LGE2024 Madiwani wasusia Baraza kisa matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Mtwara

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,678
6,476
Novemba 8, 2024, madiwani 10 wa vyama vya upinzani wa Halmashauri ya Mtwara wamesusia kikao cha Baraza la Madiwani.

Hatua hiyo inatokana na kile wanachoeleza kuwa kutokubaliana na maamuzi ya msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri hiyo, ambaye amewaengua baadhi ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti kwa madai ya kujaza vibaya fomu za uteuzi wa wagombea.

4-1-1024x768.jpg

Diwani wa kata ya Ndumbwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Mtwara, Abdull Mahupa akitoa taarifa kwa mwongoza kikao juu ya kususia kwa kikao hicho (Picha na Musa Mtepa).

1-5-1024x768.jpg

Diwani wa kata ya Ndumbwe ambae pia ni Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Mtwara, Abduly Bakari Mahupa, amesema wamechukua hatua ya kususia kikao hicho kutokana na matukio ya kiuchaguzi ambayo hayakuridhisha.

Ameeleza kwamba wagombea wao wameondolewa kwenye uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutimiza vigezo, ikiwemo kujaza vibaya fomu.
20241108-124600-1024x768.jpg

2-4-1024x768.jpg
Patrick Simwinga, Diwani wa kata ya Nanguruwe kutoka CHADEMA, amekosoa hatua hiyo, akisema ni vigumu kukubali kuwa sehemu ya kikao hicho ili hali watu wao waliotumia haki yao ya kidemokrasia na nguvu zao ya kuwa sehemu ya uchangiaji wa michango ya kimaendeleo kwenye vijiji vyao ya kuwa wenyeviti na wajumbe wanaenguliwa.

Katibu wa ACT-Wazalendo Mtwara Vijijini, Hamisi Likwenda, Likwenda amesema anaunga mkono kitendo cha kususia kikao kilichofanywa na Madiwani .

Kwa upande mwingine, Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Mtwara Vijijini, Abdala Saidi Makame, amekosoa kitendo cha madiwani hao kutoshiriki kikao, akisema kuwa ni utovu wa nidhamu huku akiwataka warudi kwenye viti vyao.

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa halmashauri ya Mtwara, Abeid Abeid Kafunda, ameeleza kuwa hajapokea malalamiko rasmi ya kimaandishi na kuwasihi viongozi wa vyama vya upinzani, wanapokuwa na malalamiko, kuwasiliana na maafisa wa uchaguzi ili kuhakikisha mchakato unafanyika kwa amani na haki.

Chanzo: Jamii FM
 
Hivi hawa watu wanakua na akili za aina gani!? Kwamba madiwani wanapokuwa na malalamiko wawasiliane na wasimamizi wa uchaguzi ili mchakato wa uchaguzi ufanyike kwa AMANI, hivi amani inaweza kutokea pasipo kuwa na HAKI!? Amani ni tunda la HAKI kama hakuna haki tarajia uvunjifu wa amani.

Fikiria nchi nzima zaidi ya 98%ya wagombea wa upinzani wameenguliwa kwa kisingizio kwamba wameshindwa kujaza fomu. Wagombea wote 100% wa ccm hawajaenguliwa hata mmoja kwamba wote wamejaza vizuri fomu zao na wanasifa zinazo kidhi nafasi walizo omba!

Hao ccm wamesimea shule gani za ujazaji fomu ambako wagombea wa upinzani hawajasomea!?

Nchi yetu taratibu taratibu tunaiharibu kwa mikono yetu wenyewe.

Halafu wasomi nchi nzima wapo wa naona haya yanatokea hakuna anayepaza sauti, mnasubiri teuzi katika mazingira ya kidhalimu!? Pazeni sauti nchi hii ni ya kwetu wote, hata ninyi kuna wakati mnaweza kuwa kwenye nafasi za kuteua wengine msijishushe kiasi hicho!
 
Mimi niliombea Magufuli afe kwa sababu hizi hizi na kweli akafa. Sasa nasema hii nchi itakuwa imekatika vipande by 2040 kama uhuni huu utaendelea. Whether am alive or died mambo haya yatatokea maana haki ni takwa la kiroho
 
Back
Top Bottom