Mpango mmojawapo wa siri wa uchakachuaji huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpango mmojawapo wa siri wa uchakachuaji huu hapa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Candid Scope, Nov 16, 2010.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mambo ambayo hatuna budi kuwa makini nayo ni yale yaliyotokea huko Shinyanga ambako mipango ya siri ya uchakachuaji matokeo ya uchaguzi kwa njia ya siri yalikamatwa lakini mpaka leo hakuna taarifa zinazoendelea kutokea.
  Mmoja ya mpango ulioshikwa ni biashara ya kununua hati za wapiga kura. Mpango huo ni hatari unaofanywa kwa siri hasa unaweza lenga kununua shahada za wanachama au watu wanaomwunga mkono mgombea fulani ili kudhoofisha idadi inayoweza kufikia kiwango cha kutangazwa mshindi. Huko shinyanga ni wakereketwa wakubwa wa haki kwani inawezekana sehemu nyingi mpango huo ulifanyika.
  Ingefaa bunge la sasa lipitishe sheria inayomtia hatiani ye yote anayenunua au kuuza hati yake ya kupiga kura, na kama akigundulika hana hati hiyo anatakiwa atoe ufafanuzi wapi kaipeleka, na kama imepotea lazima atoe taarifa muda si zaidi wa mwezi kituo cha polisi vinginevyo itaeleweka hati imeuzwa. Na haiingii akilini mwangu wengi wapotelewe na hati za kupiga kura kipindi cha kampeni za uchaguzi.
  Mpango huu ni dhahiri kutokana ni siku za nyuma zilikutwa shahada nyingi zikichomwa moto ambazo zilihifadhiwa katika ghala moja huko Dar, sikumbuki sehemu kamili lakini nadhani ni wilaya ya ilala. Kwa maana hiyo mpango huo umezoeleka katika kipindi hiki cha mchuano wa wagombea toka vyama vingi kuomba kura na hivyo kuwa maarufu kwa wale wenye uwezo na hivyo kufanikisha kitu ambacho ni kinyume cha ridhaa ya kukuza demokrasia na maendeleo ya taifa.
  Kwa maana hiyo ni muhimu kuunganisha vipande vipande vya matukio na kupata tukio zima au zoezi zima linavyoshamiri kama mafundi watengenezaji wa kanda za movie.
  Nategemea wana JF kuchangia hoja yangu ili kujipanga upya na kikamilifu kwa ingwe ya 2015 mwaka wa ukombozi. :israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel:
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dawa ya hivyo vitu ni kuondoa vitu viwili tu kwa hao watu wa shinyanga navyo ni

  i) Umaskini na
  ii) ujinga

  Vitu ambavyo chini ya hii serikali ya hawa mapoyoyo si dhani kama ndugu zangu watavipata
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Ssa wamechoma mchakachuo kesi zikianza si itakuwa ushindi wa moja kwa moja kwa Slaa???
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  digressing; interesting, historical name, candid scope!
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye RED.Sheria zilizopo zinatosha ila kinachotakiwa ni mtu wa kusimamia sheria. Fikiria TAKUKURU kama wanafanya kazi yao. Kumbuka sheria za gharama za uchaguzi. Unadhani sheria hizi zinasadia chochote zaidi ya kulinda uovu? Kwa hiyo hata ikiwepo sheria ya aina hiyo na watu wakamtiwa hatiani wanaonunua kura kwa taarifa yako hakuna atakayetiwa hatiani bali utasikia usanii wa kila aina.
   
Loading...