Katika awamu hii chini ya Rais mpya Malawi, Magufuli atumie fursa hii kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,209
2,000
Hili tatizo la mpaka kati ya Tanzania na Malawi hadi leo halijatatuliwa. Suala ni kwamba, kuna dalili za mafuta ndani ya Ziwa Nyasa, ambalo Malawi wanaliita Ziwa Malawi. Na suala la uwezekano wa mafuta lilizua upendezi mpya wa ziwa kwa Malawi wakasema kwamba mpaka kati ya Tanzania na Malawi siku zote umekuwa mwisho wa ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania, yaani ziwa lote liko ndani ya Malawi.

Tanzania wakasema hakuna kitu kama hicho. Siku zote mpaka ni mstari wa katikati ya ziwa ili kutenganisha Malawi na Tanzania, na hiki ndicho kinachokubalika kimataifa kunapokuwa na maji makubwa kati ya nchi mbili. Malawi hawakukubaliana na msimamo wa Tanzania, na wakadai wataweka watafiti wa mafuta ndani ya ziwa lao (Nyasa). Tanzania ikawaambia Malawi watafiti hao wakiingia upande wa Tanzania watakiona cha mtema kuni.

Marais wa Malawi waliopita walikuwa na msimamo mkali kuhusu ziwa Nyasa wakidai ziwa lote liko Malawi na hata walitumia jambo hili katika kampeni zao. Sijui msimamo wa huyu raisi mpya wa Malawi ukoje. Mgogoro huu ulikuwa usuluhishwe na SADC na Thabo Mbeki na Joachim Chisano walipewa jukumu la kuutatua. Sijui ripoti yao iliishia wapi, au kama waliweza kumaliza kazi yao.

Huko nyuma niliwahi kupendekeza humu JF kwamba jambo kubwa linalofanya kuwe na mgogoro wa mpaka ni mafuta ndani ya ziwa Nyasa. Nikapendekeza kwamba, kwa nini Tanzania wasikubaliane na Malawi kwamba mafuta yote yatakayopatikana ndani ya ziwa Nyasa uwe mradi wa pamoja kati ya Tanzania kwa kugawana 50:50? Sijui kama kuna walionisikiliza.

Sasa basi, kwa kuwa tuna Rais mpya Malawi, ambae ameonyesha ukaribu na Magufuli, ushauri wangu kwa Magufuli ni kutumia fursa hii kumaliza hili suala la mpaka wetu na Malawi. Nachela tusipolimaliza sasa huko mbele linaweza kuja kuzaa vita kati ya Tanzania na Malawi.

Mambo ya vita yamepitwa na wakati. Wanajeshi siku hizi hawapigani wanajenga madaraja na kujenga nyumba nk. Rais Magufuli hebu ongea na Rais wa Malawi tumalize jambo hili na kuanza kutumia hayo mafuta kujenga SGR, Stiegler Gorge, flyovers, lami hadi vijijini, nk, tuifanye Tanzania kama Ulaya!

Angalia pia;

  1. Nafurahi Kuona Mediators Wanafikiria Kama Nilivyoshauri Humu JF Kuhusu Mgogoro wa Malawi Tanzania
  2. Suluhisho la mgogoro na Malawi ni hili; sio suala la ziwa wala mpaka
 
mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,722
2,000
Usimpe Rais wetu matatizo mengi
Sasa hivi yupo bize na kumaliza masalia ya upinzani
Akimaliza hapo anahamia Ujenzi wa SGR hadi kila kijiji kiwe na yake
Akimaliza hapo aanze kudeal na Uteuzi
Atamalizia na kupandisha bidhaa za viwandani ili zifanane na Cement
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,209
2,000
Usimpe rais wetu matatizo mengi
Saivi yupo bize na kumaliza masalia ya upinzani
Akimaliza hapo anahamia ujenzi wa SGR hadi kila kijiji kiwe na yake
Akimaliza hapo aanze kudeal na uteuzi
Atamalizia na kupandisha bidhaa za viwandani ili zifanane na cement
Ukiwa Kiongozi, ubora na hekima katika Uongozi wako unaonekana katika kushughulikia mambo makubwa kama mpaka wa Tanzania na Malawi, sio kukimbizana na viongozi wa Upinzani na mashabiki wao!
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,209
2,000
Ila nina wasiwasi kama Prof. Kabudi anaweza kutatua huu mgogoro. He is just too presumptuous and cocky.

