MOU si Mkataba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MOU si Mkataba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanaukweli, Nov 3, 2011.

 1. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Memorandum of Understanding si mkataba ni makubaliano ya pande mbili ambayo hayajafikia hatua ya mkataba.

  Kawaida pande mbili zinazoshirikiana katika shughuli fulani muhimu hupenda kuweka makubaliano ya ushirikiano wa shughuli zao kwa maandishi. Makubaliano hayo kawaida yanaeleza:
  (1) Pande husika katika makubaliano,
  (2) Mambo wanayokubaliana na malengo yake,
  (3) Majukumu ya kila upande katika ushirikiano, na
  (4) Saini za Wawakilishi wa pande mbili.

  Ni makubaliano na si mkataba. (It is a gentlemen way of spelling out agreement).

  MoU haina nguvu ya kisheria.

  Wikipedia ina define MoU hivi
  A memorandum of understanding (MOU) is a document describing a bilateral or multilateral agreement between parties. It expresses a convergence of will between the parties, indicating an intended common line of action. It is often used in cases where parties either do not imply a legal commitment or in situations where the parties cannot create a legally enforceable agreement. It is a more formal alternative to a gentlemen's agreement.

  Memorandum of Understanding kati ya Makanisa ya Kiprotestanti na Katoliki kwa upande mmoja na Serikali, inatokana na ukweli kuwa Makanisa yamekuwa yakitoa huduma za jamii ambazo ni jukumu la msingi la Serikali. Huduma za Tiba zitolewazo na kanisa ziko zaidi katika maeneo ya vijijini ambako Serikali bado haijaweka huduma hizo. Ushirikiano huo ni msaada mkubwa kwa serikali ambayo ingepasika kuwajibika kwa raia wake wote hata hao wa vijijini kwa huduma hizo.

  Vilevile wilaya nyingi zilizoanzishwa miaka ya baadaye baada ya uhuru hazikuwa na hospitali za serikali zenye hadhi ya kuwa Hospitali za wilaya na Serikali imeomba ushirikiano wa Kanisa kutumia hospitali zake kama hospitali teule za wilaya. Mfano: Nkansi, Bunda, Sumve, Rombo n.k.

  Kwa haraka nimepitia Hospitali, vituo vya afya na zahanati za makanisa yaliyosaini MoU hiyo na kupata 564. Hizi karibu zote zilikuwepo wakati wa kusaini MoU hiyo.

  MoU kati ya Kanisa na Serikali inaongelea suala la huduma za jamii tu, haihusiki na mengineyo.

  Suala ya misaada ya fedha si kwa hospitali zote, zaidi ni zile Teule na za rufaa, ambazo Serikali inazihitaji.

  Bado Makanisa yanabeba jukumu kubwa la kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati. Waumini wanajua jinsi wanavyochangishwa kwa ajili ya kuchangia ujenzi na ukarabati na wakati mwingine hata kuziendesha taasisi hizo.

  Nimeweka attachment ya zahanati, vituo vya afya na Hospitali za Makanisa ili muone jinsi huduma hiyo ilivyoenea vijijini (remote areas).

  Nimeweka attachment ya pili ya pdf inayoonesha kuwa Serikali ya Ujerumani inapitishia baadhi ya misaada yake ya huduma za jamii kwenye shirika la misaada la Misereor, ambalo ni la Kikatoliki. Angalia title ya mwisho "MISEREOR has strong Supporters".
   

  Attached Files:

 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Maelezo mazuri tu, ila wakija hawatatambua hilo
   
 3. C

  Chogo matata Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ulieandika hii thread una jicho moja usiulize kwanini
   
 4. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni terminology ya kisheria na maana yake ni hiyo.

  Kwa nini isiitwe Contract bali MoU?

  Hata mtu binafsi kama ana shughuli muhimu anashirikiana na serikali anaweza kusaini MoU.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  kina faiza fox watajileta hapa sasa hivii na udini wao
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Nimefurahi kuhusu tafsiri hii, hata Muungano wetu, sio mkataba ni makubaliano tuu. Ndio maana hatuna mkataba wa muungano ila kuna hati za muungano, articles of the union zilisainiwa na mtu mmoja tuu na mwingine alipaswa japo aweke saini ya dole gumba, hakuweka na mpaka leo articles hizo are no where to be seen!.
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Weka na shule mkuu...
   
 8. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Nikitoka kazini mkuu..
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ngoja ustaadh kapungu alione bandiko lako.
   
 10. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  msubirin Mohamed Saidi. Faizafoxy, na topical waje na mapepa yao sasa hivi mtawaona.
   
 11. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Taasisi ya KiIslamu ya AGA KHAN pia ina MOU na serikali na ndio ilikuwa ya kwanza kabla ya hizo za Makanisa
   
 12. K

  Kasesela Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The legal nature of M.O.U essentially rests on the nature of rights, obligation/duties or legal relationship it creates among the parties. No doubt, it embodies understanding
  of the parties in principle, however all understandings do not mature in contracts
  or in other words may not result in conferring of rights and imposition of duties and as such
  can not be enforced by the legal process.

