhishi miongoni mwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kundi jipya limeibuka ndani ya chama hicho likitaka vigogo kadhaa wafukuzwe uanachama.
Kundi hilo limetoa majina 16 ya vigogo wa kufukuzwa, maazimio matano mazito na limezitaka serikali za nchi takriban nne zinazoaminika kutumika kuhifadhi mabilioni ya vigogo nchini zisaidie kurejesha fedha hizo.
Raia Mwema imetumiwa nakala ya tamko hilo, ambalo linaitaka Serikali za Tanzania kuomba msaada nchi za Uswisi, Costa Rica, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na serikali za visiwa vya Man na Jersey, na nchi nyingine zinazotumika kuficha taarifa za kodi, kurejesha fedha zilizowekwa huko na viongozi wa Tanzania.
Kutoka katika tamko hilo, wanaotajwa ili wafukuzwe ambao kwa sasa tunahifadhi majina yao ni pamoja na mmoja aliyepata kuwa waziri mkuu; mawaziri wawili wa Serikali ya Awamu ya Tatu; mbunge na mfanyabiashara maarufu; aliyepata kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi; na mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Katika orodha hiyo, wamo pia wabunge 11 wa Bunge la sasa wa Mikoa ya Arusha, Mara, Kagera, Kilimanjaro, Shinyanga, Dar es Salaam na Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Waziri. Sehemu kubwa ya wabunge hao ni wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na wengine ni waliowahi kuwa viongozi wa umma, wenye ukwasi mkubwa.
Kwa mujibu wa tamko la kundi hilo, vivogo hao wa ndani ya CCM wanahusishwa na kashfa 17 za kitaifa na kimataifa ambazo zimetajwa kuwa ni Loliondo, IPTL, Commodity Import Support, Mgodi wa Kiwira, Akaunti ya EPA, kampuni za Meremeta Ltd, Mwananchi Gold, Deep Green Finance, na Tangold.
Kashfa nyingine ni rada, ununuzi wa ndege ya Rais (Gulfstream 500), Richmond, Dowans, magari, silaha na helikopta za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), silaha haramu, dawa za kulevya, uuzaji wa maeneo wazi, misamaha ya kodi, ujenzi wa jengo Benki Kuu na uuzaji wa maeneo ya ufukwe Dar es Salaam.
Kundi hilo ambalo limesambaza tamko hilo kwenye mtandao, limejitambulisha kama wapiganaji wa kweli CCM- na kauli mbiu yake ni “Kwa ajili ya Taifa letu; sasa na baadaye.”
Katika mawasiliano hayo, ambayo Raia Mwema imeyapata, hakuna majina ya wanaoliunda kundi hilo, lakini limenukuu mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 na kuutumia kujenga hoja.
Mwongozo huo wa 1981 unasema: “Huko nyuma tulishinda katika mapambano yetu kutokana na umoja wetu wa kitaifa, usahihi wa siasa yetu na uongozi bora wa chama.
“Leo na katika siku za usoni tutahitaji umoja imara zaidi, siasa sahihi na uongozi bora wa chama.. vibepari na vibwanyenye vya humu nchini vimeonyesha dhahiri uhasama wao dhidi ya maslahi ya wakulima na wafanyakazi, umoja wa sasa lazima usimame juu ya misingi iliyo wazi na sahihi, misingi ya ujamaa; kwa hiyo ni umoja wa wakulima na wafanyakazi na wale wote wanaounga mkono kwa vitendo ujenzi wa ujamaa nchini.”
Kama alama ya utambulisho wake, kundi hilo linasema: “Sisi ni wananchi wa Tanzania. Sisi vile vile ni wana CCM ambao tumechoshwa na mwelekeo wa kisiasa nchini, na hasa kuhusishwa kwa baadhi ya wana-CCM na vitendo vya ufisadi ambavyo vimekipaka matope chama, lakini zaidi tumechoshwa na Serikali inayoongozwa na chama chetu kuhusishwa na ufisadi katika wizara, idara, wakala na taasisi zake mbalimbali.
“Kama Watanzania hatuwezi tena kukaa kimya na kusubiri watu wengine waje kutuletea mabadiliko; hatuwezi tena kukaa pembeni na kuacha raslimali za nchi yetu ziendelee kugawanywa mikononi mwa kikundi cha watu wachache kana kwamba ni haki yao ya kuzaliwa; hatuwezi tena kukaa kimya tukizionea haya chembechembe za ufisadi ndani ya chama na kwenye serikali.”
Kwa mujibu wa maelezo ya kundi hilo, mabadiliko yanahitajika ambayo yanapaswa kuwa ajenda kuu ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Kipengele hicho cha kuhimiza mabadiliko kinasema:
“Mabadiliko ya kweli yatakayofumua fumua mtandao wa uhalifu na ufisadi nchini na hatimaye kurejesha imani ya wananchi kwa Serikali yao na kwa CCM na kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anayo nafasi ya kufanikiwa katika Taifa lake na kuhakikisha tunaweka misingi ya mafanikio kwa kizazi kipya cha Watanzania”.
Kundi hilo lmejitambulisha pia kuwa kuwa baadhi yao ni wabunge na viongozi wa CCM, wakiwamo kutoka baadhi ya jumuiya za chama hicho na wengine ni wanachama wa kawaida, na kwamba limetoa tamko hilo ikiwa ni sehemu ya juhudi ya wazi ya kujikosoa kwa mujibu wa mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 (ibara ya 58).
Tamko hilo linaeleza kuwa Watanzania wengi wamechoshwa na ufisadi uliokubuhu na utendaji duni na wa kusikitisha wa vyombo vya Serikali, hali inayowafanya kutojali masuala muhimu ya nchi huku kila mmoja akitazama masuala binafsi na ya familia.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, tamko hilo linaweka masharti kwa CCM kuekelea Uchaguzi Mkuu kwamba; “Chama cha Mapinduzi hakiwezi na hakipaswi kusimama kuomba kura tena kwa wananchi isipokuwa baada ya ushahidi wa wazi wa vitendo wenye kung'oa chembechembe zote zenye kuendeleza vitendo vya rushwa na hongo, uzembe, kutokuwajibika, ubadhirifu, ufujaji wa mali ya umma na matumizi mabaya ya madaraka kwa ajili ya manufaa binafsi ya watu wafanyao hayo, yaani ufisadi.
Kutokana na mtazamo huo, kundi hilo limebainisha maazimio yake matano. Azimio namba moja linasomekana: “Tunakataa mpango wowote, juhudi zozote na mchakato wowote utakaolenga kutafuta umoja na upatanishi kati ya chembe za ufisadi ndani ya chama, tunaamini hakuna umoja na ushirika wa kweli unaoweza kupatikana na mafisadi au na wale wanufaikaji wa ufisadi. Chama cha Mapinduzi hakina nafasi kwao au makuwadi wao.
Azimio namba mbili linaeleza: “Tunakataa juhudi zozote za kujaribu kuwaondoa wanachama wenye uwezo wa kuongoza na walioonyesha uwezo huo kwa vitendo kwa kisingizio cha umri ili kuwapisha “vijana”. Tunaamini kama Taifa tutafanya kosa kubwa sana kuamua mara moja kuliacha Taifa mikononi mwa vijana kwa sababu ya umri tu. Tunaamini kila mwana CCM mwenye uwezo wa kuongoza na anayekubalika kwa wananchi wake asinyimwe nafasi ya kuongoza kwa kisingizio cha umri.
“Tunawaunga mkono wana CCM ambao mbali ya kuwa na uwezo wa kuongoza wameamua kukaa pembeni ili kuruhusu wanachama wengine kuingia katika safu ya uongozi. Uamuzi huu usionekane kuwa ni udhaifu au ni njia ya kuwalazimisha wengine kuufuata. Kustaafu nafasi ya uongozi kunaweza kufanywa na mtu yeyote pasipo kujali umri wake.
Azimio namba tatu linaeleza: “Kutetea raslimali za Taifa letu na utajiri wa nchi yetu kwa kukusudia kuzuia mikataba na mipango yoyote yenye kurundika utajiri wetu mikononi mwa wafanyabiashara wakubwa bila kujali maslahi ya leo ya Taifa au yale ya kizazi kijacho.
“Tunachukua msimamo huo tukiamini kuwa kama viongozi wa CCM tunalojukumu la kichama kueneza matunda ya Uhuru kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa jumla. Kwa mujibu wa Ibara ya 17:2 ya Katiba ya CCM. Jukumu hili si la wapinzani au wafadhili wa kigeni; ni jukumu letu kama Watanzania na kama wana CCM.”
Azimio namba nne: “Kupigania haki ya kila Mtanzania kugombania nafasi ya uongozi pasipo kulazimishwa kujiunga na chama cha siasa. Kama Watanzania kwanza na kama wana CCM, tunaamini haki ya kuchaguliwa isiunganishwe na ulazima wa kujiunga na chama
cha siasa kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vile vile kupingana na Tamko la Haki za Binadamu la 1948 ambalo Tanzania imeliridhia.
“Chama cha Mapinduzi na wana CCM hatuogopi wagombea binafsi, kwani tunaamini chama chetu kinakubalika, kina uwezo wa kuongoza bila kujali wagombea wengine wanatoka wapi au wanapatikana vipi.”
Azimio namba tano: “Kuhakikisha mfumo bora wa kuwajibika na kuwajibishana unakuwapo katika Serikali kwa kupendekeza mabadiliko ya Katiba na sheria mbalimbali ili hatimaye mfumo ambao umefungua milango ya kifisadi unakosolewa, kubomolewa na kubadilishwa na mfumo ambao hautatoa nafasi kwa watu na vikundi vya watu kuneemeka kwa kutumia mbinu za kifisadi.
“Bila ya kuubadili mfumo huu tunaamini mafisadi wataendelea kuibuka kati yetu na kama Taifa tutaendelea kupiga kambi kwenye hili bonde la ufisadi miaka nenda rudi. Ni lazima tuubadili mfumo huu tukizingatia vile vile malengo ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupamba na Umasikini namba mbili (MKUKUTA II).”
Katika hatua nyingine inayoweza kuhusishwa na juhudi za kundi mojawapo kati ya yanayopingana CCM, Chama Cha Jamii (CCJ) jana Jumanne kilipata usajili muda jana.
Chama hicho kama ilivyo kwa kundi hili linalojitambulisha kama wapiganaji wa kweli, kimekuwa kikihusishwa na baadhi ya vigogo wa CCM lakini ambao hawajajitokeza hadharani.
Hali hiyo ya kuhusishwa vigogo wa CCM na CCJ, na kisha kuibuka kwa kundi hili jipya la wapiganajii wa kweli, inatajwa kuchochewa na udhaifu wa kiuongozi ndani ya CCM.
Hata hivyo, wananchi wengi wamekuwa wakishangazwa na vigogo wanaodai wanapenda mabadiliko ndani ya CCM lakini waoga kujitokeza hadharani, ikielezwa kuwa kujificha huko ni udhaifu mkubwa kwa makundi hayo kwa kuwa huo si ujasiri unaostahili kuchochea mabadiliko nchini.
http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=2087

