Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 9,229
- 7,375
Kutokana na ramani nyingi ( mfano ni hiyo hapo juu) mpaka huu uko ukingoni mwa ziwa Nyasa/Malawi na ziwa lote ni la Malawi.Ina maana kuwa wavuvi na boti zetu zinaposafiri mno zinaingia bila kibali katika nchi nyingine? Au wametuazima kwa muda? Mbona hali ni tofauti kwenye maziwa Tanganyika na Victoria ambapo mipaka iliyopo inaonyesha wazi milki za Tanzania? Au kuna makaubaliano maalum kuhusu ziwa Nyasa. Nakumbuka kuna wakati almanusra tupigane na Malawi kutokana na wao kudai milki ya ziwa lote. Tuliimba sana wakati wa mchakamchaka nyimbo za kumtukuna Ngwazi Kamuzu Banda. hivi inawezekana alikuwa sahihi! Kama sio, mbona hatujarekebisha ramani?