Moshi academy huu ni zaidi ya unyama

Moshi academy huu ni zaidi ya unyama

SUYA

Senior Member
Joined
Jun 24, 2009
Posts
131
Reaction score
21
Nko hospital TMJ mwanangu kapakiwa leo kwenye basi la Kilimanjaro bila taarifa kwa wazazi.Ni bahati tu mlezi wake shule kuulizia kama mtoto wake alifika salaama maana kama sio yeye sijui ingekuwaje.Nimemkuta mwanangu stand analia na kutapika bila msaada wa matron wala kutumiwa sms kuwa mwanangu anakuja kutoka shule.

Ni aibu kubwa kwa shule kama Moshi Academy kufanya mambo ya kijinga mnathamini hela kuliko utu, kuweni na utaratibu mzuri wa kusafirisha watoto. Bag lake limepotea staki kuamin eti mlitangaza kwenye radio na tv mnafikiri watu wote wanaskiliza radio? na namba za simu tulijaza za nini?

update

mpaka leo bag la mtoto halijapatikana mkuu wa shule tarimo nashukuru kwa uamuzi uliotuahidi kulipa vitu vyote vya mtoto napenda ufahamu kuwa thamani ya mtoto haifananishwi na kitu chochote licha ya kujitetea kuwa kuna mzazi mlimkabibhi watoto, na wazazi wanaokaa dar walipitisha utaratibu wa wa kusafiri mmoja wao na watoto. Napenda nikuambie kuwa huo utaratibu sio mzuri na haufai hata kidogo ,jaribu kufikiri mtoto angepotea ungeniambia umempa mzazi fulani nani angekuelewa? Je sku nilimkabidhi nani huyo mtoto sku anakuja shule? Pili sio wazazi wote wenye uchungu na watoto kwani wapo wanao tupa watoto wao wa kuzaa wenyewe iweje mtoto wa mtu mwingine?
Tunasubiri kuona yale uliyoahidi yanatekelezwa.na sio maneno matupu
jambo hili stakaa nilisahau sku hiyo ilikuwa ngumu sana kwangu.
 
pole, watoto kama wadogo msiwapeleke bording............. Shule zenyewe hizi zinajali pesa tu sio utu....

Pole sana
 
Pole sana ndugu yangu ila as said by others acheni jamani kutesa watoto wadogo kwanza masafari marefu hivi tafuteni mashule humu humu hata za boarding Mbona ziko at least you will be near unapunguza na usumbufu kma huo,imeniuma sana ningekuwa wewe hata next year nisingerudisha my child Huko kamwe.Namna hiyo Iam sure hata huyo mtoto Hana tena mapenzi na shule iyo,to hell with their academy!
 
Mlete hapa Saint Kayumba mwaya pole sana hzo Saint mabasi ndio zilivyo
 
Nko hospital TMJ mwanangu kapakiwa leo kwenye basi la Kilimanjaro bila taarifa kwa wazazi.Ni bahati tu mlezi wake shule kuulizia kama mtoto wake alifika salaama maana kama sio yeye sijui ingekuwaje.Nimemkuta mwanangu stand analia na kutapika bila msaada wa matron wala kutumiwa sms kuwa mwanangu anakuja kutoka shule.

Ni aibu kubwa kwa shule kama Moshi Academy kufanya mambo ya kijinga mnathamini hela kuliko utu, kuweni na utaratibu mzuri wa kusafirisha watoto. Bag lake limepotea staki kuamin eti mlitangaza kwenye radio na tv mnafikiri watu wote wanaskiliza radio? na namba za simu tulijaza za nini?
Pole sana mwanangu. Ulikuwa huijua Moshi. Pesa babaangu. Rua!
 
sasa mkuu dar yote umekosa shule mpaka umpeleke mbali kote huko?

ila pole
so TMJ umempeleka hosp au?
kukaa tu stand hosp? kweli maisha ya kichina
 
Nko hospital TMJ mwanangu kapakiwa leo kwenye basi la Kilimanjaro bila taarifa kwa wazazi.Ni bahati tu mlezi wake shule kuulizia kama mtoto wake alifika salaama maana kama sio yeye sijui ingekuwaje.Nimemkuta mwanangu stand analia na kutapika bila msaada wa matron wala kutumiwa sms kuwa mwanangu anakuja kutoka shule.

Ni aibu kubwa kwa shule kama Moshi Academy kufanya mambo ya kijinga mnathamini hela kuliko utu, kuweni na utaratibu mzuri wa kusafirisha watoto. Bag lake limepotea staki kuamin eti mlitangaza kwenye radio na tv mnafikiri watu wote wanaskiliza radio? na namba za simu tulijaza za nini?

Mkuu nakushauri fuatilia hili swala kwa kina kujua kulikoni mwanao mdogo asafirishwe toka Moshi kuja Dar bila mlezi na bila taarifa kwako mzazi! Hii inanipa wasi wasi mkubwa kwamba hata huko shuleni uangalizi wa hao watoto ni dhaifu sana! Hao ma-matroni + patroni watakuwa hawana nafasi na malezi ya watoto,wanachojali ni marupurupu yao tu na watoto wanajilea wenyewe! Mpaka mzazi uje kugundua kuwa mwanao keshabadilishwa mwelekeo (ulawiti/usagaji) itakuwa tayari ni too late!
Please,hili si swala la kubonyezea keyboard ukiwa nyumbani, wajibika kama mzazi unayetambua ni nini maana ya malezi!
 
Naitamani ile enzi kama ingeweza kurudi.
Mie s/msingi nilisoma mita 250 toka nilipokuwa naishi!
Siku hizi mtoto wa miaka3 yuko boarding!
Wazazi hivi kweli tuko serious au ni mambo yakufuata mkumbo..?!
 
Yule mmiliki wa shule ni mbumbumbu sana, na hat ahizo shue kazipat akiujanjaujanja na anaendesha kiujanja ujanja kama kibaraka fulani wa watu fulani.Kila nikipita kuelekea arusha nikiangalia Northern Highlands school pale makaburini natamani kuipiga bomu.Nafikiria moto na possible ways za kuokoa watoto sioni.Jamaa kajenga ghorofa ndefu, ina ngazi nyembamba sana ktk panic wanafunzi hata watatu hawawezi pita.Hana ngazi ya nje kwa vile hakuwahi jiuliza what if moto unaanzia ghorofa za chini "ana helcopter za kuokoa?".Mbaya aliwahi jiua mwanafunzi mmoja, kwa kujitupa ghorofani ,kajamaa kwa ujinga kakatafuta quick fix kwa kuziba kila kitu kote na kuach access pekee kuwa vingazi vidogo na vichache kuserve floors zote.

huw anikiangalia ile shule nanchukia kabisa Pinda, Pinda kahudhuria sana mahafali ya kuhitimu wanafunzi pale na sijui kama issue ya security ili click ktk kichwa yake.

Sikuwa najua kwanini mambo yalikuwa hovyo sana shule za huyu jamaa hadi pale nilipoambiwa kajamaa kalikuwa failure fulani pale mawezi , halafu kaka bebwa na wakubwa zake,kilipopata deal ya shule ndipo kikjiweka ktk maisha kiliyo nayo.

Mara yangu ya kwanza ongea na haka kajamaa nilitaka tapika kalivyokuwa kakijishaua kw akutaja majina ya wakubwa na kuongea nao ktk staili ya wapiga debe wa CCM wakiwa mjini.Ile staili kila laiye karibu hata aisyetaka igilia privacy ya mtu asikie anaongea na nani.
 
shule za kichagga hizo

teh teh..mkuu kwani shule ngapi nzuri si za kichaga?hembu hesabu haraka haraka hapo dar, moro,Arusha, tanga, Mwanza etc si wa kichaga?hata za mission uwezekano wa kumkuta sister wa kichaga ndio alianzisha ni mkubwa sana.

hata versity za watu binafsi zipo za wachaga.Kama wanaweza kuwa na kuazia vijiwe vya kuuza pua , miguu ya ng`ombe, utumbo na nyeti hadi kuwa na five stars hotels and restaurants, kwanini na shule isiwe hivyo?Hakuna sijui za kichaga ila command waliyo nayo kwa biashara yoyote.
 
Naungana na mdau alietoa mada. Binafsi jana niligeuka kuwa mlezi. Nilisafiri na KLM iliyotoka moshi saa 8:00 ambayo ndo ilikuwa na hao watoto. Nilikaa na mtoto mdogo kama miaka 5 au sita wa kike. Alikuwa anatapika sana, na nilijitahid kumpa care ya hali ya juu. Hata hela ya chakula njiani hawakupewa zaidi ya kalenda walizopewa. Huu ni unyanyasaji wa watoto. Niliumia sana
 
Mkuu,nimemshauri hapo juu huyu mleta mada kuwa haitoshi kukalia keyboard nyumbani Dar na kutuma uzi JF! Kama kweli ni mzazi anayejali anapaswa kufuatilia kwa undani swala hili ili kubaini tatizo liko wapi na achukue hatua staiki! Kama wameweza kufanya hili ina maana kwamba hata yale malezi ya kila siku ya watoto huko shuleni ni tabu!
 
Yule mmiliki wa shule ni mbumbumbu sana, na hat ahizo shue kazipat akiujanjaujanja na anaendesha kiujanja ujanja kama kibaraka fulani wa watu fulani.Kila nikipita kuelekea arusha nikiangalia Northern Highlands school pale makaburini natamani kuipiga bomu.Nafikiria moto na possible ways za kuokoa watoto sioni.Jamaa kajenga ghorofa ndefu, ina ngazi nyembamba sana ktk panic wanafunzi hata watatu hawawezi pita.Hana ngazi ya nje kwa vile hakuwahi jiuliza what if moto unaanzia ghorofa za chini "ana helcopter za kuokoa?".Mbaya aliwahi jiua mwanafunzi mmoja, kwa kujitupa ghorofani ,kajamaa kwa ujinga kakatafuta quick fix kwa kuziba kila kitu kote na kuach access pekee kuwa vingazi vidogo na vichache kuserve floors zote.

huw anikiangalia ile shule nanchukia kabisa Pinda, Pinda kahudhuria sana mahafali ya kuhitimu wanafunzi pale na sijui kama issue ya security ili click ktk kichwa yake.

Sikuwa najua kwanini mambo yalikuwa hovyo sana shule za huyu jamaa hadi pale nilipoambiwa kajamaa kalikuwa failure fulani pale mawezi , halafu kaka bebwa na wakubwa zake,kilipopata deal ya shule ndipo kikjiweka ktk maisha kiliyo nayo.

Mara yangu ya kwanza ongea na haka kajamaa nilitaka tapika kalivyokuwa kakijishaua kw akutaja majina ya wakubwa na kuongea nao ktk staili ya wapiga debe wa CCM wakiwa mjini.Ile staili kila laiye karibu hata aisyetaka igilia privacy ya mtu asikie anaongea na nani.

Mkuu hapa kuna mlolongo wa watu wanaopaswa kushtakiwa kwa uhujumu na uhatarashi wa maisha ya watoto! Kuanzia Afisa Ardhi aliyeidhinisha kiwanja, Injinia aliyepisha michoro ya ujenzi, Afisa Elimu/Mkaguzi wa Shule aliyepitisha Uruhusisho wa Shule, Viongozi wa Serikali waliofika kuifungua rasmi na wanahudhuria Mahafali mbali mbali kila mara bila kuchukua hatua, nk, nk Wengine nao waongezee! Nchi hii tuna Sheria, Desturi na Kanuni nzuri sana kwenye maandaishi ila utekelezaji wake unategemea ni kigogo gani anaguswa wapi! Hakika Tanzania tuna Ombwe la Uongozi!
 
Chukua hatua haraka iwezekanavyo, BINAFSI NIMEAPA NA NINAOMBA MUNGU ANISAIDIE,sitokaa nimpeleke mwanangu bording akiwa primary,WATOTO WANATAKIWA WAKAE KARIBU NA WAZAZI WAO KWA KIPINDI CHOTE WAKIWA PRIMARY
 
hebu msigeneralise ati shule za uchagani ni mbaya kiuongozi kama hivo ungemlete kurumenge kweli,, shule za moshi zina hadhi na ndo maana mnaleta watoe wenu hata kama ni wadogo mkiwa na uhakika kwamba watalelewa vizuri nina uhakika apa kuna miss of information, kutoka chuo kwako wewe,, hao watoto huwa hawasafiri wenyewe wanakuja na sister au mlez au mzazi moja mteule kutoka mkoa husika na anahakikisha watoto wanafika kwao salama,

na wewe hivi umekimbia majukumu kumleta mtoto wako unaesema ni mdogo hata ukamleta kwetu mbali huku uchagani,? don compromise ya life style ua job for ya kids wealfare,, make sure ya take primary responsibility toya kid

kwa ufupi pole na tena pole ila usitumie nafasi hii kusema sasa mbona mwanzo hamkusema sasa imetokea hili kila mtu anabwabwaja au ninyi nanyi mna watoto wao, fuatilia kwa ukaribu kama kuna makosa wawajibishe utawala wa shule utasikia ati nina mambo mengi siwezi enda moshi sasa kwani ulivomleta ulidhani umemtoa zaka au,, fuatilia mwanao hakikisha mwanaa anapata malezi bora
 
pole mkuu ndio shida ya wamiliki namba za simu wanazo wanakuwa hawajali
 
Back
Top Bottom