Movie ya Equalizer

Movie ya Equalizer

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,536
Reaction score
3,885
Image may contain: 1 person, text




...Alipenda kutimiza ahadi..alijiapia mbele ya marehemu mkewe..kuwa angeacha kila kitu nyuma na kuanza maisha upya..

..kama mfanyakazi wa kiwanda cha Home Mart hardware store..angeishi kama raia wengine wema..

..Ndani ya jiji la boston..Robert McCall..aliyaishi maisha yake kipole..akimsaidia kila aliehitaji..na akipendwa na waliomzunguka..akawa hivo..

..Mchana anafanya kazi kwa bidii..usiku hapati usingizi kwa kusoma..
..Ndio..robert anaamini zaidi kwenye maarifa yaliyofichwa vitabuni kuliko kitu chochote..

..Alisoma..akasoma..akasoma tena..ni kwa kusoma huko ndipo alipokutana na Alina..
..Msichana muuza akili mpaka mwili..anaemilikiwa na mfanyabiashara maarufu wa madawa ya kulevya ndani ya boston..

..Alina ameichoka kazi ya kulala na wanaume zaidi ya 15 kwa siku..angefanya nini na hana pa kwenda..kula yake inatoka kwa tajiri huyu..hata lala yake pia..Alina ni mtumwa wa ngono asiejitakia..

..teenage prostitute chini ya mafia wa ki russia..mwenye mtandao mkubwa wa kishenzi ndani ya marekani..Binti huyu alikaa mbele ya robert..na alipojaribu kuongea nae wakaunda urafiki..

..Wala haikuchukua muda kujua kuwa alikosea rafiki..wanaommiliki msichana huyu walikuja kumpiga mpaka kulazwa...na kumkataza asikae na watu wasiokuwa na pesa kama robert..

..ye ni biashara..na anatakiwa kufanya vile anavoelekezwa na bosi wake...Alina alilia na machozi yake yakamsaliti pia....wala hayakumsaidia..

..akapelekwa hospitali..na Robert McCall akaenda kumjulia hali..rafiki yake mpya..ukiacha anaofanya nao kazi kiwandani..

..ni hospitali ndipo alipomjua mpaka bosi wa msichana yule..akafunga safari..akamfata..

..Akaweka dola 9800 mezani..kununua uhuru wa Alina..asiwe malaya tena..wakamwambia pesa tunachukua na Alina ataendelea kuwa malaya kwenye kampuni yetu..

..hawakujua..

..Alichomuahidi mkewe kabla hajafa..akakirudia tena..

..skillful close combat efficiency...Denzel Washington ni baharia mstaafu kwenye jeshi la Defense Intelligence Agency..binadam mwenye ukomavu wa kila kitu kwenye mwili wake..

..Ufundi na miujiza ya ajabu kwenye mapigano ya ana kwa ana ndo ilifanya marekani imtunuku kila medani ya shaba iliyohitajika kwa mwanaume shupavu..

..Akarudi nyuma..akaufunga mlango..ni kwa kutumia macho ndipo ilipoonekana mpaka muda ataotumia kuwakalisha watu chini..ni sekunde 16 tu..

..ndio ni sekunde 16 kila mtu ndani ya chumba kile alikuwa anapambania roho yake isitengane na mwili..kila wakijaribu kukumbuka ilikuwaje..ilikuwa haiwezekani..

..walikuwa wamepigwa ili wafe..kwa kutumia vifaa vyao wenyewe na kwa muda mchache..na kwa speed ya umeme..

..Akawaambia bora mngechukua pesa..wakafa kizembe..na washirika wao wakaja tena kizembe..

..Bosi wa russian mafia Vladimir Pushkin..akaandaa enforcer wake..wafanye uchunguzi na wamtafute muhusika..kweli akatafutwa na ni kweli walimpata...kilichotokea sasa!!!..

..#OLD IS GOLD..
..#EQUALIZER..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom