Morrison asimamishwa Yanga kwa utovu wa nidhamu

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Benard Morrison anadaiwa kusimamishwa na Kocha wa klabu hiyo, Nasreddine Nabi kutokana na utovu wa nidhamu.

Taarifa zinadai kuwa mchezaji huyo alipewa adhabu hiyo na wachezaji wengine wawili wa klabu hiyo, Djuma Shaban na Farid Mussa ambao kwa ujumla wamekosekana kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara, kutokana na utovu wa nidhamu.

Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliondolewa kikosini kutokana na kuchelewa kuripoti kambini baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili kwa kikosi cha Yanga baada ya kumaliza mechi ya ligi dhidi ya Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Wakati Farid na Djuma wakirejea kwenye kikosi hicho, inasemekana kuwa Morrison amepelekwa kwenye kamati ya maadili ya klabu hiyo kwa ajili ya utovu wa nidhamu.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo kimeiambia Mwanaspoti, wachezaji hao walishindwa kuripoti kambini siku iliyokuwa imepangwa na siku iliyofuatia waliporudi Kocha Nabi akawatimua.

“Wachezaji hao walizingua na kocha Nabi akawapa adhabu ya kimya kimya, ila tayari wameshaomba radhi na kurejeshwa kikosi na wameingia kambini na wenzao tayari kwa mchezo ujao dhidi ya Prisons,” kimesema chanzo hicho kutoka ndani ya Yanga.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Tupumzisheni kwanza jamani.. 😂😂
Tupo 'KATAA'
 
Mahali salama kwa Morrison ilikua simba tuu na ndipo alifurahia zaidi soka la bongo. Simba wana uvumilivu sana kukaa na watukutu kuanzia kina Hamis Gaga mpaka sasa Mkude.
 
Apewe maji ya Mwamposa ya nini wakati mgunda kasema atamsajili kwenye dirisha dogo? Uto akisema wa nini, kolo ana haha kumsajili.
Hivi Morrison kwa tabia zake angekuwa ni demu anavogombaniwa na simba na yanga nani angekua malaya hapo, ni simba, yanga, au bm.? Manake jamaa anawafanya anavyotaka na wote wanamliliaga, yaani hata kama hatakiwi ukweni (kwa mashabiki) kwa tabia zake mbovu na kukosa adabu na kuwatukana ila bado hao wanaume wawili wanapishana tu kumtaka
 
Apewe maji ya Mwamposa ya nini wakati mgunda kasema atamsajili kwenye dirisha dogo? Uto akisema wa nini, kolo ana haha kumsajili.

Bahati nzuri alifukuzwa huko uto ndo mkaona dhahabu,sasa pambaneni naye mpaka awatoe jasho
 
Na za ndaani kabisa inasemekana yupo kwao Ghana bila hata ruhusa! Mtimueni muone
 
Back
Top Bottom