Tanzania tulipokuwa na mgogoro na Kagame wa Rwanda, Kikwete alimtumia Prof. Mwandosya kwenda kumalizana na Kagame, na Mwandosya alifanikiwa sana. Hivyo Magufuli angeweza kumtumia Prof Mwandosya suala la Malawi. Ila sasa Mwandosya na Magufuli hawaivi kabisa. Mwandosya anamuona Magufuli kama koplo kwenye jeshi la siasa, na Magufuli anamuona Prof. Mwandosya anajifanya Einstein wa Tanzania na anataka kumuonyesha makoplo wanashinda vita bila kuwahitaji kina Einstein!
 
chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
7,843

Pumbavu wewe, lini Mwandosya alitatua mgogoro wa Rwanda na Tanzania?

Tanzania ilipeleka majeshi yake Drc na waasi wa M23 waliokuwa wanadhaminiwa na Rwanda walifurushwa.

Unatoa mifano ha kipuuzi, koplo wa siasa ndio nini?
 
chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
7,843
2,000
Hili tatizo la mpaka kati ya Tanzania na Malawi hadi leo halijatatuliwa. Suala ni kwamba, kuna dalili za mafuta ndani ya Ziwa Nyasa, ambalo Malawi wanaliita Ziwa Malawi. Na suala la uwezekano wa mafuta lilizua upendezi mpya wa ziwa kwa Malawi wakasema kwamba mpaka kati ya Tanzania na Malawi siku zote umekuwa mwisho wa ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania, yaani ziwa lote liko ndani ya Malawi.

Tanzania wakasema hakuna kitu kama hicho. Siku zote mpaka ni mstari wa katikati ya ziwa ili kutenganisha Malawi na Tanzania, na hiki ndicho kinachokubalika kimataifa kunapokuwa na maji makubwa kati ya nchi mbili. Malawi hawakukubaliana na msimamo wa Tanzania, na wakadai wataweka watafiti wa mafuta ndani ya ziwa lao (Nyasa). Tanzania ikawaambia Malawi watafiti hao wakiingia upande wa Tanzania watakiona cha mtema kuni.

Marais wa Malawi waliopita walikuwa na msimamo mkali kuhusu ziwa Nyasa wakidai ziwa lote liko Malawi na hata walitumia jambo hili katika kampeni zao. Sijui msimamo wa huyu raisi mpya wa Malawi ukoje. Mgogoro huu ulikuwa usuluhishwe na SADC na Thabo Mbeki na Joachim Chisano walipewa jukumu la kuutatua. Sijui ripoti yao iliishia wapi, au kama waliweza kumaliza kazi yao.

Huko nyuma niliwahi kupendekeza humu JF kwamba jambo kubwa linalofanya kuwe na mgogoro wa mpaka ni mafuta ndani ya ziwa Nyasa. Nikapendekeza kwamba, kwa nini Tanzania wasikubaliane na Malawi kwamba mafuta yote yatakayopatikana ndani ya ziwa Nyasa uwe mradi wa pamoja kati ya Tanzania kwa kugawana 50:50? Sijui kama kuna walionisikiliza.

Sasa basi, kwa kuwa tuna Rais mpya Malawi, ambae ameonyesha ukaribu na Magufuli, ushauri wangu kwa Magufuli ni kutumia fursa hii kumaliza hili suala la mpaka wetu na Malawi. Nachela tusipolimaliza sasa huko mbele linaweza kuja kuzaa vita kati ya Tanzania na Malawi.

Mambo ya vita yamepitwa na wakati. Wanajeshi siku hizi hawapigani wanajenga madaraja na kujenga nyumba nk. Rais Magufuli hebu ongea na Rais wa Malawi tumalize jambo hili na kuanza kutumia hayo mafuta kujenga SGR, Stiegler Gorge, flyovers, lami hadi vijijini, nk, tuifanye Tanzania kama Ulaya!

Angalia pia;

  1. Nafurahi Kuona Mediators Wanafikiria Kama Nilivyoshauri Humu JF Kuhusu Mgogoro wa Malawi Tanzania
  2. Suluhisho la mgogoro na Malawi ni hili; sio suala la ziwa wala mpaka
Hivi wewe huwa una akili kichwani au ni mburula ambae huwa anajifanya anajua wakati ni mpuuzi tu. Mpaka wa malawi na Tanzania hujui upo wapi? Mafuta yawe upande wa Tanzania alafu unapendekeza mradi uwe fifty fifty!

Kama kuna mgogoro Lazarus Chakwera angekuja kunya ziara bongo? Tumia common sense unapotoa mada zako
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
2,105
2,000
Pumbavu wewe, lini Mwandosya alitatua mgogoro wa Rwanda na Tanzania?

Tanzania ilipeleka majeshi yake Drc na waasi wa M23 waliokuwa wanadhaminiwa na Rwanda walifurushwa.

Unatoa mifano ha kipuuzi, koplo wa siasa ndio nini?
Hujui kitu ndiyo maana umeanza na tusi.
Uliza ueleweshe ee kopolo.
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
2,105
2,000
Hivi wewe huwa una akili kichwani au ni mburula ambae huwa anajifanya anajua wakati ni mpuuzi tu. Mpaka wa malawi na Tanzania hujui upo wapi? Mafuta yawe upande wa Tanzania alafu unapendekeza mradi uwe fifty fifty!

Kama kuna mgogoro Lazarus Chakwera angekuja kunya ziara bongo? Tumia common sense unapotoa mada zako
Hujui kama hata Tz tulijiandaa kwenda kunyonya hicho kimiminika lakini tumeacha?
Mgogoro wa mpaka upo tangu zamani na vipindi vyote hivyo marais wa Malawi ukimwacha Kamuzu Banda wamekuwa wakihudhuria sherehe za kitaifa hapa Tanzania.

Uliza siku nyingine ,usikimbilie kutukana.
 
chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
7,843
2,000
Hujui kama hata Tz tulijiandaa kwenda kunyonya hicho kimiminika lakini tumeacha?
Mgogoro wa mpaka upo tangu zamani na vipindi vyote hivyo marais wa Malawi ukimwacha Kamuzu Banda wamekuwa wakihudhuria sherehe za kitaifa hapa Tanzania.

Uliza siku nyingine ,usikimbilie kutukana.
Nani katuzuia we bwege,au unadhani mafuta yanachimbwa kama mchanga?
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,209
2,000
Hivi wewe huwa una akili kichwani au ni mburula ambae huwa anajifanya anajua wakati ni mpuuzi tu. Mpaka wa malawi na Tanzania hujui upo wapi? Mafuta yawe upande wa Tanzania alafu unapendekeza mradi uwe fifty fifty!

Kama kuna mgogoro Lazarus Chakwera angekuja kunya ziara bongo? Tumia common sense unapotoa mada zako
Ni wazi sana kwamba sio tu una tatizo la akili, bali huna elimu ya kutosha kuelewa dunia inavyokwenda. Wonyesho wako wa kukosa akili unajidhihisha pia na comment zako, kuwa "hujui mpaka wa Tanzania na Malawi uko wapi, na kama kuna mgogoro mbona Chakwera kafanya ziara bongo". Hayo ni maoni ya mtoto wa darasa la pili.

Mafuta yakiwa ziwani ardhini , sio kwamba yanakaa sehemu moja ardhini. Yanakuwa kwenye reservoir iliyosambaa. Exploration ni pamoja na kupata the optimum point ya kufanya drilling. Kwa ziwa Nyasa basi, mwamba wa mafuta unaweza kuwa umesambaa pande zote mbili, Tanzania na Malawi.

Hivyo katika maeneo madogo ya mafuta kati ya nchi mbili inakuwa busara kwa nchi hizo kufanya joint oil production projects. Na huo pia ndio mtazamo tulio nao kwa mafuta yaliyo Ziwa Tanganyika, kufanya joint oil production projects na DRC mara tutakapowaondoa rebels walio eneo la mafuta upande wa DRC.

Sasa je, suala la joint projects ni geni? Hapana. Mafuta yaliyo eneo la North Sea eneo la bahari inayayounganisha nchi kama Norway, Denmark na UK, hili pia ndilo linalofanyika. Na pia linaokoa gharama, kwa kuwa mnaweza kujikuta mnatengeneza oil production platform upande wa Tanzania na Malawi na kuchimba mafuta toka oil reservoir moja ingawa mnafuata mipaka yenu.

Sasa umejiona usivyo na akili, unabisha wala hujui unabishana na nani na ana ufahamu gani juu ya mambo haya unaleta fyokofyokofyoko mambo usiyoyaelewa. Pumbafu sana wewe. Nimekuambia unakuwa na kiherehere kujibu thread kama kipigo cha kwanza. Kakojoe ulale.

Nimetumia maneno ya kiingereza humu, usipoelewa omba jirani akutafsirie.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,209
2,000
Pumbavu wewe, lini Mwandosya alitatua mgogoro wa Rwanda na Tanzania?

Tanzania ilipeleka majeshi yake Drc na waasi wa M23 waliokuwa wanadhaminiwa na Rwanda walifurushwa.

Unatoa mifano ha kipuuzi, koplo wa siasa ndio nini?
Sasa kama hujui hata matumizi ya tungo tata kama koplo wa siasa, utawezaje kuelewa thread kama hizi? Hebu kabebe mizigo ya wakulima sokoni. Sio kosa letu kwamba hukwenda shule, acha hasira na watu wanaokuzidi ufahamu. Una matatizo kichwani wewe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom