Mpaluka Mdude Nyagali abadilishiwa mashtaka ya Uhujumu uchumi, asomewa ya Kusafirisha Dawa za Kulevya

Inawezekana wafuasi wa Chadema huwa hawakosei, wanatii Sheria zote za nchi na Ni wacha Mungu wote.

Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi alipokamatwa kwa tuhuma za ujangili mlishangilia mkaanza kusema CCM wote majizi na majangili, huyo mdude yeye hakosei?

Siku zote akitiwa mbaroni mwanachadema mnaanza kusema anabambikizwa kesi au makosa, mwana CCM akikamatwa mnaunga mkono.

Tusiwe watetezi wa kusafisha tuhuma bila ushahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Saguda47 the witch
 
Mshamba na limbukeni anatambuliwa kwa maneno yake.

Unataka kutwambia kuwa msafisha choo hana sifa ya kuishi?
Leo hii kuna wahitimu kibao wa vyuo hawana kazi unadhani wataishi vipi wakaibe?
Nilipopata taarifa za huyu bwana kuwa mpiga deki kwenye choo cha stand nilianza kuielewa CHADEMA na wanachama wake.
 
Afadhali wenye kujua abc za kisheria
kungekuwa na uhuru wa mahakama hiyo kesi wangeifukuza,hairuhusiwi kubadilisha mashitaka wakati kesi imeshafunguliwa,kama ni makosa ya mashitaka walitakiwa kuyaona hukohuko kabla ya kufungua kesi,!!
 
Hivi vile vi-wonder ambazo kelele zake zimekufa kifo cha mende kama ile slogan ya "hapa kazi tu" ilivyojifia ndio hivi vya kutengeneza kesi uchwara?
 
LIPI HAPO LINA ANGALAU KATI YA LILE LA AWALI NA HILI
Don corleone Sicilian mafia kama wewe tena God Father hujui hapo wapi kuna afadhali? Umeniangusha bob ... wamedrop hizo za uhujumu probably kwasababu hawana ushahidi ... kesi ya madawa ni hatari ukitoa ya kuvuta ( kutumia ) hii ni mil chini ya mil 1 au miak 3 ... wamesema amesafirisha maana yake ni biashara hii maisha mkuu ... sema kitakacho msaidia ni kiasi alichokutwa nacho nahisi ni kidogo sana kwa biashara ( mi sio mwanasheria uhuni tu)
 
Mwana kulitafuta mwana kulipata anavuna alichopanda
Marehemu Akwilina Akwilini alipanda nini mpaka akavuna kuuawa na wale wendawazimu? Unaweza ukaona uko salama sana lakini madhara ya udhalimu wa kichaa mmoja yakakuathiri bila kupenda.
 
Inawezekana wafuasi wa Chadema huwa hawakosei, wanatii Sheria zote za nchi na Ni wacha Mungu wote.

Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi alipokamatwa kwa tuhuma za ujangili mlishangilia mkaanza kusema CCM wote majizi na majangili, huyo mdude yeye hakosei?

Siku zote akitiwa mbaroni mwanachadema mnaanza kusema anabambikizwa kesi au makosa, mwana CCM akikamatwa mnaunga mkono.

Tusiwe watetezi wa kusafisha tuhuma bila ushahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmoja alionekana na shehena ya silaha kama ghala la kutunzia silaha la jeshi wakati wa pili hatujaona hiyo sembe akisafirisha kwa baiskel, bagadu, mkokoteni, mdomoni, ndani ya tumbo au kwenye soli ya viatu kama tulivyozoea kuwaona wanaokamatwa na hiyo sembe.

Hata hivyo, kuachiwa kwa wa kwanza kwa kosa la kuhujumu uchumi inawezekana ndiyo sababu ya kumfutia mashitaka wa pili shitaka la kuhujumu uchumi kwa sababu watu wamekuwa wanahoji kwanini kosa ni moja la kuhujumu uchumi kwanini mmoja apewe dhamana na mwingine anyimwe!
 
Mshamba na limbukeni anatambuliwa kwa maneno yake.

Unataka kutwambia kuwa msafisha choo hana sifa ya kuishi?
Leo hii kuna wahitimu kibao wa vyuo hawana kazi unadhani wataishi vipi wakaibe?
Jibaba hakuna sehemu niliyosema naidharau kazi ya kupigandeki choo cha stand wala hakuna sehemu yeyote nimesema huyu bwana Hana haki ya kuishi.

Unachachatika bure kamanda...
 
Umaskini mmbaya jmn acha tuu simshangai kilichomtokea na alicho kuwa anafanya.
 
Back
Top Bottom