Picha: Moto walipuka katika Hospital ya Rufaa Mount Meru

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Moto Mkubwa umezuka katika hospital ya Mkoa Mount Meru na kutekezeza jengo la hospital hiyo linalotumiwa kama makazi ya wanafunzi wanaosomea udaktari


Tukio hilo la moto limezuka leo majira ya SAA 9.30 alasiri na kusababisha taharuki kubwa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo huku baadhi ya nguo ,magodoro na vitanda vikiteketea na vingine kuokolewa.


Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi .ambaye alikuwepo eneo la tukio amesema kuwa jengo hilo lilikuwa likitumiwa na wanafunzi wa udaktari wapatao 14 na tiyari serikali imechukua hatua za kufanikisha makazi mbadala


Baadhi ya waathiriwa wa tukio hilo,dkt Musa hausen ambaye ni mmoja ya wanafunzi wa udaktari aliyekuwa akiishi katika jengo hilo amesema kuwa moto umeunguza vifaa mbalimbali vya udaktari ,nguo,vitanda na magodoro .

IMG_20200627_164847.jpg
IMG_20200627_164922.jpg
 
Asee jengo lilikua limechoka kwelikweli hizo bati ni kilelezo tosha
Ukipata picha ya kabla ya ajali, hizo bati haziwezi kuwa hivyo.

Huo ni uchakavu uliosababishwa na kuunguzwa na moto.

Moto huo maana yake ulikuwa mkubwa sana, ukiangalia utaona bati hadi zinaning'inia, rangi kama mahame, kabla ya ajali hapawezi kuwa palikuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom