Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,330
Wanajamii naomba tuijadili hii changamoto kwa kina
Hivi kuna mapenzi ya kujilazimisha kupenda?
Na kama umejigundua ulipenda kusiko sahihi unaweza kumwambia mwenzio waziwazi kuwa unajilazimisha tu?
Nauliza maswali haya kutokana na kisa nilichosimuliwa na mtu wangu wa karibu sana (Mars) kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake (Venus), na hiki ndicho kilichotokea
Mars: Yaani pamoja na kukaa kwa miaka yote bado unasema hujanipenda na wala hujawahi kunipenda
Venus: Nakwambia kweli kwa miaka yote mitano, nimejitahidi mno kujiforce na kujiweka karibu sana na wewe lakini naona MOYO wangu mzito na unakataa kabisa kukupokea
Mars: Mbona nimekupa na nimekufanyia kila kitu kwa uwezo wangu wote?
Venus: Yaani wewe ni Mwanaume wa shoka, kila kitu nilichotaka nakipata na pia ni mzuri mno hata kwenye 6x6 na wala sina tatizo kwa hilo,
tatizo ni MOYO, nimejaribu kujibembeleza na kujipa moyo sana kuhusu mapenzi yangu kwako, lakini MOYO umekataa kabisa na najiona ni kana kwamba kuna kitu najidhulumu au nakudhulumu.
Nakwambia ukweli kwa miaka yote niliyokuwa na wewe sijawahi wala sina mtu wa pembeni,nilijaribu kukuweka karibu sana, lakini kuna kipindi nakuwa mpweke na kujiona sipo sahihi kuwa na wewe (kilio)
Mars: Tatizo ni nini sasa
Venus: Tatizo ni MOYO unakataa kabisa, najiona napwaya na nina hofia kuwa siku za mbele tutakuja achana kwa shida na matatizo, ni bora tuachane ingali mapema na mimi niupe MOYO wangu unachokitaka, kuliko kujilazimisha kuwa na wewe, naomba nisamehe kwa niliyosema (Kilio tena),