Mpaka sasa madiwani 5 wamehama CHADEMA Arusha.

Mpaka sasa madiwani 5 wamehama CHADEMA Arusha.

super nova

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
1,478
Reaction score
1,099
Diwani wa Ngabobo (Chadema), Solomon Laizer ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na CCM kwa maelezo kwamba anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Laizer ni diwani wa tano katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kutoa sababu kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Christopher Kazeri amethibitisha leo (Julai 11) kupata taarifa za kujiuzulu kwa Ngabobo.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema kujiuzulu kwa diwani huyo ni mchezo mchafu akidai amenunuliwa.

Amesema tayari walipata taarifa za diwani huyo kushawishiwa kujiuzulu na kwamba, alifuatwa na viongozi wa wilaya na kanda wa chama hicho aliowaeleza kuwa ameshawishiwa.

“Baadaye alieleza hataondoka lakini naona wamefanikiwa kumshawishi, tunashangaa viongozi wa Serikali badala ya kufanya kazi za maendeleo wanafanya kazi za kushawishi madiwani wa upinzani kuhama,” amesema.

Hata hivyo, madiwani wanaohama wanapinga kuwa wameshawishiwa kufanya hivyo.

Hadi sasa madiwani watano wa Chadema waliojiuzulu ni Credo Kifukwe wa Kata ya Murieti jijini Arusha.

Wengine waliojiuzulu katika Jimbo la Arumeru Mashariki na kata zao kwenye mabano ni Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya (Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu).

Sent from my SM-G901F using JamiiForums mobile app
 
Waende tu hata wakitaka kujiunga na Yanga au Simba Ruksa

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Yetu macho

Sent from my C2305 using JamiiForums mobile app
 
Siungi mkono suala la wao kupewa mpunga eti wahame nooooo. Kwa hiyo cdm walimpa Lowassa mpunga ahame ccm. Ni utashi wa mtu wa kisiasa.

Sent from my itel S31 using JamiiForums mobile app
 
Hao wameahidiwa ujira mnono waache wakajiongezee kipato ila waache unafiki

Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
*CCM BADALA YA KUNUNUA MADIWANI ARUSHA PELEKENI MAENDELEO MSIJE KUUMBUKA TENA KAMA 2013*

Kuna Mchezo umeibuka Arusha katika jimbo la Arumeru Mashiriki ambao unaochezwa na viongozi wa serikali ya ccm wa Mkoa wa Arusha ni mchezo wa kitoto na unashangiliwa na watu wenye akili ya makinikia

Yaani Diwani anaacha kuwatumikia wananchi eti kwa sababu anamuunga mkono Rais anavyowatumikia wananchi yaani unaacha kufanya kazi ili umsapoti mtu anaefanya kazi vizuri, yaani mpaka uwe na uwezo mdogo kabisa wa kufikiria kama ya vijana wa Lumumba na washangiliaji wa Bungeni ndio uamini upuuzi huu.

Siasa hizi zilifanyika kipindi cha karne ya tano kipindi cha zama za kati (medieval period) kipindi cha wanafalsafa wakina Thomas Aquinas moja ya nadharia yao ni we believe in order to understand ndio watu walikuwa wanaamini kwanza ndio wanaelewa.

Katika kipindi hicho tu ndio wangeweza kuamini madiwani hao wameachia ngazi kwa sababu wanamuunga mkono Rais ili baadae waelewe baada ya uchaguzi wa 2020 kufanyika, lakini kipindi hiki cha post modernism watu huelewa haraka na kushirikisha zaidi akili yao, ccm wangejiuliza kidogo tu Arusha wanapendwa watu au chama ili mjue nini hasa kinachowafanya mshindwe.

Maana unaweza ukanunua Madiwani wote ukaitishwa uchaguzi mwingine wakashinda tena wote wa chadema ukawa umefanya biashara kichaa, Biashara hii ya kununua madiwani Arusha haijaanza Leo ngojeni niwakumbushe Mwaka 2011 madiwani Wanne wa Chadema walinunuliwa ili wapingane na maamuzi ya chama.

Ya kutokumkubali Meya wa jiji la Arusha kwa kipindi hicho alikuwa ni Gaudence Lyimo, Chadema iliamua kuwafukuza madiwani wote waliomkubali Meya fake wa ccm walifukuzwa ni madiwani Estomih Mallah (Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni). Uchaguzi ulipofanyika mwaka 2013 Chadema ilizirudisha Kata zote na matokeo ya uchaguzi mdogo yalikuwa hivi,

Katika matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Elerai, Obedi Meng’oriki mshindi alikuwa Jeremiah Mpinga wa Chadema aliyepata kura 2,047 dhidi ya 1,471 za Emmanuel Laizer wa CCM. Katika Kata hiyo kulikuwa na wagombea wengine ambao ni John Bayo (CUF; kura 302), Seif Shimba (CCK; kura 3) na Boisafi Shirima (TLP;1).

Katika Kata ya Themi, Kinabo Edmund wa Chadema aliibuka na ushindi baada ya kupata kura kupata kura 674. Msimamizi wa Uchaguzi Kata hiyo, Ezeka Mboya alisema Kinabo alifuatiwa na Victor Mkolwe aliyepata kura 326 na Lobora Ndarpoi wa CUF alipata kura 307.

Kata ya Kaloleni, Msimamizi wa Uchaguzi, Anna Ledisa alimtangaza Kessi Lewi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 1,470 dhidi ya Emmanuel Mliari wa CCM aliyepata kura 330 na Abbas Mkindi wa CUF aliyepata kura 275 na Ngilishi Pauli wa Demokrasia Makini aliyeambulia kura mbili.

Kata ya Kimandolu, Msimamizi wa Uchaguzi, Suleiman Kilingo alimtangaza Mchungaji Rayson Ngowi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 2,761 na kumshinda Edna Saul wa CCM aliyepata kura 1,163.

Wito wangu kwa wanaofanya hii biashara ya kuwanunua madiwani wa Chadema wakifikiria kuwa wanaiua Chadema wasije wakapata yaliyowakuta mwaka 2011 maeneo hayo hayo.

Pia katika Jimbo la Rombo mwaka 2012 CCM walimnunua Diwani wa kata ya NANJARA REHA maarufu kwa jina la MNENEE ambaye alikuwa miongoni mwa madiwani watatu tu wa kata wa chadema kati ya kata 24 za Rombo matokeo yake uchaguzi mdogo ulipoitishwa mgombea wa CHADEMA Mwal FRANK SALAKANA alimshinda kwa zaidi ya asilimia 65% aliyekuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi huo.

Mimi ninatoa ushauri badala ya kufanya biashara isiyo na faida ya kununua madiwani wa Chadema hebu Wapelekeeni wananchi maendeleo ili kila mmoja apimwe mwaka 2020 kwa kazi aliyoifanya.

Niwakumbushe tu kwamba mara nyingi watu huchagua chama kuliko hata MTU, msishangae kata zote zitakaporodi CHADEMA tena kama 2013 ilivyotokea.

Asanteni sana
 
Siungi mkono suala la wao kupewa mpunga eti wahame nooooo. Kwa hiyo cdm walimpa Lowassa mpunga ahame ccm. Ni utashi wa mtu wa kisiasa.

Sent from my itel S31 using JamiiForums mobile app

Utashi unatokea Arusha tu,Endelea kufikiri kwa kutumia "madabida"
 
Huu upako uliowashukia waheshimiwa Arusha .usambae na kwingine jamani.
 
Diwani wa Ngabobo (Chadema), Solomon Laizer ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na CCM kwa maelezo kwamba anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Laizer ni diwani wa tano katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kutoa sababu kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Christopher Kazeri amethibitisha leo (Julai 11) kupata taarifa za kujiuzulu kwa Ngabobo.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema kujiuzulu kwa diwani huyo ni mchezo mchafu akidai amenunuliwa.

Amesema tayari walipata taarifa za diwani huyo kushawishiwa kujiuzulu na kwamba, alifuatwa na viongozi wa wilaya na kanda wa chama hicho aliowaeleza kuwa ameshawishiwa.

“Baadaye alieleza hataondoka lakini naona wamefanikiwa kumshawishi, tunashangaa viongozi wa Serikali badala ya kufanya kazi za maendeleo wanafanya kazi za kushawishi madiwani wa upinzani kuhama,” amesema.

Hata hivyo, madiwani wanaohama wanapinga kuwa wameshawishiwa kufanya hivyo.

Hadi sasa madiwani watano wa Chadema waliojiuzulu ni Credo Kifukwe wa Kata ya Murieti jijini Arusha.

Wengine waliojiuzulu katika Jimbo la Arumeru Mashariki na kata zao kwenye mabano ni Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya (Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu).

Sent from my SM-G901F using JamiiForums mobile app
Wewe Nasari wewe mungu anakuona. Tunajua wewe ndiye unaekula njama na hao makamanda. Harafu unajifanya kulaumu ujinga.
 
f2d04e00b71fbd52653a438c34d5c904.jpg
 
Back
Top Bottom