paradiso
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 1,021
- 356
Wakati kipenga cha uchaguzi wa udiwani kikitarajiwa kupilizwa kesho tarehe 15-may-2013 aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Themi Petro Ndarivoi ameamua kuhama ccm pamoja na wafuasi wake 400 kutokana na alichodai hujuma zilizofanyika ccm Mkoani Arusha kukata jina lake katika nafasi ya uwakilishi wa nafasi ya udiwani katika kata ya Themi.
Mwenyekiti huyu maarufu wa CCM aliyejiunga na CUF, katika uchaguzi wa ndani wa ccm alishinda katika kura za maoni lakini inasemekana CCM Mkoani Arusha wakagundua kuwa kijana huyu ni kambi ya Lowasa hasa ukizingatia na yeye ni maasai, kama kawaida Mulongo Magesa na Mary Chatanda kutoka kambi ya Membe wakahakikisha anatolewa haraka sana na picha zake zikabanduliwa upesi katika ofisi za ccm kata ya Themi/fire.
Katika hali ya kushangaza kambi hizi mbili ya Lowasa na Membe zimekuwa zikisababisha CCM kukosa viti vingi vya uwakilishi hapa Arusha kwasababu CHADEMA wanatumia 'vita ya panzi ' kuongeza viti vya udiwani katika halmashauri ya arusha.

Pichani ni aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Themi Petro Ndarivoi (Kulia) akirudisha kadi ya chama cha mapinduzi kwa mwenyekiti wa chama cha CUF halmashauri ya jiji la Arusha Hamza Mustaph kwenye makao makuu ya chama hicho jana jioni
My take:
ccm Arusha wamebaki hoi kwa mpasuko huu mkubwa hasa ukizingatia chadema wameanza maandalizi ya sherehe kwa uhakika wa kutwaa kata zote 4 za arusha mjini.