Mpanda: Tundu Lissu ayalipua Maridhiano, Kingai, Byakanwa na Wambura Watajwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,788
218,420
Katika Muendelezo wa Mikutano ya hadhara inayoendelea kwenye Oparesheni 255 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , ambayo sasa imeingia kwenye Mkoa wa Katavi, Tundu Lissu ameyataja mapungufu ya Maridhiano hadi sasa.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya Maelfu ya wananchi Lissu amesema kwamba , maana halisi ya maridhiano ni kuhakikisha kwamba Makandokando ya awali yaliyotokana na utawala wa kikatili wa awamu ya 5 yanaondolewa na kuanza ukurasa mpya.

Bali anashangazwa na kitendo cha washirika wa makandokando hayo kuendelea kupewa vyeo tena katikati ya naridhiano , Amemtaja IGP Camillius Wambura kama mpishi mkuu wa kesi zote za uongo zilizomkabili yeye mwenyewe , ambazo zimetupiliwa mbali mahakamani , anadai hakuna asiyejua upishi wa kesi za uongo wa Wambura , lakini aliteuliwa IGP

Tundu Lissu amefunguka kwamba Byakanwa ndiye aliyeharibu miundo mbinu ya Shamba la Kisasa la Freeman Mbowe , baada ya hapo akala shavu na kuwa RC wa Mtwara , na sasa ameteuliwa Balozi .

Lissu Amemtaja Ramadhan Kingai kama Mhalifu aliyetunga kila uongo kwenye kesi ya Ugaidi wa uongo iliyomkabili Mbowe, hata baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali Kingai akapandishwa Cheo , Lissu amedai kwamba katika wahalifu wa awamu ya 5 ni Sabaya Pekee aliyejaribu kushughulikiwa.

Tundu Lissu amependekeza Maridhiano ni lazima kweli yazingatie kuondoa matatizo pamoja na walioyaleta .
 
SAHIHI KABISA, HAKUNA MARIDHIANO YOYOTE, SAMIA ANATAKA cHADEMA ISIMSEME, LKN NIA YA DHATI YA MARIDHIANO HAIPO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…