Mount Meru Hospital, Mlishindwa kujaribu Vertical House Construction?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,734
Hospitali ya Mount Meru Arusha kuna ujenzi umepamba moto tangu mwaja juzi nazani hadi sasa.

Eneo zima la Hospitali kwa haraka haraka ni kama heka 10+ na kinacho shangaza ni kwamba eneo lote limejaaa nyuma yaani kila kwenye nafasi upenyo basi inashuhswa jengo. Hospitali haina Parking kwa sasa make parking ilio kuwepo nayo waliona ni furusa wakaweka jengo.

Hakuna anaye waza Vertical labda haina ulaji kwao that is why wanakomaa na Holizontal.

Huwa nashindwa kuwaelewa Watalamu wetu kwakweli na hii ni kielelezo kwamba sisi Waafrica some time ni kama tulilaniwa vile.Yaani pale wamekutana ma engeneer wakaona waje eneo lote nyumba?

Hospitali inapaswa hata juwa na Garden kari sana make Garden tu ni tiba pia kwa wagonjwa na sio kujaza majengo uwanja mzima. Eneo lingetosha hata uwanja wa Helcopta ya wagonjwa kutua lakini wapi, imejazwa nyumba.

Wamissionaries ukiangalia Majengo yao ya Hospitali nyingi waliplan Hadi Garden lakini sisi nywele ngumu tunaona kama walikosea sana, Ile Hospital ya Hydom Mbulu Wazungu waliweka hadi Uwanja wa ndege yaani Air Strip, kwa wasomi wetu hakuna anaye waza kwamba Hospitali iwe na kiwanja cha ndege kidogo.

Ukiangali eneo lote limejaaa nyumba, na kwa mbeleeni wakitaka ku extend nazani watanunua kiwanja huko nje ya mji.
 
Back
Top Bottom