hs3.gif
 
MANI

MANI

Platinum Member
Joined
Feb 22, 2010
Messages
6,856
Likes
2,784
Points
280
MANI

MANI

Platinum Member
Joined Feb 22, 2010
6,856 2,784 280
Babylon waswahili husema, lisemwalo lipo kama halipo laja na dalili ya mvua ni mawingu vyote hivyo ndani ya ccm vimeonekana yetu ni subira tu.
 
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2008
Messages
1,322
Likes
21
Points
135
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2008
1,322 21 135
We need action now not matamko any more
 
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
2,707
Likes
267
Points
180
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
2,707 267 180
Hii mbona inafanana na iliyopo hapa (TAMKO RASMI LA WAPAMBANAJI WA UFISADI)
 
Pengo

Pengo

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2009
Messages
579
Likes
3
Points
0
Pengo

Pengo

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2009
579 3 0
uPUUUUUZIIIIIIIIIIIII MTUUUUUUUUUUUUUPUUUUUUUUUUUUUUUU
 
Lyangalo

Lyangalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2009
Messages
679
Likes
84
Points
45
Lyangalo

Lyangalo

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2009
679 84 45
Tumewisha wazoea wana CCM na wabunge wao, wakati wanachangia mada utasikia wanalalamika na kutoa sababu za msingi kabisa, lakini mwisho wa siku wanaunga mkono hoja 100%! Inashangaza eeeh! This is made in CCM!
 
PJ

PJ

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
297
Likes
2
Points
35
PJ

PJ

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
297 2 35
Tunataka mchukue action za kulete mabadiliko ya dharura kama walivyofanya wanajeshi kule Niger.

Muda wa kuzungumza umekwisha sasa ni wakati wa vitendo. Maneno matupu hayavunji mfupa kana alivyosema kikwete kuwa kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala. Hivyo maneno yenu yanaonekana na watawala kama wafa maji wanaotapatapa

Fanyeni jambo la wazi na la dharura sisi walalahoi ambao hatuna cha kupoteza ila minyororo yetu tutakuwa nyuma yenu
 
Mponjoli

Mponjoli

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
667
Likes
15
Points
35
Mponjoli

Mponjoli

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
667 15 35
Huu upuuzi wa kutaka kuuza magazeti yao,mtafaruku uliopo siyo mpya ni ule ule..
 
HeartBreak

HeartBreak

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2008
Messages
346
Likes
5
Points
33
HeartBreak

HeartBreak

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2008
346 5 33
nyerere alisema!!!! bora uwe masikini wa mali kuliko masikini wa akili......yaani ufahamu...sasa ccm iko na umasikini wa akili siku zote,nchi hii itachukuliwa na wenyewe tu.
 
Forum statistics

Threads 1,237,681
Members 475,675
Posts 29,297,247