===>Mimi huwa najiuliza kitu kimoja hivi akija Katibu Mkuu Mtendaji Muislamu pale NECTA hawa ndugu zetu watapata wote Div I,II au III?
===>Au atahakikisha kuwa vijana wao woote wanapewa MADESA ili wafaulu?
===>Ushauri wa bure kwa ndugu zangu waislamu,jaribuni kuwatafuta walimu wanaokwenda kwenye kusahihisha mitihani wawaambie uhalisia ukoje kabla ya kukurupuka kutoa haya Matamko na nyaraka zenye jazba
===>Boresheni mazingira na ubora wa shule zenu kuanzia kutafuta walimu wazuri,uongozi bora wa shule zenu.
===>Wekezeni kwenye Elimu,msilete maskhara na suala la Elimu,hakuna mtu atakaewalazimisha watoto wenu wakasome kama sio nyie wenyewe wazazi.
===>Panueni wigo wa udahali,miundombinu na vyuo vishirikishi vya Chuo chenu cha Morogoro,chuo kile tangu kilipoanzishwa hakina hata tawi moja mikoani hata Dsm hakuna,mnataka mkajengewe pia kile chuo?
===>Ndugu zangu waislamu mna uwezo mkubwa sana wa kifedha,wapo ndugu zenu kama wakina Bakhresa,Mohamedi Dewji na wengineo fanyeni harambee mpate pesa,mzisimamie vizuri na muwekeze kwenye Elimu,huduma za afya na maeneo mengine naamini mnaweza kufanya makubwa kuliko hata waliyofanya wakristo
===>Mungu awatie nguvu,naamini nitakuwa nimetoa angalau kamchango kangu japo kadogo lakini kanaweza kusaidia.