Mkuu unafanya makosa kuziponda movies za kibongo pamoja na wale wanaoziangalia, kumbuka wewe ni mtanzania na utabaki kuwa mtanzania hata kama utapenda movies za ulaya na marekani au hata kama ukibadilisha uraia bado wewe ni mtanzania.
Kwa mantiki hiyo wewe una mama, mama wadogo na wakubwa, wajomba, baba, baba wadogo na wakubwa, mashangazi n.k, mimi ninaamini huwa wanaangalia movies za kibongo na wanazipenda, je ni sahihi kuwatukana kwa kuwaita 'waporipori'?
Nafikiri uache hiyo kasumba na badala yake toa maoni jinsi ya kuboresha hizo bongo movies ili watanzania na afrika tusonge mbele maana hiyo ni ajira wa watanzania wenzio ambao unawatukana