Mpapai na Gunzi vina uhusiano gani?

Kitaalam ni kwamba Carica papaya (mpapai) una tabia ya kubadilisha jinsia kulingana na physical stress kwa hivyo mpapai unavyokua mara nyingi kuna uwezekano wa kuwa wa kiume, kwa hvyo wakulima hufunga gunzi/ au kupigilia msumali nk wkati ukiwa mdogo hii hali inasababisha mechanical stress kwa mpapai ambao unarespond kwa kufanya resproductive hormone rearrangement na kubadili kuanza kuazalisha hormone za kike na hivyo hubadilika kuwa wa kike. Ki wastani mpapai mmoja wa kiume unaweza kuzalisha pollens za kuchavisha/kurutubisha mipapai ya kike 25 na kuendelea. Kwa hivyo unaweza kuona, wakulima wanahitaji mipapai ya kike kuliko ya kiume kwa ajili ya uzalishaji wa matunda.
 
Daaah mpapai unaogopa kudhalilika, unaamua kubadili jinsia.

Nimeshuhudia aisee inafungwa. Nilipohoji nilionyeshwa uliocheleweshwa kufungwa gunzi na haukuzaa, na uliowaishwa ulivyoanza kuzaa ukiwa mdogo. It real works aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni suala nililolisikia muda ila nimethibitisha baada ya mpapai kurefuka tu bila kuzaa nikaufunga gunzi ukazaa mapapai mawili, kutokana na mvua gunzi lilianguka, ukaacha kuzaa, ukafungwa gunzi tena sasa hivi una mapapai mengi tu.

Je, hili suala laweza thibitika kisayansi?
Ni coincidence tu.
 
Kitaalam ni kwamba Carica papaya (mpapai) una tabia ya kubadilisha jinsia kulingana na physical stress kwa hivyo mpapai unavyokua mara nyingi kuna uwezekano wa kuwa wa kiume, kwa hvyo wakulima hufunga gunzi/ au kupigilia msumali nk wkati ukiwa mdogo hii hali inasababisha mechanical stress kwa mpapai ambao unarespond kwa kufanya resproductive hormone rearrangement na kubadili kuanza kuazalisha hormone za kike na hivyo hubadilika kuwa wa kike. Ki wastani mpapai mmoja wa kiume unaweza kuzalisha pollens za kuchavisha/kurutubisha mipapai ya kike 25 na kuendelea. Kwa hivyo unaweza kuona, wakulima wanahitaji mipapai ya kike kuliko ya kiume kwa ajili ya uzalishaji wa matunda.
Kweli nimeshuhudia mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna mpapai jike na dume na ikiwa michanga huwezi kugundua jinsia yake, inaaminika ukifunga gunzi ni sawa na mama amebeba mtoto mgongoni kwa mbeleko. Mwanaume wa ukweli hawezi kubeba mtoto mgongoni kwa mbeleko na huo mpapai Kama ulikuwa na mpango wa kuwa mwanaume utaona bora tu uwe mwanamke uzae kuliko kujidhalilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
R
 
Wakuu hiyo imesibitishwa kisayansi.. Ipo hivi kuna mipapai dume (male plant) hii haizai matunda, na kuna mipapai jike (female plant) na yenye jinsia zote mbili (hermaphrodite) hii ndio inayozaa matunda isipokua dume tu! Sasa kuna mimea inaweza kubadili jinsia yake (sex labile plant) moja wapo ni mipapai na inabadilika pale mazingira yatakapokua magumu kwa yenyewe kuishi sasa ili uendeleze kizazi chake ni lazima ubadilike kutoka dume kuwa jike ile uweze kuacha kizazi chake

Kufunga bunzi/gunzi ni watu wameaminishwa tu ila unaweza kufunga chochote kile ata ukipigilia misumari ilimradi mmea upate shuruba (stress) hapo mmea utahisi kuwa upo kwenye mazingira magumu na unaweza kufa muda wowote . Hapo mmea utachukua hatua ya kubadili jinsia na kuzaa matunda haraka sana kabra haujafa ili uache kizazi chake.. kama binadamu tu akinusurika na ajari utasikia sina hata mtoto.

Siku moja tu ya uumbaji ila mimea ina physiology nyingi na zakustaajabisha!

Sent from my iPhone using JamiiForums
Binafsi sikuamini kwenye Gunzi, ila Kutokana na maelezo yako, nina Mpapai Dume hapa kwangu, Ngoja niupige msumali nione matokeo.
 
Kigunzi kinaashiria dushe ambalo mpapai unatafuta kabla ya kutoa maua, hivyo ukilipa mpapai dushe (gunzi) linaacha papara na kuanza kuzaaa na hindi.
 
Ilikua dume nikatoa maoteo machanga zaidi ya mara5 huku nikiwa nimefunga gunzi hatimaye umetoa maua ya mapapai
IMG_20200411_144218.jpeg
IMG_20200411_144154.jpeg
IMG_20200411_144204.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna mpapai jike na dume na ikiwa michanga huwezi kugundua jinsia yake, inaaminika ukifunga gunzi ni sawa na mama amebeba mtoto mgongoni kwa mbeleko. Mwanaume wa ukweli hawezi kubeba mtoto mgongoni kwa mbeleko na huo mpapai Kama ulikuwa na mpango wa kuwa mwanaume utaona bora tu uwe mwanamke uzae kuliko kujidhalilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kuustress na ndio mwisho unahama jinsia mkuu
 
Yes, pruning is the reliable scientific method but there are several cases when corn(maize) cobs managed to turn a male Papaya tree into a female tree.

Probably corn cobs contains certain enzymes or organic chemicals which turns male papaya tree into a female or hermaphrodite papaya tree when the two gets in contact for several days.
ni vingi ambavyo ukibhana shina la mpapai tissue zinakuwa stressed zinapelekea kuhama jinsia na sio kwa mpapai na hata mnazi.
njia kama kuchoma msumari,kugonga kigunzi (corn cob) na kufunga waya shina hivyo kwenye transportation ya mmea huathiriwa na ndio this is what we call plant stress and the response in turn inaonekana kuna mechanisms zinatokea zinahamisha jinsia nimesahau jina la process ila ni something "LIBIDOS"
 
Nakubaliana na maelezo yako 100%.
Ni jibu la kisayansi kabisa.
Again, Ahsante kwa ufafanuzi mzuri sana.
 
Imani nyingine iliyopo ukiupigilia msumari kwa chini wanadai papai halidondoki adi utungue mwenyewe, mama yangu amefanya hivyo, papai linaiva adi linaozoe juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom