Mpambano Arumeru ni kama Fallujah: Mwanzo wa Safari ya CDM kuelekea 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpambano Arumeru ni kama Fallujah: Mwanzo wa Safari ya CDM kuelekea 2015

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 26, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kita cha Pili cha Fallujah kule Iraq mwaka 2004 kwa Wamarekani kilikuwa ni mpambano ambao ungeamua matokeo ya vita ya Iraq. Baada ya uvamizi wa Wamarekani katika kumuondoa Sadam Hussein wapiganaji wa Kiiraq walianza mapambano ya mijini (urban warfare) wakitumia mbinu na njia mbalimbali. Hata hivyo, hakuna mpambano mkubwa ambao wapiganaji wale wa Kiiraq walifanikiwa sana kama kuchukua eneo la Fallujah kutoka kwa Wamarekani na washirika wake mapema mwaka 2004 mwezi Aprili.


  Mji wa Fallujah ulikuwa ni miongoni mwa miji ambayo ilikuwa imependelewa wakati wa Sadam na wakazi wake wengi walikuwa ni watumishi kwenye vyombo mbalimbali vya usalama. Hata baada ya Wamarekani na Washirika kuingia Fallujah haikuhofiwa sana kuwa na waasi na hivyo vikosi vya wavamizi havikuwa kwa wingi katika mji ule hasa baada ya kuwa na kiongozi wa mji ambaye alionekana anawahusudu Wamarekani.  Matukio kadhaa yaliyowagonganisha wakazi wa Fallujah na askari wa Wamarekani yaliwafikisha pale ambapo watumishi 4 wa kampuni ya Ulinzi ya Blackwater walipouawa na miili yao kuning'inizwa kando yam to Euphrates. Hakukuwa na shaka kwa wataalamu wa Inteligensia kuwa Fallujah ilikuwa imeshikiliwa na wapiganaji wa Kiiraq. Kamandi ya Kijeshi ya Wamarekani wakaamua kuandaa kampeni ya kijeshi ya kwenda kuwaondoa wapiganaji wale na kuleta amani katika Fallujah.
  Aprili 1 mwaka 2004 Gen. Mark Kimmit alitangaza nia ya Wamarekani kuhakikisha kuwa Fallujah inatulia. Mipango ya kampeni ya kijeshi ilianza kwa umakini mkubwa. Mwezi Mmoja baadaye (Mei 1, 2004) Wamarekani walijikuta wameshindwa kuleta amani, na mipango yao yote ya kuwatumia Wairaq wenyewe kuleta amani imeshindikana, silaha walizowapatia Wairaq hao zikiangukia mikononi mwa waasi na amri ya kujiondoa (withdraw) kutoka Fallujah ikatolewa na mji wa Fallujah kwa asilimia 100 ukarudi mikononi mwa wapiganaji wa kikundi cha Sheikh Muktadar Al Sadr. Kwa wapiganaji wa Jeshi la Mahdi ulikuwa ni ushindi mwororo. Hata hivyo walijitambua kuwa Wamarekani wangepanga siku nyingine kujaribu tena. Hicho kilikuwa ni kita (battle) cha kwanza cha Fallujah.


  Kita cha pili cha Fallujah
  Miezi ilipita wakati Wamarekani na Washirika wake pamoja na vikosi vya Kiiraq wakijipanga kuichukua Fallujah. Muda wote Wamarekani wanajipanga wapiganaji wa Al Sadr nao walikuwa wanajipanga kwa kile ambacho tunaweza kukiita ni mpambano wa mwisho (the final confrontation). Siyo lengo langu kuangalia siasa za vita hivyo nzima ya Iraq au kuangalia masuala mengine zaidi ya kuangalia mipango ya kivita tu ya taifa lenye nguvu zaidi linapolazimishwa kupigana mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba na wapiganaji wasio na jeshi! Hadi leo hii mpambano wa Fallujah ndio ulikuwa mpambano mkali zaidi wa vita nzima ya Iraq na wanahistoria wa mambo ya kivita wanataja mpambano huo kuwa uliandika upya kitabu cha vita vya mjini (urban warfare).


  Ilikuwa Novemba 8 katika kile kilichoitwa Operesheni Ghadhabu Isiyoonekana (Operation Phantom Fury) ndipo vikosi vya Wamarekani wakiongozwa na Marines walipoanza kuishukia Fallujah. Walitumia nguvu zote walizokuwa nazo, utaalamu wote na mbinu zote za kijeshi. Waingereza walipeleka askari 13000; Wamarekani 6500 na Jeshi la Iraq wapiganaji 1500. Upande wa waasi kulikuwa na wapiganaji kati ya 3000-4000 hivi.


  Mwisho wa kita kile yaani Disemba 23, 2004 mambo kadhaa yalikuwa wazi; ilikuwa ni mpambano mkali zaidi ambapo vikosi vya Wamarekani vimewahi kuona tangu Vietnam huku askari wake 95 wakiuawa na 560 wakijeruhiwa. Nguvu ya waasi wote ilivunjwa pale na licha ya majaribio ya vikosi vya waasi kujipanga tena hakukuwa na mafanikio yoyote. Pamoja na majaribio mengine Wamarekani wakawa wamejifunza kupigana mtaa kwa mtaa, na kwa kumzidi adui kwa namna ya kipekee. Tofauti zote za kisiasa au kimtazamo za makamanda wale hazikuwa wazi kwani walijua walichokuwa wanapigania na ni kutoka katika mafunzo ya Fallujah, vita vya Ramadi na maeneo mengine yaliweza kuzuiliwa kuangukia mikononi mwa waasi. Miaka mitatu baadaye Fallujah ikarudishwa kwa utawala wa kiraia wa Wairaq mwishoni mwa 2007.


  CHADEMA na Arumeru Mashariki
  Kwa maoni yangu hakuna mpambano muhimu sana kwa CHADEMA katika historia yake yote ya kisiasa kama kiti cha Arumeru Mashariki. Nimeandika mahali pengine kwa nini hili ni kweli lakini itoshe kusema hapa kuwa CCM na Serikali yake watapeleka nguvu na uzoefu wao wote. CCM haitaki kushindwa na hautoshindwa kirahisi. Mfanano ninaouzungumzia hapa zaidi ni katika taswira ya kijeshi kati ya Fallujah na Arumeru Mashariki – kwamba sehemu zote mbili maslahi makubwa zaidi yanagombaniwa.


  CCM inataka kuonesha kuwa CHADEMA hakina ubavu wa kushinda uchaguzi mdogo na hivyo kina hamu na kiu ya kuendeleza rekodi yake ya kuinyanyasa CDM. CCM inaingia ikiwa na rekodi ya kutisha kabisa – haijalishi ilipatikanaje – ya kuweza kushinda chaguzi karibu nane mfululizo hata katika mazingira ambapo CDM walifikiriwa wangeweza kushinda. Hakuna mahali ambapo CDM walikuwa na harufu ya ushindi kama Igunga lakini matokeo yake tunakumbuka. CDM ikabakia kulalamikia mambo yale yale ambayo ililalamikia kuanzia Kiteto – shahada, polisi, serikali, vyombo vya habari n.k!


  Lakini kule Igunga CDM ilikuwa imemsimamisha mgombea ambaye kwa kweli alikuwa anajulikana zaidi na watu wa pale lakini hakuwa na umaarufu na ujiko wa Dr. Peter Kafumu. Kafumu alikuwa amelitaka jimbo la Igunga tangu 1994 na hivyo kwa baadhi ya watu walijua mapema kuwa ni mrithi "halali" wa Rostam Aziz. Lakini vile vile tuliona jinsi ambavyo CCM isingekubali jimbo la Rostam ambaye alikuwa anatajwa kuwa ni kinara wa ufisadi nchini liangukie upinzani kwani itakuwa ni uthibitisho wa wazi wa madai ya watu. Huko Arumeru Mashariki hata hivyo mgombea wa CCM hana sifa hizo – hana uzoefo, hajulikani na hana nafasi ya kutisha ndani ya chama au hata serikalini. Ni mgombea dhaifu zaidi ambaye amesimamishwa na CCM labda katika historia ya uchaguzi wake tangu Uhuru! Inapofika mahali CCM wenyewe wanasema ati wapiga kura wamchague tu "wasiporidhika naye watambadilisha mwaka 2015" maana yake ni kuwa hata wao ndani ya CCM wanajua kuwa wamemsimamisha mtu dhaifu.

  Lowassa tofauti ya CDM kushindwa au kushinda
  Licha ya kwamba mgombea wa CCM ni dhaifu hata hivyo hana udhaifu nyuma yake. Anakuja akiwa na silaha zote za CCM na anakuja pamoja na silaha inayosadikiwa kuwa na nguvu kubwa ya fedha na ushawishi yaani Edward Lowassa. Lowassa licha ya kuwa ni mkwe wa Siyoi Sumari vile vile ni mwanasiasa wa Arusha na anamaslahi mbalimbali huko Arumeru. Lowassa kama jemedari wa kisiasa hayuko tayari kushindwa Arumeru Mashariki. Atatumia mbinu mbalimbali na hakuna mbinu ambayo anaitumia vizuri sasa hivi kama vita vya kisaikolojia. Amekuwa kama jinamizi ambalo linatishia kuwa litaibuka wakati wowote!


  Ushindi wa CCM Arumeru Mashariki utakuwa ni pigo lisilo na utata kwa CDM. Watu wasifarijiane kwa kuridhishana kwa uongo kuwa CCM ikishinda basi CDM imejitahidi, au imekubalika zaidi au imepata mashabiki zaidi. Kushinda kwa CCM ni kutuma ujumbe kwa wapinzani kuwa hawana mbinu, ujuzi, mikakati wala uwezo wa kuzuia nguvu za CCM. Ni kama unyanyasaji wa aina fulani hivi – CCM imewashinda Kiteto, Biharamulo, Buchosa, Mbeya Vijijini, Tunduru, n.k CCM itaweza kusimama kwa fahari tu kuwa "hawatuwezi" na hakutakuwa na ubishi!


  Kushinda kwa CDM upande mwingine kutakuwa ni ushindi mkubwa wa kisaikolojia. Ni sawasawa na kumpiga Goliathi kwa Kombeo. Utakuwa ni ushindi ambao Vietnam iliupata dhidi ya Marekani licha ya kuzidiwa kijeshi kwa kila hali. Utakuwa ni ushindi ambao siyo tu utawapa nguvu CDM lakini utatuma ujumbe pande nyingine za nchi ambapo kutakuwa na chaguzi mbalimbali baadaye kuwa CCM inaweza kubwaga licha ya nguvu nyingi inazoweza kutumia.

  Lakini athari kubwa zaidi ya ushindi wa CDM Arumeru Mashariki itakuwa ndani ya CCM. Kutakuwa na kujichunguza kujua ni kwa nini walimsimamisha Siyoi, jinsi gani walifungua kampeni (maneno ya Mkapa) na hata mkakati wa kushindwa kujenga hoja zenye mashiko. Lakini pia kutakuwa na mgogoro wa wazi wa nafasi ya Lowassa ndani ya CCM kwani maoni ya wengi ndani ya CCM ni kuwa Siyoi amepewa nafasi hiyo si kwa sababu ya utii wake kwa chama au kujionesha kuwa ni kiongozi mzuri bali kwa sababu ya Lowassa, mkwewe. Ndio maana wapo wengine tunaoamini kuwa CCM imempa Lowassa kamba Arumeru ajimalize mwenyewe.


  Wiki ya CDM kuonesha ina mikakati nje ya mikutano ya hadhara
  Wamarekani waliweza kuichukua Fallujah baada ya kugundua kuwa ushindi hauji kwa kuwaangushia mabomu watu huku anayerusha mabomu hayo yuko kwenye meli baharini au mbali angani. Walitambua hakukuwa na ujanja isipokuwa kwenda nyumba kwa nyumba mtaa kwa mtaa na kuchafuka na kupigwa na kulipuliwa. Siku hizi zilizopita tumeona jinsi ambavyo CDM na viongozi wake wakishambuliwa na wakati mwingine wao wenyewe kushambuliana kuelekea mpambano wa Aprili Mosi. NInachokiona ni kuwa Arumeru ni muhimu sana kiasi kwamba wapo watu wanaoweza kusababisha mpambano wa wenyewe kwa wenyewe.


  Kazi kubwa ya viongozi wa CDM ni kujua ni wakati gani kujibizana ndani kwa ndani na binafsi nitafurahi nikiona viongozi makini wakikaa kimya kushambuliana na kutoingia kwenye mtego wa kuondoa macho yao kwenye zawadi. CDM wakianza tu kuzungumzia mambo mengine nje ya ushindi wa Arumeru Mashariki na sehemu nyingine wiki hii watapoteza nafasi hii adhimu kwao na kama nilivyosema mahali pengine ni lazima VIONGOZI WOTE WA KITAIFA wajiuzulu.


  Kutokuelewa uzito wa nafasi hii ya kihistoria ambayo kama Fallujah kwa Wamarekani ni kutoelewa historia vizuri. Ninaamini kabisa safari ya CDM 2015 inaanzia Arumeru Mashariki. Wakishindwa Arumeru Mashariki nafasi yao kwenda 2015 itakuwa ni ile ile ya kutaka kukubalika zaidi, kupata wabunge wengi na kugombea nafasi za kugombea badala ya kutaka kushinda. CDM itapimwa na inapaswa kupimwa siyo kwa idadi ya watu wanaonesha alama ya V au wanaovaa rangi za chama au wanaokitetea mitaani. CDM itapimwa na kwa haki kabisa inapaswa kupimwa kwa kushinda uchaguzi. Sasa hivi rekodi yao kwenye chaguzi ndogo ni mbaya na ya kusikitisha.


  Wakijipanga kivita, wanaweza kubadilisha hilo.

  Harufu ya ushindi inanukia, lakini ni harufu iliyochanganyika na damu. Ipo ya adui, na ipo ya marafiki. Haya ni mapambano na yeyote ambaye hatambui hili ni watu wasiostahili kwenda mstari wa mbele. Wanaotaka kwenda mstari wa mbele wawe tayari kupigana na adui; hakuna soga, hakuna kuchekeana, hakuna kudekeana na kubembelezana. It's a war out there – win or resign! Hakuna lolote ambalo CCM inafanya Arumeru ambalo CDM walikuwa hawalijui so there is no excuse for defeat; NONE WHATSOVER.


  It's as simple as that. CCM hawatawarahisishia kazi hiyo na kwa haki kabisa ni lazima CCM wajitahidi kuhakikisha CDM haishindi – wanaodhani CCM itabania halafu itaachia kiulaini wanaota ! Ndio tofauti kati ya vita na ngoma.
  I believe while CCM will more other opportunities to make a stand for CHADEMA it is in Arumeru East where it will and must make its FINAL STAND.  Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  MMM,

  Ni kweli kwamba CDM wanajua ccm inafanya nini Arumeru.
  CCM wanatumia dola kuhakikisha ushindi unapatikana.
  Ni vigumu sana ku determine wameru, kwamba ni watu wa namna gani.
  La msingi ni kwamba CDM wajikite kwenye sera badala ya kujibu matusi.
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Umenena MMM...nadhani vita ya ardhini ni bora zaidi kwasasa..mabomu na kila aina ya silaha tulizotumia hapo nyuma zimetosha kudhoofisha ngome ya adui..sasa twaweza kushuka chini na kupigana uso kwa uso.Hakika kama tunapima ushindi kwa kuangalia idadi ya watu kwenye kampeni CDM tunanafasi nzuri kwa hilo..lakini hilo alitoshi,je ni wangapi watatupigia kura? Tunahitaji ushawishi wa karibu na wenye tija.Tunahitaji vijana wakee na vijana wenzao wawaambie ubaya wa CCM,tunahitaji wanawake wakae na wanawake wenzao wawaeleze ubaya wa CCM,tunataka wazee kama akina Ndesamburo wakae na wazee wenzao wawaeleze ubaya wa CCM..tukifanya haya hakika tutavunja kuta za CCM na itaanguka chini. Nadhani,ni wakati wa kuacha maneno ya majukwaani,twende kwenye mashina zaidi,unapoongea na mtu kwa ukaribu una uwezo wa kumvuta na kumshawishi..ni wazi kwa vita vya majukwaani Sioyi ni dhaifu kupindukia,na ni wazi usiopingika kuwa Nassari mpaka ametudhibitishia kuwa kwa vita za majukwaani ni bora zaidi.Sasa tushuke chini tuongee na wale wazee wanaoamini kuwa CCM ni vyote katika vyote,wale akina mama wanaoamini kuwa CCM haina mbadala nk.Tukifanya haya ushindi kwa CDM ni wazi April mosi. MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI CHADEMA,MUNGU MMBARIKI KIJANA WETU JOSHUA S.NASSARI
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  =========

  Mzee
  Shukrani kwa piece hii ya Fallujah. Angalia hapo kwenye red ikibidi ufanye marekebisho maana hapaeleweki.
   
 5. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MzeeMwanaKijiji, MMM tafadhali uwe unafanya utafiti kabla ya kuandika. Umeongopa sana kuhusu Fallujah, sijui hizo habari wewe umezitoa wapi au umejitungia tu ili uifurahishe nafsi yako au sijui pengine umeandika kiitikadi zaidi kuliko ukweli yaani sikuelewi kabisa mzee mzima na heshima yako kuandika uongo na uzushi, aibu!!

  Kwa taarifa yako Fallujah iko kwenye Sunni triangle maeneo ambayo yako chini ya Sunni islam na siyo Shia islam ya Muktar Al Sadri, Mahdi Army jeshi la Muktar al sadri hawajawahi kuweka mguu fallujah na wakifanya hivyo hawezi kurudi makwao na vichwa vyao, huko iraq shia na sunni hawapikiki chungu kimoja

  Hapakuwa na mapigano mawili fallujah baada ya mauaji wa walinzi ambao miili yao ilining'inizwa darajani, palikuwa na mpambano mmoja tu ambapo wapiganaji wa ki sunni ambao walikuwa ni wafuasi wa al aqaida walipata mkong'oto wa uhakika na fallujah ilitulia toka siku hiyo hadi leo. Licha kwamba fallujah ndo palikuwa makao makuu ya alqaida in iraq, a sunni insurgency against america

  Please check your facts before you post, humu JF members wengine wanaishi nje ya bongo na baadhi yao waliuona huo mpambano wa fallujah live, hivyo unajishushia heshima yako bure kuandika uongo na uzushi. Nadhani source yako ya habari hii iko biased and distorted.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  CHADEMA - madhabahu kwa madhabahu, mringaringa kwa mringaringa, boda boda kwa boda boda, nyanya kwa nyanya that's is the way to go.
   
 7. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Ndugu mwanakijiji, kwa kweli uchambuzi wako umenifanya niarishe kupata chai asubuhi hii. Huu ni uchambuzi wa ulioeenda shule.Hongera! Ni kweli ama baadhi ya viongozi wa cdm wanatumiwa na adui au wanafanya kwa kutojitambua kuibua hoja ambazo muda wake bado. Hivi sasa macho na fikra za watu ni kwenye uchaguzi mdogo wa arumeru. Inakuaje watu wanaingiza tena suala la urais. Huu ni muda wa kuonyesha watu kuwa cdm wanaweza na hivyo kwa ujumla wao, viongozi wanatakiwa wawe kitu kimoja. Kuna hoja ya urais mh Zitto ameliibua katikati ya vita. Magazeti yakaamplify, ikaonekana kuna vita ndani ya chadema kati ya zitto na Slaa/Mbowe. Kama ulivyosema hapo kwenye blue, viongozi wa chadema wanatakiwa kujua ni wakati gani walumbane na wakati gani wawe pamoja. Sisemi kutofautiana ni kubaya as long as ni haki yake kutamani kile amabacho anakitaka. Lakini madhara ya kila jambo lazima yazingatiwe kabla ya kutenda.

