Mbona hata wanawake wanaoumiza bila sababu wapo wengi tu ... " hii mada ukitaka ui-jadili kwa fact unapaswa kuweka mbali mahaba ya kijinsia ya jinsia yako kando kwanza ... kisha uanze kuzitazama hizi changamoto zinazo sababishwa na hizi jinsia zote 2 katika Jamii .. ndio utakubaliana na mimi .. kinyume na hapo ..utaishia kubishana tu mkuu ..without logic consistent ...
Mkuu wanaume huwa tunaumizwa sana " ila huwa tunaficha" kwa sababu hatutaki kuonekana kuwa sisi ni viumbe dhaifu .. na ndio huwa tunakufa mapema pia kwa sababu huwa tuna ubebesha moyo mambo mengi ambayo mwisho wa siku huwa yanalipuka na kuzalisha maradhi na kuathiri mfumo mzima wa uzalishaji kinga za mwili .(hili haswaa huwa linachangiwa na uwepo wa stress za muda mrefu baada ya kufanyiwa ndivyo sivyo " na nyinyi "
Narudi kwenye msimamo wangu "
Men lier " Woman lier hakuna mwenye nafuu mkuu "
Sent using Jamii Forums mobile app
SEHEMU YA 59
“Halo meneja! Nipo na mke wangu, sidhani kama nitatoka,” alisema Theo hata kabla ya meneja wake kuongea kitu chochote kile.
“Theo! Una uhakika upo na mkeo?” aliuliza meneja, kwa jinsi alivyouliza, alionekana kama mtu aliyeonekana kukasirishwa.
“Ndiyo! Kuna nini? Mbona umeuliza kana kwamba huniamini?” aliuliza Theo.
“Umeingia Instagram?”
“Hapana!” “Hebu ingia kwanza halafu utaniambia kama upo na mkeo nyumbani ama la,” alisema meneja na kukata simu.
Theo akashtuka, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea ila hilo halikuwa tatizo.
Akainuka na kukaa kitako kitandani kisha kuingia Instagram.
Kwa sababu kulikuwa na watu wengi waliokuwa wameiposti picha ya mke wake, moja kwa moja macho yake yakatua kwa Violeth akiwa hospitalini huku uso wake ukiwa umelowanishwa na machozi.
Kwa jinsi alivyoonekana ilikuwa rahisi kugundua kwamba alichanganyikiwa. Hakujua ni kitu gani kilitokea lakini kwa namna ambavyo mwanamke huyo alivyokuwa, ilimpa picha kulikuwa na jambo baya.
Haraka sana akatoka Instagram na kumpigia simu mke wake, haikuwa ikipokelewa, bila shaka iliachwa nyumbani. Alihitaji kujua ni mahali gani alipokuwa, akaingia tena na kusoma comments za watu kuhusu picha hizo.
Zilimtia hasira kwa sababu nyingi zilikuwa ni za kumzungumzia yeye kwamba alimtelekeza mke wake, alimwacha hospitalini wakati akimuuguza mtoto wao.
“Hospitalini? Akimuuguza mtoto wetu?” alijiuliza Theo huku akionekana kuchanganyikiwa.
Hapo akapata jibu ya kile kilichokuwa kikiendelea, alimkumbuka daktari alipomwambia kwamba mtoto wao alikuwa na tatizo katika moyo wake, tatizo ambalo lingemfanya kupata matatizo muda wowote ule hivyo hakutakiwa kumwambia mke wake.
Moyo wake ulimchoma, aliendelea kusoma na kugundua kwamba alikuwa katika Hospitali ya Dk. Mjuni iliyokuwa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Hakutaka kuchelewa, hapohapo akasimama, akavaa nguo.
“Unakwenda wapi?” aliuliza Iyanya huku akimwangalia Theo.
“Mke wangu! Namuwahi mke wangu!” alisema Theo.
“Ila mimi ni zaidi ya mkeo kumbuka,” alisema Iyanya.
Shangazi nitaftie Theo nna matusi yake mengi sn [emoji36][emoji21][emoji21]
Nakusalimia [emoji113]Heri ya mwaka mpya mama kheri na baraka kwako na familia.[emoji8][emoji8]
Sent using Jamii Forums mobile app
Loh![emoji23][emoji23][emoji23]yaani inabidi mjieleze vzr mueleweke,
Wanaume mnajua kutuumiza pasina sababu,
Sie hungonja mkianza bc sie tunamaliza (kwa wenye ujasiri wa visasi ) hapo ni 80/20
Sent using Jamii Forums mobile app
SEHEMU YA 60
Theo hakutaka kuongeza kitu chochote kile, alichokifanya ni kuondoka na kuelekea huko hospitalini. Ndani ya gari alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya.
Moyo wake ulimpenda mno Violeth, alikumbuka jinsi mwanamke huyo alivyokuwa mzuri, alivyohangaika kumpata, hakutakiwa kumfanyia yote hayo aliyokuwa akimfanyia.
Alisikia hukumu nzito moyoni mwake, aliendesha gari kama kichaa mpaka alipofika hapo hospitalini ambapo moja kwa moja akaelekea ndani, tayari waandishi wa habari walikuwa wamekwishafika tayari kwa kuchukua matukio ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Walipomuona Theo, wakaanza kumpiga picha huku wengine wakimsogelea kwa lengo la kuongea naye. Siku hiyo alikuwa mkali kama mbogo, alichanganyikiwa, kitendo cha mtoto wake, Rachel kupelekwa hospitalini pale kilionyesha kabisa hali haikuwa nzuri, na kama angeleta masihara basi wangeweza kumpoteza.
Daktari alipomuona tu, akamsogelea, akamsalimia na kumchukua kuelekea katika chumba alichokuwa mke wake na mtoto, akaingia ndani, macho yake yalipotua kwa Violeth, machozi yakaanza kumtoka moyoni mwake, hakuamini pamoja na uzuri wa mke wake, jinsi alivyompenda leo hii alikuwa akimsaliti.
Haraka sana Violeth alipomuona mume wake, akasimama na kumsogelea kisha kumkumbatia na kuanza kulia tena huku akimwambia kwamba Rachel alikuwa akienda kufa kwa picha ile iliyokuwa kitandani ilimuumiza mno.
“She is going to die...she is going to die,” (atakufa...atakufa...) alisema Violeth huku akilia kifuani mwa Theo.
HV vitam tule wote marry wng!Yeeey bby tumepewa vitamu wacha tujilie [emoji39][emoji39][emoji39]
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante shangazi heri ya mwaka mpya na kwako pia
Hao ndio wanaume bwana
Hahaa kama haukubali shauri yako ...ila kama nimfuatililiaji mzuri wa mikasa inayo ufika huu ulimwengu kwa kupitia hizi jinsia mbili basi utanielewa tu ...Mi ngoja nisherehekee mwaka kwanza.
Kesho ntarudi hapa,napata tabu kukubali hiyo 50/50
Sent using Jamii Forums mobile app
embu usinitie hamasa mimi nikaenda kuliwa sasa hivi mimiUmeona eeenh kukulana kutamu jamani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]chizi weweSuruali zangu zote zipu ni nzima, hiyo zipu mbovu umeiona wapi?
woyooo nakupenda mieYeeey bby tumepewa vitamu wacha tujilie [emoji39][emoji39][emoji39]
Sent using Jamii Forums mobile app