Movie ya EONII hakuna kitu

tabia ya kukatishana tamaa zipo kwenye damu za wabongo
 
JF kuna wajuaji kazi kukosoa tengenezeni yenu tuone mfano
Huhitaji kuwa mpishi kujua chakula hiki kiamu au si kitamu, huhitaji kuwa mwanamziki kujua huu muziki ni mzuri.
Mwisho wa siku masuala ya tupende vya kwetu huwa hayafanyi kazi watu wanapenda vitu vizuri. Ukitaka kujua watu ukitengeneza kitunkizuri cha ndani watanunua tu, ona watu wanavyopenda suti zinazotengenezwa local.
Sijaiona ila sikutegemea iwe woow, la msingi ni mwanzo baada ya hapo wataboresha zaidi na zaidi wakijifunza. Shida inakuwa zaidi kwenye story na script. Inawezekana ingekuwa simple sci-fiction story yenye script nzuri ingependeza zaidi
 
We director Adam Juma. Serious? Huyuhuyu tunayemjua wa video za miaka ya 2000s. Wangemhusisha Seko Shamte au kutafuta co-directors kutoka nchi jirani hususani bondeni.
Tatizo sisi hatujawahi kuwa serious. Unapoamua kufanya kitu fanya kweli usijaribu.
 
Hivi wewe muvi unaangalia kweli [emoji848][emoji848]
Mimi sio mtu wa movie lakini kwa akili ya kawaida unategemea uangalie movie ya kibongo huku ukiwa na comparison na movie za Hollywood ? budget, technology, experience, skills and knowledge zina fanana? siwezi kwenda kuangalia mechi ya Yanga na Simba huku kichwani nikiwa na fikira za Real Madrid Vs Barcelona
 
Sasa nani amefanya comparison
Mleta mada anasema hiyo movie ni mbaya. Yani ni mbaya tu in general bila kulinganisha na Hollywood wala nini

Muvi ya EONII kama Eonii ndio inayolalamikiwa hapa, mleta mada kaangalia amesema Ile movie hakuna kitu.

Movie za Kibongo nyingi hata usipozilinganisha na Hollywood, zenyewe kama zenyewe tu hazina mvuto
 
Tatizo la hii movie ipo below standard, ni movie ambayo watoto wakiangalia watafurahi lakini mtu mzima huwezi kuangalia hiyo movie ukafurahia. Imagine hata waingizaji wamemezeshwa maneno na anayeangalia anajua kabisa. Movie inaatakiwa iwe na ladha hii haina ladha mana mboga haina chumvi, mafuta, nyanya, vitunguu. Yani harage limechemshwa halafu tumepewa tule.
 
Mwanzo mzuri....Azam juzi walikua wanauza juice leo wako kwenye film industry kama kina TBC na IPP wangeendeleza hivyi tungekua mbali sio kila siku movie location ni mjini na kijijini tu watu wakipiga story za mapenzi.
 
Una low budget halafu unatengeneza movie ya sci-fi lazima utoe boko

Bongo bado hatuna script-writers wazuri sishangai kuona visa katika hiyo movie havieleweki
Hapa ndio shida ilipo hatuna script writers. Takataka zote wanazoonyesha Dstv Itv nk ni mbovu kwasababu script ni mbaya.

Hata uwe na camera nzuri, set design nzuri nk. kama script ni mbaya na content yako itakuwa mbaya vile vile.

Angalau maigizio ya Itv ya zamani walijitahidi kuwa na script nzuri ila sasa hivi ni sifuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…