Mpangaji mwenzangu ananiroga!

Mpangaji mwenzangu ananiroga!

Habari za asbh wana JF,

Napenda kuwaambia kuwa kuishi na mpangaji mwenzio alafu anakuonea wivu wa kimaendeleo ni shidaaa. Wiki 2 mbili sasa kichwa hakiachi kuuma, nimekwenda Hospital mara kadhaa bt sikupata nafuu ndipo nilipoona nijaribu kwa Sanonga(mganga wa kienyeji) ndipo aliponieleza kuwa mpangaji mwenzako anakuroga coz mimi nafanikiwa na mambo yangu.

Sasa je nimfanye nini huyu mpangaji mwenzangu? Au na mimi nimmalize kabisa?

Cc mshana jr hebu njoo saidia huyu mlipa kodi..
 
Usipende sana kuamini kila unacho ambiwa jaribu tena tiba za hospitali,Waganga wanatumia saikolojia tu ukichunguza kwa makini itakuwa wewe ndio ulimwambia mganga kuwa mpangaji mwenzio ndio mchawi.
 
Mganga alijuaje kuwa umepanga na una mpangaji mwenzio?
Bila shaka ulimpa stori kwanza kwa kujijua kuwa unampa stori au kwa kutokujijua kuwa unampa kabla hajatoa hukumu, na sasa kaitumia hiyo stori yako kukupa jibu, ingawa si kweli! Wewe ni unaumwa tu kichwa cha kawaida wala si cha kutogwa sababu hamna kitu kama hicho, na pia imani yako ndo inayoumiza kichwa, imani ya kuwa umerogwa ma mpangaji mwenzio.
 
Ila mambo ya kurogana yapo sana kwenye nyumba za kupanga,me nakumbuka nilikuwa nafanyiwa urozi na mama mwenye nyumba kisa siwachapi mabinti zake,kwahiyo nilikoma mazee
 
Naona wewe unajiroga...Nenda hospital pengine una upungufu wa damu au upungfu wa maji
 
Habari za asbh wana JF,

Napenda kuwaambia kuwa kuishi na mpangaji mwenzio alafu anakuonea wivu wa kimaendeleo ni shidaaa. Wiki 2 mbili sasa kichwa hakiachi kuuma, nimekwenda Hospital mara kadhaa bt sikupata nafuu ndipo nilipoona nijaribu kwa Sanonga(mganga wa kienyeji) ndipo aliponieleza kuwa mpangaji mwenzako anakuroga coz mimi nafanikiwa na mambo yangu.

Sasa je nimfanye nini huyu mpangaji mwenzangu? Au na mimi nimmalize kabisa?
Avatar yako inaonekana na wewe ni walewale!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom