mtoa mada ameonyesha udhaifu mkubwa sana kimalezi. Ni udhaifu mkubwa; ni unyanyaji kwa kumpeleka mtoto mdogo shule ya kulala. Watoto wadogo wanahitaji uangalizi wa karibu wa wazazi ili kujua miiko, mila, tamaduni n.k vya jamii yao. Waswahili wanasema "kazi sio kuzaa mwana, bali kulea mwana. Naona wazazi walielimika wanazaa kisha kuwapa watu hela za kulea watoto wao ili hali bado wadogo. Hao wafanyabiashara wakiboronga, wazazi au walezi husika wanathubutu kulalama hadharani.
Jaribu kujiuliza, hao abiria kwenye klm walipataje adha ya kuwatunza watoto wa watu walioelimika na kutajirika kisha kusahau majukumu yao ya msingi kama wazazi.
Huyo mtoto (kimoyomoyo) anamlaumu mzazi kwa unyanyasaji anaoupata, kisha baadaye anawalaumu waalimu na walezi wa shule. Unyanyasaji aliofanyiwa hautafutika kirahisi moyoni mwake.
Serikali kupitia wizara ya elimu imeshakataza kupeleka watoto wadogo shule za kulala, ila kuna watu wanaona 'kuwatesa' kwa sababu dhaifu sana ya 'elimu bora, ni ufahari.
Alichofanya mtoa mada kisaikolojia kinatafsiriwa kama projection.
"kila mtu atavuna alichopanda", kila mtu atabeba mzigo wake"