Mpaka sasa hakuna Mvujo wa Taarifa za Serikali, hakuna anayeweza kunusa kabisa nini kinaweza kutokea

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,410
1. Mpaka saa Hakuna Mvujo wa Taarifa za Serikali. Hakuna anayeweza kunusa kabisa nini kinaweza kutokea. Zimebaki kuwa confidential kwa asilimia .

2. Viongozi waliopo kwenye Utumishi wa Umma wawe makini Sana. Kwa muda mfupi niliomsoma Mama anataka viongozi wenye Discipline ya kutosha. Kwa kumuangalia Usoni haogopeshi Ila maamuzi yake yanaogopesha Sana.

3. Kuondolewa kwa Gelasius Gasper Byakanwa[aliyevunja Green House za Mbowe zenye dhamani ya bilioni 1] mkuu wa Mkoa wa Mtwara ni muendelezo wa kuelekea kwenye Political reconciliation. Huyu mkuu wa Mkoa ni yule aliyevunja Green House ya Mbowe kule Hai na kupewa promotion toka kuwa mkuu wa Wilaya hadi mkuu wa mkoa. Kuna kitu watu hawajakielewa Mama anataka kuyaleta makundi yote Pamoja. Kuna watu bado wapo kwenye Enzi za matumizi ya Nguvu badala ya akili. Kwa walioteuliwa Mpaka sasa kumbukeni Hili zama zimebadilika.

4. Jambo Lingine naloliona kwa sasa Mama anasikiliza Sana anaowaongoza. Hapo nyuma Kidogo watu wangeweza kupiga kelele kuhusu uadilifu wa Mtu flan lakini mamlaka ikamuacha tu as long as wanaolalamika ni wapinzani. Kwa sasa viongozi wanaoteuliwa pona yao ipo kwa wananchi. Yaani wananchi wakikuchukia utatolewa. Niwahusie wote walioteuliwa Mpaka sasa kuwa mtaji wao upo kwa wananchi. Kiwango Cha kukubalika na wananchi kitaamua umri wako kwenye nafasi uliyopewa.

5. Vipengele Muhimu katika uongozi vimeshaonekana (Power & Authority). Power uwezo wa Ku influence wengine kufanya au kutokufanya jambo flani. Cha pili ni Authority, huu ni uwezo wa kumshurutisha mtu kuacha au kufanya jambo flan "Mamlaka" ambayo kutokana na kazi yako na nafasi yako kazini unakuwa na mamlaka ya kumwamrisha wa chini yako au unaowaongoza.

Kauli Moja tu ya "Kudemka" ilitosha kunyamazisha wabunge na mijadala yao ya kumfananisha na JPM.

Ole Mushi
0712702555
 
Hujuma zikiwa zinatokea ndani ni ngumu sana kuzidhibiti. Kuna watu wameapa kuilinda 'nchi' dhidi ya matishio yoyote. Hata rais akiwa tishio wata deal nae na kumhujumu usiku na mchana.

Ni kazi ngumu sana na ya hatari, na baadhi wamekufa wakiwa kwenye harakati za kufanyia kazi viapo vyao, tena ukifa inatukwa cover story kuwa ulikua jambazi 😃, Mungu awapumzishe wazalendo hao.
 
Back
Top Bottom