  Mwisho, namshauri Mh Zitto aungane na makamanda wenzake, ajizuie kwanza uchaguzi upite, wafanye tathmini na kuangalia muda muafaka wa kutoa matamko. Zitto ni kiongozi mzuri na mzalendo, tatizo lake ni moja tu, "kutoa matamko ya utata kwa muda usiofaa". Haya mabo yanavuruga fikra za watu. Na adui hutumia hii mbinu kupitia vyombo vya habari kuleta fitina kwenye chama.
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  dah .... umenikumbusha mabali sana .....

  View attachment 50209

  chief propagandist Mohammed saeed al Sahhaf ..... anaother Mwigulu Nchemba
   
 9. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Unarekebisha,Unakosoa,Unasuta, au unaleta mipasho?
  Sidhani kama Mwanakijiji yupo kwa ajili ya kupotosha au kuleta Uzushi ni moja ya watu wenye kipaji cha juu cha uchambuzi wa habari za kitaifa au kimataifa, unajua wakati mwingine inawezekana source alizotumia ndizo zina Mushkeri lakini sio lengo lake kuupotosha umma wa JF.
  One thing! Kuwa na staha mkuu wangu inawezekana lengo lako lilikua zuri lakini umeharibu kwa comments zako za shari!
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Angalizo: thread za Mwanakijiji huwa zinakua ndefu sana jamani msiwe mnaquote thread yote!
  Mods liangalieni na hili maana ni shida kwa wanaotumia Mobile.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kuwa Fallujah waliopambana na jeshi la Marekani na maswahiba zake walikuwa ni wanamgambo wa ki-Sunni na si jeshi la Ki-Shia la Mahdi la Muqtada al-Sadr [not Muktadar al-Sadr]

  Juu ya hivyo, kwa mlinganisho wa vita vya Fallujah na uchaguzi wa Ingunga na Arumeru, kuifananisha CCM na wanamgambo wa ki-Sunni na CDM na wapiganaji wa jeshi la Kimataifa linaloongozwa na Marekani ni pumbazo la aina yake
   
 12. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Ushauri wako ni mzuri ila vya kuzingatia hapa ni nguvu kubwa wanayoitumia CCM kuendelea kulishikilia jimbo la Arumeru.. Tunaona nguvu kubwa na hatarishi zinazotumiwa na chama tawala nje na ndani ya Arumeru.. Hawanadi sera tena kwa maana wananchi wamezichoka sera zicizo tekelezeka.. Wanalenga wale ambao wanaonekana wanaweza kuwatoa kwenye uongozi.. Na kwa sababu wao ndio wanashikilia kila kitu haitashangaza wao kubadilisha matokeo in their favour.. Huwezi kuilaumu CDM CCM watakapofanya hivyo unless u condone the use of force (peoples power).. Ukweli ni kwamba CDM hawako tayari kuliingiza taifa kwenye machafuko na ndio maana mara nyingi inapofikia mahali wananchi wametahayari ni Viongozi wa CDM ndio wanaenda kuwatuliza wananchi (kumbuka wamachinga wa mbeya).. So hata CCM na vyombo vyake wakipora ushindi wa upinzani bado itakuwa sio salama kwao.. na itakuwa chachu zaidi kwa watanzania wapenda mabadiliko..
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unapokosoa historia jaribu basi kuonesha kujua historia japo kidogo.
   
 14. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Umenena vema mzee Mwanakijiji juu ya CDM kutumia wiki ya lala salama kufanya kampeni za nguvu na za uhakika wa ushindi. Hii ni nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na kata kwa kata yaani ni hakuna kulala ili kuondoka hivi vijisababu vya kila tunaposhindwa na kuwasha vema indicator ya kutwaa nchi 2015.
  ni
  Ushindi Arumeru mashariki kwa CDM ni LAZIMA no matter what stand in between. Otherwise tutaendelea kujifariji tu kuwa chama kinazidi kukua lakini matunda ya ukuaji hatuyaoni. Nyomi ya watu iwe inareflect kura zao kwenye masanduku ya kura. kama ni kujifunza wamepata fursa ya kujifunza mara 8 katika chaguzi ndogo kwa sasa utekelezaji wa walichojifunza.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi CCM inataka kupata ushindi kwa njia ya Psychological warfare; kuwafanya CDM na wapiga kura Arumeru wakate tamaa. Ukiangalia wiki hii nzima utaona kuwa habari nyingi za CCM zitakuwa zinaonesha kuwa CCM ina edge over CDM na hivyo baadhi ya watu - kama ilivyokuwa 2010 - kuamua kuwa "CCM watashinda anyway so kwanini kupiga kura". Ikumbukwe ni kweli CCM inaingia ikiwa inapendelewa kwa kila kitu lakini siri ya kura iko kwenye kura moja moja. CCM inahitaji kuhamasisha wanachama wake tu kwenda kukipigia CCM wakati CDM inahitani kuhamasisha hadi wana CCM kwenda kukipigia kura.

  Lakini vile vile CDM ni lazima itafute mbinu - sijui strategists wao wanasema nini - ya kuweza kucounter the psychological warfare inayoendeshwa na CCM. Na upande mwingine - sadly- CDM wenyewe wameingia kwenye mtego usio na sababu. Angalia viongozi wangapi na watu wangapi wamekaa kujadili habari ya Zitto kutaka kugombea Urais as if ina umuhimu wowote wiki hii.
   
 16. adil_abdallah

  adil_abdallah Member

  #16
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama chadema watachukua arumeru,basi 2015 watachukua....
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio pointi. Hapa eanajaribishwa kupita katika tanuru la moto wakipita salama 2015 inawasubiria.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio pointi. Hapa eanajaribishwa kupita katika tanuru la moto wakipita salama 2015 inawasubiria.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio pointi. Hapa eanajaribishwa kupita katika tanuru la moto wakipita salama 2015 inawasubiria.
   
 20. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,786
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Binafsi mwanzoni nilidhani Ulikuwa mpango wa CDM kumtumia Zitto kutoa tamko hilo ili kuamsha mawazo ya watanzania (hasa wa Arumeru) kuwa sasa CDM kitakuwa chama tawala 2015 ndiyo maana wanaaza kuzungumzia habari za nani atakuwa rais, hivyo wampe ushindi mgombea wa CDM. Kumbe nilikosea kabisa.

  Sasa kama Mh.Zitto hakuwashirikisha viongozi wenzake wa CDM kabla ya kutoa kauli hii ya URAIS, naanza kuwa na wasiwasi na naye.

  Kwani kutoa kauli hii katika siku za mwisho wa kampeni za Uchaguzi wa Arumeru bila kuwafahamisha wenzako ni kutengeneza mazingira ya kuwavuruga wenzako ili wahame kiakili kutoka katika jukumu zito la kuhakikisha ushindi unapatika katika chaguzi zilizoko wakati huu. Ni hili tunaweza kulisema kuwa Mh.Zitto kafanya HUJUMA DHIDI YA CDM na watanzania wengine wanaopenda mabadiliko ya kiutawala wenye tija kwa raia wote. Hii inaweza ikawaongezea imani watanzania kuwa mheshimiwa huyu ni agent wa Chama tawala.

  Mh.Zitto hakutakiwa kufanya hivyo bila kukitaarifu chama chake kwa kuzingatia shughuli nzito iliyopo mbele ya chama kwa wakati huu, ninajua kuwa anayohaki na uhuru kusema yaliyo moyoni mwake kwa mujibu wa katiba ya nchi tuliyonayo.
   
Loading...