Mpango wa kuanzishwa magari ya cable kupanda mlima Kilimanjaro

Mpango wa kuanzishwa magari ya cable kupanda mlima Kilimanjaro

Ni kweli cable cars itaongeza idadi ya watu watakaopanda Kili. Na watu wakiziidi uharibifu wa mazingira itazidi pale juu. Pale kwenye summit ni alpine environment, na mimea zinachukua muda mrefu kustawi. Watu wakikanyaga hovyo ndio mwisho wa mimea. Kuzidi kwa utalii mara nyingi inakuwa laana! Miji kama Venice wamegundua hilo na sasa wanatafuta mbinu ya kupunguza idadi ya watalii.
 
Idadi ikiwa kubwa ya watalii wa nje na ndani watapanda mlima, kutakuwa na biashara nyingine nyingi zitaongezeka kwenye vituo vya kupandia na kushukia. nchi nyingi zimefanya hivi, ingawa pia wanaotaka kupanda kwa miguu waachiwe waendelee.Ni wazo zuri.
Watalii wa ndani wengi nia itakuwa kupanda hayo magari wala si kufika kileleni. Ni burudani kwa sisi wananchi ila nauli iwe fair.
 
Tanzania Kwasasa Ni Tajiri
Hilo Litafanyika Haraka Sana
 
Bei ya bidhaa kama mbege itaongezeka sana !!!!!
Idadi ikiwa kubwa ya watalii wa nje na ndani watapanda mlima, kutakuwa na biashara nyingine nyingi zitaongezeka kwenye vituo vya kupandia na kushukia. nchi nyingi zimefanya hivi, ingawa pia wanaotaka kupanda kwa miguu waachiwe waendelee.Ni wazo zuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila kuna Adventure flani hivi katika kuuupanda mlima kwa miguu, huoni hiki ni kigezo cha kuAttract watalii wengi sana bongo? plus the more they stay the more tunapiga hela....pia am sure cable cars wanazo uko nje, sasa kuja bongo nahisi ni vzuri wakute vitu tofauti ili iwe more interesting
Sio watalii wote wanaweza panda kwa miguu nazan ni option nzuri kwa wazew na wenye physical challenges kutimiza ndoto zaokupanda mlima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ina mpango wa kuanzisha CABLE-CARS yaani magari ya cable kupanda mlima kilimanjaro, ila mpaka sasa wapo baadhi ya wadau wanaopandisha watu/wageni kwenye mlima huo (Kumbuka hawa watu hulipwa), sasa huu mpango wao naona utakua umeteka soko la ajira kabisa kwa local industry....

View attachment 1065458

Ingawa huu mpango utaongeza idadi ya wapandaji mlima, ila pia itapunguza muda wa watalii kukaa Tz cus itakua ni day trip tofauti na zamani ilivyokua wanatumia siu mpaka siku kupanda mlima huo...

vip wadau kuhusus hili swala mnahisi Serikali imeingia 'chaka' au huu mpango unafaida?
karibuni kwa maoni....


Hii itasaidia kuwapa watalii nafasi ya kutembelea vivutio vingi zaidi kwa kutumia muda watakaookoa kutokana na kupanda mlima Klm kwa hiyo teknolojia
 
Hivi hapo utakuwa umepanda mlima au umepandishwa? Yaani bado ukishuka utajisifu kuwa nishapanda mlima? Kweli???? Labda wafanye hizo cars ziwe very expensive

Sent using Jamii Forums mobile app


Itakuwa sawa na mtu anayesema nimefika ulaya na marekani, kiuhalisia amefikishwa
 
Hii italeta ufanisi mkubwa tu katika industry hii ya tourism kwani hata vikija hivyo vigari bado nafasi pia itakuwepo kwa watu watakotaka kupanda kwa miguu hivyo tourguides bado watakuwa na nafasi japo inawezekana ikawa kwa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila kuna Adventure flani hivi katika kuuupanda mlima kwa miguu, huoni hiki ni kigezo cha kuAttract watalii wengi sana bongo? plus the more they stay the more tunapiga hela....pia am sure cable cars wanazo uko nje, sasa kuja bongo nahisi ni vzuri wakute vitu tofauti ili iwe more interesting
The ideq ni ku conquer the Kili sio kama scenic tour.
Huko wanakotumia cable ni sehemu za pass kwenye hiyo vijilima vyao sio kama the mighty kilimanjaro.
Huo mpango hata mm nitaupinga hata mimi hawawezi kuifanya Mount Kilimanjaro like a walk in the park.
Muhimu watafute namna ya kupunguz gharama na kuweka ufanisi sio kurahisisha rahishisha kama jando la vijana wa sasa no pain no maadili just nothing to remember na wengine hata hawajui kama mwanamme anazaliwa akiwa na govi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hapo utakuwa umepanda mlima au umepandishwa? Yaani bado ukishuka utajisifu kuwa nishapanda mlima? Kweli???? Labda wafanye hizo cars ziwe very expensive

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo cars zikiwa expensive ndio utakua umepanda mlima na sio kupandishwa??

Very Pathetic.
 
Back
Top Bottom