Mpango wa CCJ kumtumia Nyerere wakwama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpango wa CCJ kumtumia Nyerere wakwama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,914
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  CHAMA cha siasa chenye usajili wa muda cha CCJ (Chama Cha Jamii), kimeondokana na mpango wa kutumia picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwenye kadi zake za uanachama...

  Hatua hiyo imesababisha chama hicho kichapishe kadi mpya tofauti na za awali zilizokuwa na picha ya Rais wa Kwanza wa Tanganyika na Tanzania.

  Awali kadi hizo zenye rangi ya njano, zilikuwa na picha ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mistari miwili ya rangi ya kijani na bluu pamoja na michoro ya familia ya baba, mama na mtoto.


  Akizungumzia hatua hiyo jana, Katibu Mkuu wa CCM, Renatus Muabhi alikiri awali kuwa na picha ya Mwalimu, lakini iliondolewa baadaye kutokana na ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa.


  “Ni kweli tulikuwa na picha hiyo kwenye kadi zetu za uanachama kwa maana ya kumuenzi na kuunga mkono juhudi za Baba wa Taifa kulikomboa Taifa hili, lakini kabla ya kupata usajili wa muda, Msajili alituita na kutwambia tuiondoe,” alisema Muabhi.


  Hata hivyo alilalamikia kitendo cha Msajili kuwataka waiondoe sura ya Baba wa Taifa kwenye kadi hizo, akishangaa kuwa awali wakati wanawasilisha maombi ya usajili ofisini kwake, Tendwa aliiona na kuwakubalia.


  “Wakati tunawasilisha maombi yetu, tulimpelekea na sampuli ya kadi lakini hakuwa na kipingamizi, lakini muda mfupi kabla ya kutupa usajili wa muda, alituita tena bila barua na kutushauri kuiondoa picha hiyo.


  “Alitwambia kuwa eti CCM wanalalamika kuwa Mwalimu alikuwa mwanachama wao, hivyo isingekuwa vizuri sisi kuitumia picha yake katika kadi zetu za uanachama,” aliongeza.


  Pamoja na hatua hiyo, alisema kadi mpya zisizo na picha ya Mwalimu ziko tayari na kuwataka wanaopenda kujiunga na chama hicho waende katika ofisi za makao makuu yaliyoko Mwananyamala karibu na hospitali ya Wilaya Kinondoni, wakakate kadi za uanachama.


  “Hatukati tamaa na tumeshachapisha zingine na yeyote anayehitaji aje na tunaziuza kwa Sh 500, lakini kwa wasio na uwezo, tunaweza kuwapa hata bure ili wajiunge na chama hiki,” alisema.


  Si kawaida kwa kadi ya chama cha siasa kuwa na picha ya mtu au kiongozi wa chama chenyewe na pengine ndiyo sababu Msajili akawazuia kutumia kadi kama hizo, ingawa pia hatua hiyo ingeweza kuleta mtafaruku baina ya wafuasi wa CCM na CCJ.


  Alipoulizwa sababu hasa za kutumia picha hiyo kwenye kadi ya uanachama, Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo, alisema ufafanuzi kuhusu hilo, utatolewa kabla ya Machi 14 mwaka huu, ingawa hakutaka kusema ni lini hasa utatolewa.


  Hata hivyo, alifafanua kuhusu rangi katika kadi yao kuwa njano inamaanisha utajiri wa nchi hususan wa madini, kijani ni uoto wa asili, bluu ni maji na familia ni Watanzania.


  CCJ ilipata usajili wa muda hivi karibuni baada ya kusababisha mtafaruku miongoni mwa wanasiasa nchini, kikidhaniwa kuwa ni chama kitakachoigawa CCM kwa kuchukua vigogo ambao hawakubaliani na mwenendo wa chama hicho tawala.


  Hata hivyo, uongozi wa chama hicho kipya umekuwa ukishikilia kuwa hakina uhusiano wowote na vigogo wa CCM wala mpango wa kuwachukua na kinajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu.


  Juhudi za kumpata Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Tendwa, kuzungumzia suala la picha ya Mwalimu kwenye kadi za uanachama, zilishindikana jana kutokana na simu yake kutopatikana.


  CHANZO: HABARI LEO
   
 2. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kuna tetesi kuwa makao makuu ya Chama kipya cha Jamii (CCJ) kilichopata usajiri wa muda hivi karibuni yatakuwa Butihama, Musoma. Sina uhakika na habari hizi, hivyo naomba wanaJF wenye data watupe ili kupata mwanzo wa kujadili hoja itakayoenda sambamba na makao makuu ya chama hicho kuwa huko Butihama.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  khee yale yale ya kuwa CCJ ni zao la kongamano la MWALIMU foundation sitashangaa nikija sikia madaraka nyerere ndo mwenyekiti wa kitaifa wa CCJ
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Hiyo picha ndo iko wapi sasa?
  Au we ni kizazi cha dot.com mtandaoni!
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Watashindwa kupata watu siku zote mageuzi yananzia mijini sasa style yao sio nzuri sana
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,440
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Hii thread mbona ipo kwenye Jamii Photo? Picha yenyewe wapi?
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kweli mkuu. Hii inatakiwa iende kule kwenye jukwaa la siasa.
   
 8. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ni kweli wakuu nilitakiwa niiweke kwenye jukwaa la siasa. Sorry for any inconvinience!!!
   
 9. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #9
  Mar 8, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,013
  Likes Received: 1,217
  Trophy Points: 280
  Kwamba Makao Makuu ya CCJ yatakuwa Butiama,mimi bado zijazisikia habari hizi. Navyofahamu mimi watu wa Butiama ni CCM damu damu,CCM dyed-in-the-wool. Katika Uchaguzi uliopita yule Chief aliwaunga mkon CHADEMA, akajikuta yuko peke yake.
  In brief,iwapo CCJ wakitaka kuweka Makao Makuu yao Butiama,sidhani kama itakuwepo legal problems,sispokuwa tu complaints za wakazi wa pale.
  Mimi sioni sababu yoyte ya kutoa maoni kuhusu CCJ. CCJ wanataka kuwa mysterious at this point in time. I have no objection to that. They can speak out when they are ready,kutueleza what is their policy on education,on Foreign Affairs,on Darfur,on the economy.
   
 10. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilisoma mahali kwamba ofisi za CCJ ziko Mwananyamala Kinondoni. Bila shaka ndio Makao Makuu yao kwa muda huu maana hapo ndipo wanapopatikana Mwenyekiti na Katibu wake na hapo kadi zinauzwa/kutolewa bure (kwa wasio na uwezo wa kununua).
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...