Mpaka sasa Rais Magufuli kashafanya teuzi zaidi ya 550, tunahitaji mabadiliko ya kimfumo

Je ni kweli huo uteuzi utaleta mabadiliko yanayotakiwa? Siyo political willpower? Mfumo kama tubaki ileile tutakuwa tunapoteza pesa za wananchi Burke badala ya kupelekwa kwa wananchi
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Retirement or terminal benefits plus luggage transportation for both old and newly appointed officials zitalipwa na nani?
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Naomba mkumbuke kuwa sio kosa lake katiba inampa mamlaka hayo.
Suala pekee la kutuokoa katika kadhia hiyo ni katiba mpya.
Si maanishi katiba ya Andrew Chenge, na maanisha rasmu ya pili ya jaji Sinde Warioba.
Hii ndiyo itaboresha utendaji na kupunguza utitili wa hizo teuzi kutoka kwa rais wetu Mwema.
Tukifanya hivo tutakuwa tumepunguza mamlaka ya rais.
Katiba ilipingwa kwa nguvu zote kwa nia ovu ya Chama Cha kijani. Hii ilieleweka.
 
Tumia busara. Huyo machinji ni wa chama kimoja siyo mtumishi wa watanzania. Jaws wanakwenda kutuzimia wstanzania
 
Kwa sasa kuendelea kumdhihaki Magufuri ni kujifedhehesha, tumpe muda maana sasa ndo kakamilisha serikali yake itakayokuwa na spidi anayohitaji!
 
hilo ni jambo la kawaida kwa kila uongozi mpya. tuwape muda wateule ;
 
Katiba inamruhusu kuteua hadi walimu wakuu wa Shule za Msingi bila kuhojiwa,na hapo ndio raha ya Urais ilipo,sasa hii mtu si unaweza kuteua ukoo wako wote bila kuhojiwa.

Nadhani kuna tatizo la kimfumo na dawa ya tatizo hili ni kubadilisha Katiba itakayompa nguvu Mwananchi mnyonge kupitia Bunge kwa kupunguza Madaraka makubwa ya Rais.

Rais ana nafasi zaidi ya 5000 za teuzi mbalimbali,kuanzia Waziri mkuu,wakuu wa idara,Mawaziri, wakuu wa Mashirika, Bodi Mbalimbali balozi,akibaki kufanya kazi za teuzi peke yake anaweza kumaliza miaka yake akiwa anateua tu,nadhani kuna haja ya wananchi kumsaidia Rais katika teuzi na wengine wangechaguliwa na mfumo.

Any way Muhudumu naomba uniletee Shisha nyingine
 
Dereva akiwa katika mwendokasi nanyi abiria mkaanza kumpigia kelele apunguze mwendo, kuna mawili yanaweza kujitokeza:
1. Kelele zenu zimchanganye na kupelekea kuliingiza gari kwenye bonde kwa kiwewe hatimae mfe wote au
2. Kufikiri mnamshangilia kwa mwendo wake hivyo kuendelea kukanyaga mafuta huku mkifa kimyakimya mmoja mmoja kwa presha.


Kazi kwenu abiria.
 
Kwa maana hiyo sasa hivi hatutakiwi kukosoa?sasa twambie tumpe muda gani
this is a new administration and it has nearly a year since it has started to take charge you have to first note that, reasonable time should be considered before we start complaining and criticising
 
Back
Top Bottom