Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 198
- 209
MOTO WAZIDI KUWAKA UWT K'NJARO,WANACHAMA WATISHIA KUREJESHA KADI ZA CCM
HALI bado si swari ndani ya Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT)baada ya wanachama wake na wale walioenguliwa katika kinyang'anyiro cha kura za maoni kutishia kurejesha kadi za Umoja huo endapo mamlaka za juu za chama hicho hazitaurejea mchakato huo..
Tishio hilo la wanachama linakuja siku chache baada ya madai kuwa viongozi wa UWT mkoa wa Kilimanjaro waliwaengua wanachama wenzao kutokana na kuwa na majina ya wagombea mfukoni.
Wanamtuhumu mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoani Kilimanjaro,Elizabert Maro Minde kumsaidia kushinda mmoja wa wagombea hao, Zuena Bushiri na baadae kuhudhuria sherehe ya kupongezana nyumbani kwa Zuena kata ya Kiusa Manispaa ya Moshi.
Kutokana na shutuma hizo kuendelea kushamili,Elizabert Minde amejitokeza na kutupilia mbali shutuma hizo na kudai ucaguzi huo ulifanyika vizuri huku akikiiri pia kuhudhulia sherehe ya kupongezana nyumbani ka Zuena Bushiri.
"Kusherehekea ushindi ni jambo la kawaida mimi nisingeenda kula na watu wakati nimeshapata Ubunge,Mbunge aliyebaki Moshi wakamuona na kwenda kusherehekea naye alikuwa Zuena mwingine hatujui tuliambiwa ameondoka ameenda Arusha kwa hiyo tungeenda kumfuata huko Arusha?" alihoji Minde.
Ameongeza kuwa hata watu waliokuwa wanamsaidia huyo anayelalamika walikuwa nyumbani kwa Zuena kwa sababu tayari wameshapata wabunge.
"Mimi nilienda kumuangalia kama ameshafika nyumbani nikakuta watu wamekaa ningekimbia,nimesimamia chaguzi nyingi sana watu wakimaliza wanampeleka mgombea wao nyumbani wakifika wanaagiza soda wanakunywa kwani wamevunja sheria gani?" alisema Minde
Akijibu kuhusu baadhi ya Wilaya ambazo zimelalamikiwa kutokuwa na watia nia Minde amesema kuwa utaratibu ni kila nafasi moja kubeba watu watatu na kwenye idadi ya watu 28 walipaswa kupeleka majina 6.
Amedai kuwa hakuna Wilaya ambayo haikuguswa na kwamba walikuwa waangalia, ushiriki wawatia nia katika chama,mchango wao na namna wavyokisaidia Chama na si vinginevyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wagombea hao ambao majina yao yameenguliwa wamesena Mwenyekiti aliwabeba wagombea hao wawili ambao walipata ushindi kwa kulipa fadhila.
Wamesema kutokana kitendo alichokifanya Mwenyekiti wao, hawana imani nae tena na kwamba wako tayari kurejesha kadi za Umoja huo, na kwamba hawatashiriki shughuli zozote zinzahusu wanawake.
kama hukubahatikana kusoma andiko langu juzi basi nanirejea tena hapa uendeleee kusoma
Huko mkoani Kilimanjaro hali si shwari ndani ya Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha mapinduzi(UWT)kutokana na kilio cha wanachama wake kulalamikia vitendo vya rushwa,kujuana,upangaji wa matokeo na upendeleo katika kwapata washindi wa kura za maoni ndani ya jumuiya hiyo.
Kinacholalamikiwa na wengi ni kwamba wanachama wenye ushawishi na wenye sifa walienguliwa katika kinyang'anyiro hicho na viongozi wa UWT mkoani humo akiwamo mwenyekiti wao Elizabert Maro Minde na katibu wake Jane Chatanda lengo ni kuwawezesha watu wao kushinda bila vikwazo.
Wanasema wilaya zote saba za mkoa wa Kilimanjaro zilitoa watia nia lakini cha kushangaza wilaya nyingi majina ya watia nia hayakurudi kabisa si kwa sababu wagombea hao hawana sifa hapana hii ni kutokana na mwenyekiti,Elizabert Minde kuwa na mtu wake aliyekuwa akimhitaji.
"Hata baada ya kumalizika kwa uchaguzi mwenyekiti alienda kwenye sherehe ya mmoja wa walioshinda ni kwa sababu ndiye alikuwa chaguo lake na huyo ndiye aliyempigania akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa UWT mkoo wa Kilimanjaro kwa hiyo alikuwa analipa fadhila",anasema mmoja wa waliokuwa sehemu ya watia nia ambaye jina lake lilienguliwa.
"Rushwa imetumika sana kwenye huu uchaguzi,sisi hatuna shida na chama chetu cha mapinduzi na kina nia njema kabisa lakini uharamia umetumika ndani ya UWT,haiwezi ingia akilini kwamba wapinzani wote wa Zuena Bushir hawana sifa hapana hii ni kwa sababu ya rushwa lakini kwa nini mwenyekiti awe na mgombea wake?",amehoji mtu mwingine.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utekelezaji UWT mkoani humo anatajwa kuwa alikuwa akimpigia kampeni mmoja wa watia nia kitendo ambacho kinadaiwa kuwa ni kinyume kabisa na taratibu za uongozi kwani mjumbe huyo ni sehemu ya viongozi wa kutoa maamuzi.
Kwa nini upangaji wa matokeo?,watia nia hawa wanasema ukiangalia aliyeongoza kwenye kura Esther Maleko aliyepata kura 1149 na wa pili Zuena Bushir (kura 964) na Regina Chonjo aliyepata kura 145 ni dhahiri kuwa kulikuwa na upangaji wa matokeo.
Kwenye mchakato huo,Caroline Lyimo alipata kura 109,huku Never Zekeya akipata kura 108 wakti Pamela Mallya akipata kura 69 ambapo mary nashenda alipata kura 19 na wa nanne alikuwa Haika Ngowi aliyepata kura 12.
Walionguliwa katika kinyang'anyiro hiki ni Rusma Ndosi kutoka wilaya ya Hai ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kilimanjaro,Sophia Virgo,Edna Mafue na Winnie Jonas,mwingine ni Khadija Kangero kutoka wilaya ya Rombo na mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Rombo.
Wilaya ya Same aliyeenguliwa ni Namrinji Mzanza mfanyabiashara na mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya UWT mkoa wa Kilimanjaro,mjumbe wa Halmashauri kuu ccm wilaya na pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya,yupo pia Edith Banzi diwani aliyemaliza muda wake.
Kwenye wilaya ya Mwanga yupo Clara Mdee huyu anatajwa kuwa ni mmoja wa makada mashuhuri katika wilaya ya Mwanga .
HOJA YA UKOMO WA VITI MAALUM IKOJE?
Chama cha mapinduzi kimeweka ukomo kwa wabunge wa viti maalumu waliokaa muda mrefu kwenye nafasi hiyio na kanuni hizo zitaanza kutekelezwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2030 lakini katika mkoa wa Kilimanjaro kanuni hiyo imeanza kutekelezwa kabla ambako Shally Raymond alienguliwa kwa kigezo hicho.
Lakini mkoani Simiyu miongoni mwa watia nia alikuwemo Esther Mdimu ambaye amekuwepo kwenye nafasi hiyo tangu mwaka 2005 na katika uchguzi huu jina lake lilirudi na amekuwa sehemu ya washindi,yupo Catherine Magige wa Arusha,yupo Liziki Rulida wa Lindi naye ni moja wabunge wa muda mrefu hawa majina yao yalirudi lakini wameangushwa kwenye sanduku la kura.
Hapa unaweza kuona wanaokichafua chama cha mapinduzi ni hawa viongozi wa hizi jumuiya ambao wamekuja na agenda zao za kuwa na wagombea kwenye mifuko yao,una maoni gani kuhusiana na hizi tuhuma za upangaji matokeo,kubebana na matumizi ya rushwa?