Movie ya Unknown

Movie ya Unknown

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,536
Reaction score
3,885
Image may contain: 3 people, text that says 'TAKE BACK YOUR LIFE. invngla LIAM NEESON UNKNOWN OnAns d FEBRUARY'

..Mkutano mkuu unaowahusisha wanasayansi wakubwa duniani..Dr. Martin Harris alipokea mwaliko..akafunga safari mpaka ujerumani..mkewe akiwa pembeni..

..Ni ndani ya mji wa berlin kwa ajili ya biotechnology summit..mkutano ulimuhusu dr martin..yeye kama mmoja wa madaktari wasomi,walioshiriki kikamilifu kutimiza mradi huo...

..Ni begi tu..ndio ni begi la dr martin lilisahauliwa na dereva taxi airport..akamwacha mkewe aandikishe majina hotelini..ye akakodi teksi nyingine ili aliwahi begi lake..

..Alikosea..angejua asingerudi..

..Ilianza ajali ya teksi aliyopanda..ikaja kupoteza fahamu kwa siku nne..na alipozinduka hakukumbuka chochote alichokuwa akikifanya hapo kabla..zaidi ya jina la mkewe na hoteli..

...Siku nne zilitosha kumhukumu martin kwenye maisha yake yote yaliyobaki..

alipofika hotelini alimkuta mkewe..alipotaka kuzungumza nae..alikutana na kitu kilichomshtua kuliko mwanamke kulala nje ya nyumba ya mumewe kwa siku mbili...

..Mkewe alimkataa..

..Na sio kumkataa tu..alikuja mwanaume mwingine akambusu mbele yake na wakakumbatiana..alipotaka kumjua mwanaume yule..akaambiwa anaitwa dr martin harris..what is this..

..Dr alichanganyikiwa..

..Yaani mkewe yupo na mwanaume ambae ana majina yote matatu yaliyofanana na ya kwake..ni ni hiki..

..Akaambiwa aoneshe vitambulisho kama anasema kweli..vitambulisho hana maskini..

..mume mwenzie alipoambiwa atoe vitambulisho alitoa pale pale..

..Na sio vitambulisho tu..hata picha zake na mkewe zipo ila kila penye sura yake ilikuwepo sura ya huyu mwanaume mpya..

..Kwenye picha ye kaenda wapi na picha alipiga yeye!!!..

..Atawaambia nini watu kuwa yeye ndo dr harris na wakati vitambulisho vyote vimepotea kwenye ajali na begi lake hajalipata!..

..Mtu kuiba utambulisho wake haikuwa kesi..ila kumchukulia mkewe ndo ilimuuma sana..na kwanini mkewe amsahau haraka vile!..

..Kama ni ajali alipata yeye..ye ndo alitakiwa amsahau mkewe sio mke amsahau mume..

..Dr martin aliumia..akauliza sababu ya kufanyiwa vile..akaitiwa mabaunsa kabla swali hajalimaliza..na majibu aliyopata yalimkuta kashafika nje...

..Afanye nini!..na nini asifanye!..

..Serikalini hawataki kumsikiliza kwa sababu kila penye ushahidi kuwa ye ni dr harris..ilikuwepo kila alama kuwa dr harris ni yule mume mwenzie...

..Ina maana huu mchezo umechezwa ndani ya siku nne!!..na walijuaje kila kitu kinachomuhusu yeye..mpaka shule aliyosoma na mpaka chakula alichopenda babaake!..

..Mpaka meseji alizokuwa anawasiliana na wenyeji wake ujerumani huyu mwanaume mpya alikuwa anazijua tena anazo kichwani...

..Anaishije kwenye mji wa watu ikiwa hata aliowafata wamemkataa..na bahati mbaya ni kuwa sura za waalikwa kwenye mkutano zilikuwa hazijulikani..

..kilichohitajika ni utambulisho wako na maelezo yako ya kidaktari kuhusu mkutano..dr harris alikuwa na udaktari tu..utambulisho ulikuwa umechukuliwa..

..Na aliechukua ana kila kitu..udaktari kama wake..na utambulisho wake...

...Dr harris akiwa hajui cha kufanya..risasi zilimfundisha cha kufanya...

..Ndio..sio tu kumchukulia utambulisho wake na kila kila kitu chake..dr martin alitakiwa kufa kabla ya siku ya mkutano..

..Kila alipokanyaga ndani ya ujerumani aliwindwa...hakuwa na pa kula wala pa kulala..njia pekee ya kupona kwenye hili ni moja tu..

..Ni kuurudia uanaume wake wa miaka 15 iliyopita..

..Dr martin harris akachoka kukimbia..akaurudisha umri wake nyuma..

..Alipanga kurudi kwao marekani..bila mkewe..lakini uchizi wa kumwaga damu ulipomjia kichwani..akakata shauri..

..Akaamua kuurudisha uhuru wa utambulisho wake na uhuru wa mkewe kwenye mikono yake..

..MWANAUME AKARUDI KAZINI..

..Wasiomjua wakamjua..sio daktari tena..dr martin ni mafia msomi...aliwaambia nimesahau kila kitu baada ya ajali..ila sijasahau jinsi ya kuua...

...Wawindaji wakawindwa..mji ulichafuka..kila ukweli uliofichwa ukafichuka..

...#Liam neeson kwenye ubora wake mwingine wa kufungua password ngumu..

...#LIAM NEESON CHAPTER
 
Image may contain: 3 people, text that says 'TAKE BACK YOUR LIFE. invngla LIAM NEESON UNKNOWN OnAns d FEBRUARY''TAKE BACK YOUR LIFE. invngla LIAM NEESON UNKNOWN OnAns d FEBRUARY'

Mkuu hizi nyuzi zako mbona ziko vizuri sana ebu panga movie kama tatu uwe unazielezea mzee uko good sana Kweli kwenye kusimulia itabidi niitafute nimepata hamu sana nikaipakue mzee 🙏🙏
 
Back
Top Bottom