Ni Asset? Unajua ilisemwa anakuja na Wabunge wangapi? Mpaka sasa hata wale wa kufa kupona wanagombea huko CCM ....unajua nguvu kubwa inayotumika kupangua hoja za ufisadi kuliko kunadi ilani ya Chadema? Hivi nyie mashabiki mnaijua hata hiyo ilani japo kidogo? Bora hata magufuli anatembea nayo na kuinadi .....Hivi unaamini idadi ya mahudhurio kwenye mikutano ndio kura? Pengine hukujua nini kilitokea kwa Mrema na hata Dr Slaa mwaka 2010 .....huu uchaguzi tunapoteza vibaya hadi level ya ubunge (mark my word) ....hatuna hoja nzito zaidi ya kuaminisha watu kuichoka tu CCM tena kazi hiyo ikifanywa na akina Sumaye ......Aibu tu ....
Pole sana rafiki
umeongea kwa uchungu na huzuni sana
unajua kuna tofauti hapa ninaiona, kuna wale wanaofuatilia siasa kila siku, na hawa wenye mihemko ya uchaguzi ambao hawana basis zozote zile
Nilisema mara nyingi na sita sita kurudia , moja ya kosa kubwa kabisa kufanya sisi wananchi ni kutokuwa na uwezo wa kuwawajibisha hawa viongozi wa vyama. Kuna kipindi nilipenda sana, tuwanyooshe, watusikilize, kutuelewa, tuwakosea na tukiwauliza watujibu maswali
Hawa viongozi wanachofanya ni kuandaa watu ambao watawatete kwa nguvu zote.....na kupaza sauti!
Leo hii ukionekana au kusikia unaikosoa chadema, NCCR, CCM haijalishi hata kama wewe ni mwanachama husika wa hicho chama.....utaitwa majina mabaya yote
tukubali tu, miaka 20 upinzani umeipoteza, na wakishindwa huu uchaguzi, Mbowe asubiri mwana CCM mwingine atakayekatwa 2020