Mpaka sasa Rais Magufuli kashafanya teuzi zaidi ya 550, tunahitaji mabadiliko ya kimfumo

JGG

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
323
136
Rais Magufuli mpaka leo ameshafikisha ajira ngapi? Kwa kumbukumbu zangu za haraka:
Mawaziri 30+makatibu 40+RC 26+DC 139+DAS 139+DED 185+mabalozi+mashirika+idara +etc etc = over 550 people,

Marekani rais wao ana uwezo wakuteua bila idhini ya senate only 163 people.

Mwisho wa siku hii hali jumlisha na 87% ignorant voting population in Tanzania, nadhani tutafute njia nyingine ya kupata mabadiliko.
 
Kuteua kama hawa?
 

Attachments

  • images-14.jpg
    images-14.jpg
    10.2 KB · Views: 51
Kwa system hii sidhani kama kuna kiongozi atakuja kuifanyia mambo mazuri Tanzania, wote watakuja kuwa wazuri baadae zitakuja lawama tuu. Nchi hii alieitoa kwa wakoloni ndie wa kumlaumu na mpaka leo wengine wanaofata bado hawajui kosa.

Siasa iko mbele zaidi kuliko huduma za jamii Uongozi wa kiimla, uteuzi mkubwa kama huu ni hatari kufanywa na mtu mmoja. Tanzania itachelewa sana ingawa magufuli sahivi mapema analaumu kwa kuziambia awamu zilizopita zimechelewa lakini yeye ndio atapwewa kabisa hata hatonyanyua mguu.Mfumo ni wa Ovyo kabisa angelijua hilo angefumua kwanza kabla ya kuanza kuwagaia watu vyeo kama njugu.
 
Huyu ni zigo tena lenye lumbesa hapa Tanzania

Halafu unataka kutumbia unawajua wote uliowateua??

Hata kama anawajua. Tatizo litakuja hapa: atateua rafiki zake. Anaowajua.

Hii ya mamlaka ya Rais kuwa na uwezo wa kugawa ajira zaidi ya 500, imewafanya baadhi ya watu kwa sasa wawe wa

kujipendekeza ili wateuliwe u-RC,DC,DED,DAS nk.
 
Hata kama anawajua. Tatizo litakuja hapa: atateua rafiki zake. Anaowajua.

Hii ya mamlaka ya Rais kuwa na uwezo wa kugawa ajira zaidi ya 500, imewafanya baadhi ya watu kwa sasa wawe wa

kujipendekeza ili wateuliwe u-RC,DC,DED,DAS nk.
Exactly mkuu , hii nchi kila siku tukiamka ni mazingaombwe tu.

Katiba mpya ilizikwa kwa nia ovu kama hizi zinazojitokeza.
 
Kwa katiba ya Tanzania kwa sasa, rais ni sawa na mungu hapa duniani.
He can't be questioned, challenged or even criticized basing on what he does.
Yani Rais Ana nafasi kubwa ktk nchi mpaka basi, Ni vigumu Sana kupata mabadiriko katika mazingira kama haya...,,
 
Nasubiri kwa hamu akianzisha mchakato wa kurudisha katiba ya Warioba, kwa katiba hii acha ateue tu wakatafune kodi zetu maana hakuna namna nyingine
 
Huyu ni zigo tena lenye lumbesa hapa Tanzania

Halafu unataka kutumbia unawajua wote uliowateua??
Naomba mkumbuke kuwa sio kosa lake katiba inampa mamlaka hayo.
Suala pekee la kutuokoa katika kadhia hiyo ni katiba mpya.
Si maanishi katiba ya Andrew Chenge, na maanisha rasmu ya pili ya jaji Sinde Warioba.
Hii ndiyo itaboresha utendaji na kupunguza utitili wa hizo teuzi kutoka kwa rais wetu Mwema.
Tukifanya hivo tutakuwa tumepunguza mamlaka ya rais.
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Back
Top Bottom