Mbowe na Dkt Slaa wakikuhaidi njia inaelekea kulia lower your expectations na ukate kushoto. Wengi waliwahi kuwaamini kuwa wanaweza kuleta miujiza kwenye nchi yetu na tulishuhudia ni unafiki na usaliti wa hali ya juu.
Walisimama Mwembeyanga na list of shame mwaka 2007 wale waliowaita mafisadi kwa miaka 8 wakawapa nafasi ya kugombea Urais. Mbowe akaapiza over his dead body hawezi kumkataa yule waliyemuita fisadi kwa sababu ya Dkt. Slaa amemgomea (𝐣𝐢𝐮𝐥𝐢𝐳𝐞 𝐤𝐰𝐚𝐧𝐢𝐧𝐢? 𝐀𝐥𝐢𝐩𝐨𝐤𝐞𝐚 𝐩𝐞𝐬𝐚)
Unajiuliza kwa haraka Mbowe na Dkt. Slaa walikaa lini kuondoa tofauti zao ni Dkt. Slaa aliyemuita Mbowe ni Gaidi, Ni Dkt Slaa alikiri mbele ya hadhara Chadema kuna vikundi vya utekaji na ana uhakika kuwa kuna uwezekano aliyemshambulia Lissu kwa Risasi ni Chadema. (𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐮 𝐧𝐢 𝐳𝐢𝐥𝐞𝐳𝐢𝐥𝐞 𝐃𝐤𝐭. 𝐒𝐥𝐚𝐚 𝐚𝐦𝐞𝐥𝐞𝐭𝐚 𝐩𝐞𝐬𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐬𝐡𝐚𝐫𝐭𝐢 𝐧𝐚𝐟𝐮𝐮)
Tujiulize vile vikundi vya utekaji alivyovieleza Dkt. Slaa nani ameviondoa? Kwenye siasa hakuna adui wa kudumu ila wanasiasa ni wanadamu sababu Dkt Slaa anafanya mazungumzo na Mbowe kipindi ambacho Lissu hayupo? Huu ni mpasuko mkubwa.
Mbowe haioni sign ya chama kukataliwa na wananchi Temeke wamekataa kulishwa uongo mchana wa wazi anapokwenda kumpokea Dkt. Slaa ni kujichimbia kaburi la siasa zao ni rahisi kwa Wananchi kumsamehe mpinzani aliyekwenda chama tawala na ngumu sana kwa Wananchi kumpokea mpinzani aliyetoka chama tawala kurudi upinzani. (𝐖𝐚𝐬𝐚𝐥𝐢𝐭𝐢 𝐡𝐚𝐰𝐚𝐩𝐞𝐧𝐝𝐰𝐢 𝐝𝐚𝐢𝐦𝐚)
Rekodi zipo wazi kabisa, Wananchi wa Tanzania wanampenda shetani wanayemjua kuliko malaika wasiyemuona. kuanguka kisiasa kwa wapinzani waliokwenda chama tawala na kurudi chama pinzani ni kikubwa kuliko mpinzani aliyekwenda chama tawala.
Ni kambi mbili sasa ndani ya CHADEMA imani ya Lissu na Imani ya Mwenyekiti Mbowe, Jahazi limechanika tanga na bahari imechafuka. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar akiongea ni vipande vipande.
𝐍𝐢𝐦𝐞𝐤𝐚𝐚 𝐩𝐚𝐥𝐞...!!!
View attachment 2698788
View attachment 2698789