Habari zenu wana Jamii Forumβ¦ Natumaini sote tumesherehekea Eid vizuri wale Eid iliyokuwa mbaya kama mimi nawapa pole tupo pamoja Mimi ni member wa muda mrefu ila imebidi nije na ID mpya kutokana na haya yanayonisibuβ¦.. \
Ndugu zangu wana jamii forum naombeni mchango wa mawazo hili jambo ni zito nashindwa kulibeba na nimeona nikiandika huku huwenda nitakuwa nimetua mzigo natanguliza shukran.
Shukran nitafanyia kaziPole sana yaani hapo jifanye kama haujui lolote na mwombe Daktari ndio aje kumweleza hiyo hali ya afya yake. Pole sana
Unachokisema kinaweza kuwa sahihi niliwaza hivyo pia naona anahisi tutaumia sana esp mimi pengine aliamuua akae zake kimya.Ukiusoma kwa makini uzi wako ni kama mama yako anaijua hali yake, isipokuwa ni ama ameamua kuishi hivyo hivyo bila kutumia ARV...
Ongea na daktari aliyekupa habari za hali ya mama yako, afanye kama anamuita kutaka kujua maendeleo yake, then akiwa huko amchane hali yake ya afya...
Be blessed nduguJikaze bi mdada,ukisikia UKUBWA ndio huo,
Tafuta Daktari or nesi aje aseme nae+ kuanza dawa asap na cha zaidi mtie moyo na kumuonyesha upendo...
AhsantePole kwakweli
Pole sana ndugu na pia hongera kwa kupata ujasiri wa kushare,Habari zenu wana Jamii Forumβ¦ Natumaini sote tumesherehekea Eid vizuri wale Eid iliyokuwa mbaya kama mimi nawapa pole tupo pamoja Mimi ni member wa muda mrefu ila imebidi nije na ID mpya kutokana na haya yanayonisibuβ¦.. Nitajaribu kuelezea kwa ufupi sana kadri nitakavyojaaliwaβ¦
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 31 ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto wa3 wote tukiwa ni wa kike kwa bahati mbaya wazazi wangu walitengana miaka mingi sana iliyopita sisi tukiwa wadogo⦠Kwa miaka yote hiyo tumekuwa tukilelewa na mama ambaye yeye ndiyo sababu ya mimi kuandika uzi huu
Mama yangu amekuwa akitulea kwa mapenzi makubwa mno na alipambana kuhakikisha sote tumesoma vizuri na kupata mahitaji ya msingi Alhamdulilah.
Baada ya kumaliza degree yangu ya kwanza Mungu alinisaidia nikapata kazi nzuri na nashukuru nimeweza kuisupport familia yangu kwa kipindi chote hiki
Miaka kadhaa nyuma nilianza kuona mabadiliko kwa mamangu na kwa kuwa ni mtu ambaye nampenda sana hata kitu kidogo tu kikiwa hakipo sawa nakuwa wakwanza kugundua tofauti na ndugu zangu.
Mama yangu ni mwanamke mrembo sana ambaye ni mchanganyiko wa Mtanzania na Mgiriki hivyo ni mtu aliyekuwa na muonekano wa kuvutia sana nakumbuka katika miaka yangu yote ya kusoma akiwa anakuja shule marafiki na walimu walikuwa wanabisha kuwa ni mama yangu na wengi walidhani ni dada yangu wa kwanza kutokana na muonekano na namna anavyojipenda.
Tuendelee mama alianza kubadilika na taratibu urembo wake ukaanza kupotea akawa hana raha, afya ikaanza kuyumba na kuna muda inakaa sawa nikawa naongea nae kumuuliza ana shida gani tofauti na Pressure inayomsumbua lakini akawa anadai yupo sawa basi siku zinazidi kwenda⦠2021 akawa anashambuliwa na maradhi mara kwa mara anaenda hospital anakuwa poa kusema kweli nilianza kuwa na hofu kubwa juu yake⦠lakini siku zikawa zinakimbia
Moyoni mwangu kuna sauti ilikuwa inaniambia kuna kitu kikubwa hakipo sawa nilichokuwa nafanya kila nikisali nilikuwa namuomba Mungu amrejeshee furaha mama yangu
To cut a story short mwaka huu mwanzoni mwa mwezi wa tatu nilisafiri kwa majukumu ya kikazi na nikiwa huko wadogo zangu walinipigia wakanambia mama amepata typhoid kali sana na yupo kwenye dawa ila nisiwe na hofu⦠ila niliporudi Mungu wangu mama yangu alikuwa ameisha nyie nilipomuona sikuweza kuzuia machozi yangu nikawauliza wadogo zangu imekuwaje hii hali wakanambia amekuwa mvivu wa kula.
Ikabidi siku iliyofuata nimpeleke hospital mimi na last born wetu nilivyofika nikaingia kwa doctor na dozi alizopewa za Typhod nikaomba amfanyie mama vipimo vyote ili nijue shida nini⦠majibu yakatoka doctor akanambia nani anaishi nae nikamwambia ni mimi na ndugu zangu akanihoji maswali kadhaa na mwishowe akaniambia MAMA YAKO NI HIV POSITIVE kwa mujibu wa vipimo. Naomba nikiri sijawahi kusikia maumivu kama niliyosikia ile siku niliona kama dunia imenielemea nyie mama yangu kipenzi changu
Nilisali pale Mungu anipe uvumilivu nisionyeshe mabadiliko yoyote kwa mama na ndugu yangu maana walikuwa nje na Doctor alinishauri nisimwambie yeyote hata ndugu zangu ila nimkazanie ale kisha nitafute hospital ya wilaya aanze CLINICβ¦. nilipotoka wote wakaniuliza umeambiwaje kwa ujasiri nikajibu ni Typhod inabidi umalize dozi
Nikiri hakuna siku nililia kama ile maana tuliporudi home niliwaaga wadogo zangu nikatoka mara moja nikatafuta mahali nikalia sana ndugu zangu naomba niwaambie nimekata tamaa nawaza nitaanzaje kumwambia mama hali yake moyo wangu umejaa maumivu makali sana.
Niliwashawishi wadogo zangu wasafiri for eid ili mimi nibaki na mgonjwa niongee nae wameondoka tangu jana lakini mpaka ninavyoandika hapa sijaweza kumwambia chochoteβ¦. kila nikikaa ni machozi tu yanatoka na ameanza kunotice ananiuliza mbona huna raha.
Ndugu zangu wana jamii forum naombeni mchango wa mawazo hili jambo ni zito nashindwa kulibeba na nimeona nikiandika huku huwenda nitakuwa nimetua mzigo natanguliza shukran.
acha kumsumbua si umeelewa lkn na unaona ana stressWewe sio msichana ni mwanamke
Wewe ulitaka uanze kupambania sioWewe sio msichana ni mwanamke
Mmmmmh aiseee...Pole sana dada.
Allah atawapa nguvu na ujasiri wa kulikabili hili.
Mimi kwa umri ni kaka yako, kwa miaka 5 zaidi. Najitolea, kuwa mfariji wako na unitambulishe kwa mama kama rafiki yako wa muda tu nilikua mkoani nikiishi huko.
Tuongee na mama pole pole na kwa kipawa nilichojaaliwa na Allah tutafanikisha kumueleza mama hali yake. Nna imani ataipokea. Ntakuja na daktari, tutashauri kitu na hali ataipokea mwenyewe. We jifanye hujui kitu.
After all, maisha lazima yaendelee, no matter what. Ni jaribu tu hili. Litapita.
Karibu.