  As per Section 10 of the Contract Act 1872 (UK), the essential requirements of a legally
  binding agreement are as follows: -
  a) There must be offer from one party and its acceptance by another,
  b) Consent of the parties must be free,
  c) Parties must be competent to contract,
  d) There must be lawful consideration,
  e) There must be lawful object.
  f) There must be intention to create legal relations

  In a pure and simple MOU, there may be offer and acceptance among competent
  parties with their free consent and object may also be lawful but still no binding relationship
  is created or come in to existence because when it is tested on the touchstone of above
  ingredients it emerges that MOU lacks consideration and intention to create legal relationship.
   
 13. d

  dotto JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kati ya orodha hiyo ambayo jumla yake ni 564, zahanati na hospital 364 ni za RC! Kuna kipindi Serikali hii legelege ilitaka kuwaletea fujo za kodi. Na jamaa wa pedo vipi!
   
 14. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tunashukuru kwa tafsiri hii, ila watakuja wakiwa wamefumba macho na watachonga. Hawajui kama Agakhan iliandikiana MOU na serikali lakini kwa kuwa ni Muslim basi hilo haliwahusu, mbaya zaidi hizo hospital za agakhan hata kuzitumia hawazitumii na zipo centered mijini tu na maskin kama mimi bei zao hata siziwezi. Unakuta na pedal zao wanajaa kwenye kwenye hospital za makafiri. Waswahili bwana wakiwa wazima wanabwabwaja sana wakiugua wanaawasaliti hata wenzao wanaopinga. Shauri ya bima sewikalaga baho na ubwanzi wako
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hii issue licha ya JK kuitolea ufafanuzi wakati wa baraza la Iddi lakini bado maelezo ya kina yanatakiwa kutolewa na waziri wa afya. Maana kuna watu wamepotosha na wanazidi kupotosha dhana nzima ya MOU kati ya serikali na makanisa. Pia nadhani ni wakati mzuri kwa rais wa awamu ya pili atoe ufafanuzi kwa ndugu zake ambao wanaendelea kubeza kazi nzuri inayofanywa na mahospitali ya Kanisa.
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii ishu tusiiangalie tu kwa jicho moja. Hebu tujiulize, hivi hizo hela zinazoenda huko huwa zinafanyiwa auditing? Kama ndiyo anafanya nani? Je Ludovick Uttoh (Government Chief Auditor) huwa anatumaga vijana wake?
  Kwa taarifa yenu zaidi ya 50% ya bajeti ya wizara ya afya inayotumwa kwenye taasisi za afya zinaenda kwenye taasisi za makanisa. No auditing, no anything. This is terrible men/women kwa kodi za waTz kutokujulikana kimaandishi kuwa zinafanya nini zaidi ya kufikirika tu kuwa zinatoa huduma. Who knows hata kama zinaenda kuwalipa makasisi mishahara au wanatumia kutangaza imani yao.
  Narudia tena, Haya madai ya waislam/watanzania si ya kupuuza hata kidogo. Nina mengi ya kuwaeleza ila ndo hivyo muda hauniruhusu.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Kwa vile ni taasisi za dini, wamemtanguliza Mungu, hawawezi kabisa kuiba au kufanya matumizi mabaya ya fedha. Kwanza huduma tuu zinazotolewa bila usaidizi wa serikali ni mara dufu ya kinachotolewa na serikali, huo mchango wa serikali ni peanut halafu ije ifanywe auditing gani kwenye peanut?!.
   
 18. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Asanteni nimepata kakitu hapo
   
 19. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2011
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  District Designated Hospitals zinazomilikiwa na makanisa zinaongozwa na District Medical Officer, ambaye ni mwajiriwa wa Serikali. Anatoa ripoti serikalini kama kawaida na mahesabu yanakaguliwa na CAG.

  Vituo vingine vya afya, dispensaries na hospitali nyingine zinajiendesha zenyewe na hazipati pesa yoyote toka serikalini.

  Kama una ushahidi tuwekee hapa.
   
 20. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2011
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  1. Ni hospitali za Teule za wilaya kama Sengerema, Huruma-Rombo, Namanyere-Nkansi n.k, na za rufaa KCMC na Bugando ndio zinapata fedha toka serikalini. Fedha zenyewe zinakuwa kwenye bajeti ya wizara ya afya. Kuna fungu maalum kwa ajili ya Hospitali za rufaa. Pia kila wilaya inatengewa fedha zake za huduma za afya. Pale ambapo hospitali teule ya wilaya inamilikiwa na kanisa ndipo tu ambapo fedha hizo zinaenda. Mganga mkuu wa wilaya anaripoti wizarani, na mahesabu yanakaguliwa.

  2. Hospitali nyingine zote za kanisa zisizokuwa Hospitali teule za wilaya wala za rufaa hazipati fedha yoyote toka serikalini.

  3. Hakuna shule yoyote ya kanisa inayopokea msaada wowote toka serikalini.

  4. Hata kabla ya kusaini MOU mwaka 1992 serikali ilikuwa ikitoa fedha hizo na hakikubadilika kitu chochote.
   
Loading...