Moyo Ulioonja Maumivu

Moyo Ulioonja Maumivu

SEHEMU YA 54

Maisha yakaendelea kama kawaida. Theo akawa makini kwenye kila kitu alichokuwa akikifanya. Alikuwa akiwasiliana na Iyanya kwa siri kubwa, hakukuwa na mtu aliyekuwa akifahamu.

Alimkumbuka mno, kitendo cha kukaa kwa muda wa siku kadhaa pasipo kuonana naye kwake yalionekana kuwa mateso makubwa mno. Alimwambia alitamani sana kumuona hivyo akamtumia tiketi ya ndege kwenda nchini Tanzania.

Hilo likafanyika! Haraka sana Iyanya akasafiri na kuelekea nchini Tanzania ambapo huko akapangishiwa hoteli ya kifahari na kukaa huko huku Theo akiahidi kwenda kuonana naye usiku wa siku hiyo.

Alihakikisha anajipanga, hakutaka kuona mke wake akishtukia kitu chochote kile, alimwambia kwamba alitaka kwenda kumalizia baadhi ya vipande vya ngoma yake ile ya kwanza Afrika Kusini hivyo mke wake akamruhusu kuondoka.

Hilo lilikuwa kosa kwani video ilikamilika ila alichokihitaji kilikuwa ni kwenda kuonana na Iyanya tu. Haraka sana akaelekea huko, akaingia hotelini mpaka chumbani na kwenda kuonana naye.

Walipoonana tu, wakakumbatiana kwa furaha, wakaangukia kitandani na kuanza kubusiana hapa na pale, wakaanza kubadilishana mate, walikumbukana mno na muda huo ulikuwa ni wa kufurahia maisha yaka walivyofanya nchini Afrika Kusini.

Theo hakutaka usumbufu kabisa, anapokuwa na Iyanya alihitaji sana kutulia naye, mawazo yake yawe kwa msichana huyo tu hivyo alichokifanya ni kuizima simu yake na kuiweka pembeni kabisa.

“Give me all you’ve got,” (nipe vyote ulivyokuwanavyo) alisema Iyanya, alimaanisha apewe kila kitu kitandani pale.

“I’ll give you my baby,” (nitakupa mpenzi) alisema Theo na hivyo hatua ya kwanza kabisa ilikuwa ni kuanza kushikana hapa na pale, saa ya ukutani ilionyesha tayari ilikuwa ni saa nne usiku.
Wanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA 55

Moyo wa Violeth ulipoa kabisa, hakumfikiria vibaya mume wake, kila kitu kilichokuwa kimetokea kilionekana kama video, hakufikiria kusalitiwa tena, kwake, mume wake alionekana kuwa mwaminifu kuliko mtu yeyote yule.

Hakufahamu kuhusu tatizo la moyo alilokuwanalo mtoto wake, Rachel, daktari na Theo walikubaliana wamfiche juu ya suala hilo kwani waliamini kwamba angepata matatizo zaidi kama tu wangemwambia kwamba hata yule mtoto aliyekuwa amenusurika alikuwa na tatizo hilo.

Ilipofika majira ya saa tano usiku, huku akiwa macho akimsubiri mume wake aliyekuwa na mwanamke mwingine, akashtuka kuona mtoto wake akianza kulia kwa sauti.

Alishangaa, kwa jinsi alivyokuwa akilia siku hiyo ilionekana kuwa tofauti na siku nyingine, alisikika akilia kwa maumivu makali, alishtuka hivyo kumuinua na kuanza kumwangalia huku akimbembeleza.

Upumuaji wake ulikuwa tofauti, ulifanana na mtu ambaye alikuwa akikaribia kukata roho. Alichanganyikiwa, kijasho chembamba kikaanza kumtoka, alihisi akitetemeka kana kwamba yeye ndiye alikuwa akiumwa.

Haraka sana akachukua simu yake na kumpigia mume wake ili ampe taarifa juu ya kile kilichokuwa kikiendelea, simu yake haikuwa ikipatikana kitu kilichomfanya kuwa na hofu kubwa.

Alikuwa chumbani, haraka sana akatoka huku akiwa amembeba na kuelekea nje, kulikuwa na gari lakini kwa jinsi alivyochanganywa na hali ya mtoto wake, akaona kama gari lingemchelewesha hivyo kutoka nje na kuanza kukimbia huku akielekea hospitalini.

Ilikuwa ni rahisi kusema mwanamke huyo alichanganyikiwa, alikimbia pasipo kuangalia nyuma, alikuwa na nguo ya kulalia tu lakini hakutaka kujifunga hata khanga, kwake, kuyaokoa maisha yake kilikuwa kitu muhimu kuliko hata kujisitiri.

Alikuwa akikimbia huku akilia, hakutaka kuangalia umaarufu wake, angeonekanaje, kwake, kuokoa maisha ya mtoto wake kilikuwa kitu cha kwanza kabisa.
Nani km mamamapenzi tele kwao na Mungu awabariki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitakaye mpenda atakuwa wa aina gani humu?
IMG-20181019-WA0008.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanazidi ya wanaume mweeh

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa sasa unataka league " na sio vinginevyo ... wanaume wengi huwa tunapatwa na misuko suko toka kwa wanawake .
Lakini kwakuwa ki-nature yetu huwa hatupendi kuielezea jamii kuhusu matatizo ambayo tunakutana nayo katika mahusiano ambayo huwa yana sababishwa na wanawake .
.. basi dunia inakuta inafahamu machache kuhusu sisi " na kuona kwamba hatuumizwi kivyovyote " kwa sababu jamii inakuwa ina uhaba wa taarifa za manyanyaso zinazo tuhusu ...

So tuko 50/50 hahahaahaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom