Mpanda: Tundu Lissu ayalipua Maridhiano, Kingai, Byakanwa na Wambura Watajwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,476
215,319
Katika Muendelezo wa Mikutano ya hadhara inayoendelea kwenye Oparesheni 255 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , ambayo sasa imeingia kwenye Mkoa wa Katavi, Tundu Lissu ameyataja mapungufu ya Maridhiano hadi sasa.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya Maelfu ya wananchi Lissu amesema kwamba , maana halisi ya maridhiano ni kuhakikisha kwamba Makandokando ya awali yaliyotokana na utawala wa kikatili wa awamu ya 5 yanaondolewa na kuanza ukurasa mpya.

Bali anashangazwa na kitendo cha washirika wa makandokando hayo kuendelea kupewa vyeo tena katikati ya naridhiano , Amemtaja IGP Camillius Wambura kama mpishi mkuu wa kesi zote za uongo zilizomkabili yeye mwenyewe , ambazo zimetupiliwa mbali mahakamani , anadai hakuna asiyejua upishi wa kesi za uongo wa Wambura , lakini aliteuliwa IGP

Tundu Lissu amefunguka kwamba Byakanwa ndiye aliyeharibu miundo mbinu ya Shamba la Kisasa la Freeman Mbowe , baada ya hapo akala shavu na kuwa RC wa Mtwara , na sasa ameteuliwa Balozi .

Lissu Amemtaja Ramadhan Kingai kama Mhalifu aliyetunga kila uongo kwenye kesi ya Ugaidi wa uongo iliyomkabili Mbowe, hata baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali Kingai akapandishwa Cheo , Lissu amedai kwamba katika wahalifu wa awamu ya 5 ni Sabaya Pekee aliyejaribu kushughulikiwa.

Tundu Lissu amependekeza Maridhiano ni lazima kweli yazingatie kuondoa matatizo pamoja na walioyaleta .
 
Katika Muendelezo wa Mikutano ya hadhara inayoendelea kwenye Oparesheni 255 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) , ambayo sasa imeingia kwenye Mkoa wa Katavi , Tundu Lissu ameyataja mapungufu ya Maridhiano hadi sasa.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya Maelfu ya wananchi Lissu amesema kwamba , maana halisi ya maridhiano ni kuhakikisha kwamba Makandokando ya awali yaliyotokana na utawala wa kikatili wa awamu ya 5 yanaondolewa na kuanza ukurasa mpya.

Bali anashangazwa na kitendo cha washirika wa makandokando hayo kuendelea kupewa vyeo tena katikati ya naridhiano , Amemtaja IGP Camillius Wambura kama mpishi mkuu wa kesi zote za uongo zilizomkabili yeye mwenyewe , ambazo zimetupiliwa mbali mahakamani , anadai hakuna asiyejua upishi wa kesi za uongo wa Wambura , lakini aliteuliwa IGP

Tundu Lissu amefunguka kwamba Byakanwa ndiye aliyeharibu miundo mbinu ya Shamba la Kisasa la Freeman Mbowe , baada ya hapo akala shavu na kuwa RC wa Mtwara , na sasa ameteuliwa Balozi .

Lissu Amemtaja Ramadhan Kingai kama Mhalifu aliyetunga kila uongo kwenye kesi ya Ugaidi wa uongo iliyomkabili Mbowe , hata baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali Kingai akapandishwa Cheo , Lissu amedai kwamba katika wahalifu wa awamu ya 5 ni Sabaya Pekee aliyejaribu kushughulikiwa.

Tundu Lissu amependekeza Maridhiano ni lazima kweli yazingatie kuondoa matatizo pamoja na walioyaleta .
SAHIHI KABISA, HAKUNA MARIDHIANO YOYOTE, SAMIA ANATAKA cHADEMA ISIMSEME, LKN NIA YA DHATI YA MARIDHIANO HAIPO
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom