Jamani hii inaonyesha Wanyarwanda wanafanyaga home work kweli kweli kama walivyo Wakenya, jamaa hawa popote waendapo hawakurupuki i.e wako highly organised at the end of the day they end up na mikataba yenye mshiko kwa Taifa lao na wananchi.
Sasa sijui tatizo letu ni nini?Nafikiri na exposure ina matter sana, sisi tuna kauzubaifu ka aina fulani hivi!
Kitu kingine Serikali sio lazima kuwasikiliza sana washauri wateule, waulize pia wananchi ambao wengi wao wana exposure kubwa kuliko hao washauri na Viongozi wengine, Serikali isijifungie kwenye cacoon na kufikiri raia wa kawaida awawezi kumshauri Rais hata kwa maadishi, Rais Mwinyi alikuwa na kawaida ya kukutana na raia wa kawaida sikumbiki mara ngapi kwa mwezi, I don't think it was chaotic au akijisikia anakwazika hata Baba wa Taifa ingawa alikuwa anacheza nao mchezo wa bao lakini alikuwa anaelezwa kilicho kuwa kinaedela kwenye grassroot na ushauri mwingine wenye mshiko, kama kiongozi hivi si vitu vya kupuuzia hata kidogo.
Watanzania wengi wako talented ndio maana wanakubalika sana nchi za nje kuliko hapa Tanzania, kwa nini Serikali aianzishi dawati la kusikiliza ushauri kutoka kwa raia wa kawaida lakini wenye ujuzi, exposure na taaluma ambazo zinaweza kusaidia sana kuendeleza Taifa letu na wala sio kwamba wanatafuta ajila wala nini sijui!!
Msichukulie Mawaziri, wasaidizi wao na battery ya washauri wachache wa Rais kama ndio alfa na omega, mnasahau Raia walio mpigia kura Dk.Magufuli mnawachukulia si lolote si chochote awawezi kumwambia kitu - hapo ndio mnakosea sana.
Msifikiri labda nia yangu ni kuwasema vibaya current Admin - far from it - hapa tuna sahihishana tukiwa na lengo zuri tu, hapa tunaona Wanyarwanda wameweka list ndefu ya makubaliano kati yao na Mfalme wa Morocco, kila kitu kimeanikwa adhalani - ebu na sisi tuonyeshwe makubaliano kati yetu na Morocco tulinganishe na Wanyarwanda tuone kama sisi kweli tulifanya home work ya kutosha kabla ya kukutana na Mfalme wa Morocco - mke wangu kwa mfano aliwahi kutembelea Morocco kikazi, anasema Taifa hilo limendelea sana katika viwanda vya bidhaa za ngozi bidhaa hizo hata ukiziangalia ni first class kabisa, wanawauzia watalii na Ulaya.
Aliniambia vile vile kwamba Morocco wako mbali sana kwenye nyanja za Real Estate Development pwani pwani na ndani ya nchi, wako mbali sana kwenye ujezi wa viwanda vya sukari na wanavyo vingi nchini mwao - mgemwambia Mfalme mnafikiri angekataa kijenga kiwanda walao kimoja cha sukari nchini kuliko makanjanja wanao tuzuga eti watajenga viwanda vitatu kwa mpigo!
Akamalizia kwa kusema Morocco wako mbali sana katika nyanja za Utalii na viwanda vya kuzalisha bidhaa mbali mbali.
Binafsi naona ziara ya Mfalme wa Morocco ilikuwa ni golden chance kwa Taifa letu kuitumia kupiga hatua nyingine mbele kimaendeleo - swali ni je, fulsa hiyo tuliitumia vizuri?