Moyo umekuwa jiwe

Moyo umekuwa jiwe

kidonse

Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
36
Reaction score
40
Nilimpenda sana nilimtunza kama almasi. Aliponikosea sikutaka kuuliza ila kukaa kimya sikupenda kumuudhi. Alipohitaji msaada nilikua karibu nae wala sikujali usaliti wake na siku zote niliamini ipo siku atabadilika na ndoto zangu za kuwa mume wake siku moja zitatimia.

Bahati mbaya nafanya kazi sehemu moja ni mwaka sasa tangu tumeachana aliondoka huku akinitolea matusi na kashfa akiniita mimi mwanaume suruali, sina chochote cha kujivunia. Hayo yote yalitokea baada ya yeye kupata mwanaume mwingine ndo akawa ananitolea maneno yote hayo ya kashfa.

Nashukuru Mungu nilipata ujasiri wa kukaa kimya wala sikumjibu zaidi ya kumwambia kila la heri huko uendako na Mungu akusaidie. Baada ya hapo sikujua tena nini kiliendelea katika maisha yake zaidi ya kuonana nae kazini.

Na tulipokutana nae nikimsalimia akawa haitikii nami nikaona isiwe tabu nikaamua kuuchuna Kaniblock social network zote. Bahati mbaya kila siku anazidi kubadilika anazidi kuzeeka na kupoteza nuru. Maisha yamekua magumu kwake.

Namuonea huruma sana kule alipotegemea rafiki yake alinifata akanambia kuwa ameshaachika nimsamehe nirudiane nae Sina mpenzi kwa sasa nimekua na chuki sana na mapenzi Sijui nina tatizo gani. Sifikirii kabisa kuwa na mahusiano kwa sasa.
 
Mwombe Mungu akupe mwngne huyo ni shetani, don't give her second chance
 
Muombe Mungu akuponye kidonda ulicho nacho moyoni. Akupe amani ya moyo. Huyo c wako... kwa maana akupendaye hawez kukufanyia dharau kiasi hiki kamwe.
Muombe Mungu akupe wako
 
Kidonse unatafuta mtu? Mbona hujamaliza sasa maelezo yako au inabidi wenyewe tu wakuonee huruma wajilete?
 
DAH WADADA KAMA HAWA WANAFANYA WANAUME WAWAOEWANAWAKE KAMA COBRA TU...MATUSI YOTEYA NINI SI ANGEKUACHA KWA AMANI.....HUYOACHANNA NAE FANYA KAMA ULIKUWA HUMJUI TU NA MAMBO YA KUOA AU KUWA NA MTU KWAKUONEANA HURUMA NI DISASTER MKUU...MOVE ON SLOWLY
 
Rafiki yake kakwambia umrudie? sasa unamrudiaje mtu ambae anaonekana pamoja na yote hana hata habari na wewe, wala salam yako hataki na kuonyesha msisitizo kakubloc koote. Move on bro
 
Usipende kushauriwa kwenye mapenzi kaa chini gikiria vizuri, Fanya maamuzi songa Mbele ukipewa pewa ushauri siku likitokea la kutokea utaanza kutapa tapa
 
Hii biashara ya mapenzi mara nyingi ni biashara ya hasara, wachache sana inawalipa.

Kama moyo umekuwa jiwe ndio biashara ya mapenzi utaiweza, ukiwa na moyo lege lege kwenye hii industry utaumizwa daily na kila siku we utakuwa unawekeza faida haionekani.
 
Matatizo ya kutongozewa, Mwanaume jiamini ww una uume ndani yako.
 
OA mwingine. Nenda kazini ukichekelea kama Hillary kumbe moyoni wewe ni Trump.
 
Back
Top Bottom