Moshi, Kilimanjaro: Moto unateketeza majengo na vifaa mbalimbali vya ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme (Tamesa)

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Jengo la ofisi za TANROADS mkoani Kilimanjaro linateketea kwa moto.

Taarifa zaidi kukujia.

====

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika, umezuka kwenye Ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) mkoani Kilimanjaro ambapo magari kadhaa yanaungua na kuna hatari kisima cha mafuta ya serikali kuwaka na juhudi za kuukabili zinaendelea.

======

Moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana umeibuka katika bohari ya mafuta ya Serikali katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, leo Machi 25, 2022.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jitihada za kuendelea kuuzima zinaendea ambapo amesema atatoa taarifa zaidi.

Pia soma;

Moshi. Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana, unateketeza majengo na vifaa mbalimbali vya ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme (Tamesa) mjini Moshi.

Mashuhuda mbalimbali wameieleza Mwananchi Digital kuwa moto huo ulianza saa 11:30 alasiri leo Machi 25, 2022 katika ofisi hizo za Tamesa ambazo zipo karibu na Bohari ya Mafuta ya Serikali na ofisi za Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Kilimanjaro .

Mwananchi Digital imeshuhudia jitihada mbalimbali za uokoaji zikiendelea ambapo waokoaji walikuwa wanahamisha magari ya serikali na vifaa ili visifikiwe na moto.

Nao wafanyakazi wa duka la samani lililo karibu na ofisi hizo za Tamesa wamefanikiwa kutoa samani na kuziweka barabara ya Kristu Mfalime kuelekea mzunguko wa magari wa Bonite.

Hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyepatikana kuzungumzia moto huo, lakini Afisa Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari cha TPC anayeshughulikia Utawala, Jaffar Ally akizungumza kwa njia ya simu amesema tayari wametuma gari la Zimamoto kwenda Moshi kusaidia kuzima moto huo.

"Ni kweli nimepokea simu kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Moshi juu ya moto huo mkubwa na tayari tumeshatoa gari letu limeelekea huko,"alisema Ally.
 
Jengo la ofisi za TANROADS mkoani Kilimanjaro linateketea kwa moto.

Taarifa zaidi kukujia.

====

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika, umezuka kwenye Ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) mkoani Kilimanjaro ambapo magari kadhaa yanaungua na kuna hatari kisima cha mafuta ya serikali kuwaka na juhudi za kuukabili zinaendelea.

======

Moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana umeibuka katika bohari ya mafuta ya Serikali katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, leo Machi 25, 2022.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jitihada za kuendelea kuuzima zinaendea ambapo amesema atatoa taarifa zaidi.
View attachment 2164303
Moto wa mchongo
 
Ingewaka ya Dodoma maana Mizani ya Nala imekuwa kero kubambikia watu uzito.
 
Jengo la ofisi za TANROADS mkoani Kilimanjaro linateketea kwa moto.

Taarifa zaidi kukujia.

====

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika, umezuka kwenye Ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) mkoani Kilimanjaro ambapo magari kadhaa yanaungua na kuna hatari kisima cha mafuta ya serikali kuwaka na juhudi za kuukabili zinaendelea.

======

Moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana umeibuka katika bohari ya mafuta ya Serikali katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, leo Machi 25, 2022.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jitihada za kuendelea kuuzima zinaendea ambapo amesema atatoa taarifa zaidi.
View attachment 2164303
Ni ofisi za Tamesa Moshi.
 
Back
Top Bottom